Wakili Ishabakaki: Idris Sultan anahojiwa kwa kuicheka picha ya Rais

Wakili Ishabakaki: Idris Sultan anahojiwa kwa kuicheka picha ya Rais

Ipo clip iddy anacheka mpk chozi Linamtoka
Mpaka anataka kuanguka kwa kucheko
Nahs Hali Ile imeonesha kama Ana mdhiaki rais
Na kwa. Kitendo kile lazima apate dhoruba
Na akitoka sijui kama atarudia

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
Mungu mwenyewe siku zote anachekwa, anadhihakiwa na mambo chungu nzima!

Lakini unaandika hapa: "Akitoka sijui kama atarudia." Sijui kutoa onyo?

Hawa miungu mnaowatengeneza watayazuia hayo?
 
Nimeangalia ile sio commedy, alilenga kumdhalilisha Mkuu wa Nchi lazima achunguzwe huwenda kuna mtu anamtumia nyuma ya pazia
Hii habari ya "kumdhalilisha Mkuu wa Nchi" ni habari za Ujima tu.

Nchi zilizoendelea kama Marekani na Uingereza, rais Donald Trump, Malkia Elizabeth, Waziri Mkuu Johnson wanakuwa caricatured kila siku, na hakuna mtu anayefungwa kwa hilo.

Ni ushamba fulani unaochangia tuwe masikini.

Tunaheshimu sana watu fulani kuliko hata mifumo na uhuru.

Yani comedian kufanya comedy kwa rais ishakuwa shida?

Ushawahi kuona kipindi kinaitwa "Saturday Night Live" ?
 
Kule Afrika Kusini mama wa kikaburu alishtakiwa kwa kuwafundisha mbwa wake kubweka kila wakiona picha ya Jacob Zuma kwenye runinga aliyekuwa raisi wa SA,pamoja na yote waafrika tuna utamaduni wetu,tuwaheshimu watu waliotuzidi umri,pia nadhani tunakumbuka kwenye biblia Nuhu alipolewa akapitiwa na usingizi na kuacha mwili wake utupu ,mwanae mpumbavu alipomuona akaanza kumcheka, lakini akaja mtoto mwingine mwenye busara akaja kinyumenyume akamfunika nguo baba yake mzee Nuhu, hatima ya aliyemcheka baba yake kwa kuwa tupu akaachiwa laana na uzao wake wote.Tujitafakari huyu kijana angekuwa baba yake angemcheka na kumfanya kichekesho,na huyo Halima yeye anayoyafanya pamoja na kuwa ya hovyo mbona hachekwi?heshimu wakubwa uongeze siku zako za kuishi.
 
Bado sioni kosa la "kuwekwa rumande bila dhamana" kwenye hali hiyo uliyoielezea hapo; na bado nakushangaa kabisa umepatwa na mkasa gani kuyashangilia haya.

Kimsingi Idriss hajafanya kosa la kuweza kushikiliwa acha tu kunyimwa haki yake ya msingi ya dhamana...
Ninachosema mimi haikuwa sawa yeye kufanya vile hasa kwa utawala huu tulionao sasa. Sio mara ya kwanza Idriss kushikiliwa kwa kujaribu kumhusisha Rais katika masuala yake ya comedy, sasa kwa akili ya kawaida tu, kwanini arudie kufanya yaleyale ambayo ni wazi mhusika hapendezwi nayo?
Ninachokiona hapa ni kiherehere cha kujizolea sifa za kwenye mitandao kinachomponza Idriss.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hivi huwa wanapekua nini nyumbani kwa mtuhumiwa? Mpaka kesi za mitandao wanafanya upekuzi, huwa wanataka kupata nini? Wajuzi mtuelimishe
 
Kwan
Wewe hujui kitu unaropoka. Wakili alishaongea kuwa ni shitaka la kumdhalilisha rais. Wewe una bisha kitu gani? Uwe na uhakika wa unachosema kabla hujaandika utumbo wako hapa. Hata kama umetumwa na Polepole basi uwe unatumia akili kiidogo.

Kwani wakili ndo nani? Pole nadhani umesoma umeelewa nilichoandika. Kama maandishi uyaoni uzuri unaona utumbo badala ya maneno. Tafadhali muone daktari wa macho.
 
Kwahyo ukimtukana Rais unakuwa Tajiri?
Hii habari ya "kumdhalilisha Mkuu wa Nchi" ni habari za Ujima tu.

Nchi zilizoendelea kama Marekani na Uingereza, rais Donald Trump, Malkia Elizabeth, Waziri Mkuu Johnson wanakuwa caricatured kila siku, na hakuna mtu anayefungwa kwa hilo.

Ni ushamba fulani unaochangia tuwe masikini.

Tunaheshimu sana watu fulani kuliko hata mifumo na uhuru.

Yani comedian kufanya comedy kwa rais ishakuwa shida?

Ushawahi kuona kipindi kinaitwa "Saturday Night Live" ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mchekeshaji Idriss Sultan wa Tanzania anashikiliwa na polisi tangu Jumanne wiki hii.

