Wakili Dkt. Rugemeleza Nshala(PhD) aitwa Polisi kutokana na maoni yake kuhusu bandari

Wakili Dkt. Rugemeleza Nshala(PhD) aitwa Polisi kutokana na maoni yake kuhusu bandari

Nguvu yote hii ni kwa ajili ya kunyamazisha watu wasiukatae mkataba ambao hauko sawa tu ama kuna jingine.
Mkataba upi unaouongelea?

Ameitwa kwa DCI akauelezee vizuri huo mkataba mnaoungelea.

Wewe unao? Kwanini huendi kumsaidia kwa DCI?
 
Tuunganishe nguvu tuwe kitu kimoja.

Kwa hapa ni rahisi lakini kiuhalisi ni vigumu kwani kuna chnga moto nyingi hasa kwenu Tangnyika kwani hamuaminiki hasa mkiwekewa kitu kidogo ni rahisi kununuliwa , mfano huyo Slaa anayejifanya hivi sasa kuwa yuko mstari wa mbele kupinga
 
Kama sio Zanzibar na Tanganyika pia basi tuunganishe nguvu pamoja maana kajificha kwenye serikali mbili anaiburuza Zanzibar na Tanganyika.
Hajajificha ni mfumo ndio unaoburuza , yeye aliwekwaa hapo na kwa bahati mbaya au nzuri magufuli amefariki na hiyo nafasi ikabidi aichukuwe yeye
 
Dr, Nashala anatakiwa aende saa tisa alfajiri (asubuhi) kama alivyo ambiwa ktk barua ya wito. Atakuta ofisi ya DCI imefungwa anarudi zake nyumbani kulala.
Hakuna kesi tena alishatii wito.
Yule Kigai hamna kitu pale alishindwa kujua maana PGO ndio ataweza kuandika saa tatu ya kiswahili.
 
Zipo laws of natural justice ambazo sio lazima ziwe coined na katiba yoyote ila kila mmoja mwenye akili timamu anapaswa kufahamu lakini pia tuna tamaduni zetu ambazo ndio msingi na uhai wa taifa letu. Wakili anapayuka sana mpaka kupoteza stara licha ya kujenga hoja zinazoeleweka. Anafoka as if anawafokea watoto wake, mamlaka huwa zinalindwa na kuheshimiwa duniani kote sio busura kwa mtu msomi kama huyo jamaa kutoa kauli zingine kama kejeli, aadhibiwe.
Aliemwita Magufuli dikteta uchwara ile ilikuwa kauli ya staha sana au sio🤣🤣🤣! Matokeo yake mtu akamiminiwa njugu mkaja juu
 
Mkataba upi unaouongelea?

Ameitwa kwa DCI akauelezee vizuri huo mkataba mnaoungelea.

Wewe unao? Kwanini huendi kumsaidia kwa DCI?
Hahahah utateseka sana huu mwaka. Makubaliano yakiwa legally binding ni mkataba tayari.
 
Nchi ya hovyo sana hii. Hivi najiuliza kungekuwa na amshaamsha kama Kenya CCM si wengejinyonga
Wasipoangalia wanaweza sababisha wananchi wakafikia huko maana kwa mwananchi wa kawaida hoi, tozo kupanda kwa bidhaa sokoni, mkulima pembejeo juu na wasomi hawana ajira, baada ya kutafuta njia za kumkomboa ndio wanazidi kudidimiza
 
Kama kichwa cha habari kilivyojieleza,

kwamba serikali iliamua kuibnafisisha bandari ya dar,na nyinginezo nchini kwa kuwa ufanisi ni zero hivyo ikaona haja ya kuleta DPW kuinua ufanisi na mapato ya serikali

Imeelezwa kuna ukwepaji mkubwa wa ulipaji kodi na wizi mkubwa katika bandari zetu


Hii inamaanisha vyombo vya ulinzi na usalama havina msaada kwa taifa,yaani TISS,TAKUKURU,JESHI LA POLISI,MAGEREZA,JWTZ, TRA na vinginevyo ni mdebwedo hasa.


Swali: Vimeshindwaje kudhibiti haya madhira yanayotekea kwenye bandari zetu?, je viapo vyao ni bure kabisa? .ni kweli hivi vyombo vimeshindwa kukomesha uhuni bandarini?,huyu mgeni DPW ndio suluhisho?


Mpaka nchi inaingia mkataba wa kijinga na DPW,, yaani ili DPW akomeshe uhuni huo?, seriously kweli?


Na kama vinatimiza wajibu wake ,mamlaka ndio hazitaki kuchukua hatua visikibali kudhalilika namna hii,na viongozi wake wajiuzulu mara moja na haraka sana
Mkuu mbona unaipa majukumu mapya JWTZ? Jeshi la wananchi na maswala ya ulipaji Kodi na wizi linahusika vipi? Umeongea hayo yote kwa mihemuko ili mradi nawe uwe umechangia au ndipo uwelewa wako ulipoishia?
 
Back
Top Bottom