Wakili Dkt. Rugemeleza Nshala(PhD) aitwa Polisi kutokana na maoni yake kuhusu bandari

Nguvu yote hii ni kwa ajili ya kunyamazisha watu wasiukatae mkataba ambao hauko sawa tu ama kuna jingine.
Mkataba upi unaouongelea?

Ameitwa kwa DCI akauelezee vizuri huo mkataba mnaoungelea.

Wewe unao? Kwanini huendi kumsaidia kwa DCI?
 
Tuunganishe nguvu tuwe kitu kimoja.

Kwa hapa ni rahisi lakini kiuhalisi ni vigumu kwani kuna chnga moto nyingi hasa kwenu Tangnyika kwani hamuaminiki hasa mkiwekewa kitu kidogo ni rahisi kununuliwa , mfano huyo Slaa anayejifanya hivi sasa kuwa yuko mstari wa mbele kupinga
 
Kama sio Zanzibar na Tanganyika pia basi tuunganishe nguvu pamoja maana kajificha kwenye serikali mbili anaiburuza Zanzibar na Tanganyika.
Hajajificha ni mfumo ndio unaoburuza , yeye aliwekwaa hapo na kwa bahati mbaya au nzuri magufuli amefariki na hiyo nafasi ikabidi aichukuwe yeye
 
Dr, Nashala anatakiwa aende saa tisa alfajiri (asubuhi) kama alivyo ambiwa ktk barua ya wito. Atakuta ofisi ya DCI imefungwa anarudi zake nyumbani kulala.
Hakuna kesi tena alishatii wito.
Yule Kigai hamna kitu pale alishindwa kujua maana PGO ndio ataweza kuandika saa tatu ya kiswahili.
 
Aliemwita Magufuli dikteta uchwara ile ilikuwa kauli ya staha sana au sio🤣🤣🤣! Matokeo yake mtu akamiminiwa njugu mkaja juu
 
Mkataba upi unaouongelea?

Ameitwa kwa DCI akauelezee vizuri huo mkataba mnaoungelea.

Wewe unao? Kwanini huendi kumsaidia kwa DCI?
Hahahah utateseka sana huu mwaka. Makubaliano yakiwa legally binding ni mkataba tayari.
 
Nchi ya hovyo sana hii. Hivi najiuliza kungekuwa na amshaamsha kama Kenya CCM si wengejinyonga
Wasipoangalia wanaweza sababisha wananchi wakafikia huko maana kwa mwananchi wa kawaida hoi, tozo kupanda kwa bidhaa sokoni, mkulima pembejeo juu na wasomi hawana ajira, baada ya kutafuta njia za kumkomboa ndio wanazidi kudidimiza
 
Mkuu mbona unaipa majukumu mapya JWTZ? Jeshi la wananchi na maswala ya ulipaji Kodi na wizi linahusika vipi? Umeongea hayo yote kwa mihemuko ili mradi nawe uwe umechangia au ndipo uwelewa wako ulipoishia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…