Wakili wa mchekeshaji maarufu nchini Tanzania Idriss Sultan ameiambia BBC kuwa msanii huyo anahojiwa na polisi juu ya 'kuicheka picha ya Rais John Pombe Magufuli'.

Kwa mujibu wa wakili Benedict Ishabakaki, japo bwana Sultan hajafunguliwa mashtaka rasmi na polisi, maswali anayohojiwa kufikia sasa yanahusiana na mkanda wa video aliotuma mitandaoni hivi karibuni akionekana akiicheka picha ya zamani ya rais Magufuli.

"Hawajamwambia mpaka sasa kama amevunja kifungu chochote cha sheria...lakini mwenendo wao wa maswali ni kuhusiana na ile video," wakili Ishabakaki ameiambia BBC.

Bw Sultan anashikiliwa na polisi toka Jumanne mchana punde tu alipoitikia wito wa kuripoti kituo cha polisi na mpaka sasa bado hajapatiwa dhamana wala kupandishwa kizimbani.

Wakili wake pia ameiambia BBC kuwa Jumatano jioni polisi walienda kufanya upekuzi nyumbani kwa mteja wake.
"Tunataraji anaweza kuachiwa kwa dhamana hii leo...masharti tuliyopewa ni awe na wadhamini wawili wanaotambuliwa na serikali ya mtaa," amesema wakili Ishabakaki.

Kumekuwa na kampeni katika mitandao ya kijamii nchini Tanzania ambapo watu kadhaa wakiwemo wanasiasa wa upinzani wa wanaharakati wanatuma ujumbe wa kutaka msanii huyo kuachiwa huru.

Kampeni hiyo inaendeshwa kwa kutumia anuani maalumu ya mtandao ya #FreeIdrisSultan.

Kwa hapa tulipokuwa tumefikia, hii nchi hatujazowea hii kamatakamata kwa mambo ya kipuuzi tu kama haya. Huku tulikuwa tumevuka. Lakini nchi imeshikwa na vichaa. Hata mzaha na ucheshi ni kosa? Rais alichaguliwa na nani huyu? Mbona kageuka mungu wa nchi?

Najua kuna muda na yeye atarudi kuwa raia wa kawaida. Na anaowatuma nao watabaki hapahapa Tanzania. Siku kikombe kikijaa, hawa watu watakinywa!

Upumbavu. Ushamba. Ushenzi mtupu...

FREE our innocent comedians.
 
Kwahyo ukimtukana Rais unakuwa Tajiri?

Sent using Jamii Forums mobile app
Jamii zenye maendeleo ya kiuchumi (mfano Marekani na Uingereza) ni jamii zilizojengwa katika misingi ya uhuru wa watu kujieleza na kuishi bila hofu, kiasi kwamba watu wanamkejeli na kumtukana rais au Malkia bila woga.

Si kwamba ukimtukana rais unakuwa tajiri.

Hicho ni kipimo tu cha level ya tolerance for free speech and free thought iliyo katika jamii.

Jamii zenye free speech na freedom of thought, zina misingi ya maendeleo makubwa ya kiuchumi kuliko jamii zinazobana watu wake hata kumkejeli rais.

Kwa maelezo zaidi kwenye habari hizi, kama hujasoma, tafuta kitabu kinaitwa "Why Nations Fail: The Origins of Power, Prosperity, and Poverty" by Armenian-American economist Daron Acemoglu from the Massachusetts Institute of Technology and British political scientist James A. Robinson from the University of Chicago.

Nchi inayokataza rais kukejeliwa, ina uwezo mkubwa wa kuminya watu wenye mawazo mazuri wanaotofautiana na rais kumshauri rais afanye hayo mambo mazuri.

Kwa sababu, huyo rais kafanywa kuwa Mungu mtu, hawezi hata kudhihakiwa.

Si mtu tena!
 
Acheni siasa, ile ni dhihaka na sio vinginevyo. Tupingane na Rais katika mambo ya msingi ila sio kumdhihaki.

Sent from my iPhone using JamiiForums
Imagine ingekuwa mzazi wako anadhihakiwa kwa jinsi hiyo. Sometimes tunakosa kuwa na values sijui ni malezi au? Yet bado watu hawaoni kama ni kosa lile, iko wapi value kwenye jamii yetu? Respect is earned, kama huwezi heshimu hata mamlaka utamheshimu nani? Vijana wanapotoka sana...Mh. amsamehe tu kwakua ni mzazi
 
Jamii zenye maendeleo ya kiuchumi (mfano Marekani na Uingereza) ni jamii zilizojengwa katika misingi ya uhuru wa watu kujieleza na kuishi bila hofu, kiasi kwamba watu wanamkejeli na kumtukana rais au Malkia bila woga.

Si kwamba ukimtukana rais unakuwa tajiri.

Hicho ni kipimo tu cha level ya tolerance for free speech and free thought iliyo katika jamii.

Jamii zenye free speech na freedom of thought, zina misingi ya maendeleo makubwa ya kiuchumi kuliko jamii zinazobana watu wake hata kumkejeli rais.

Kwa maelezo zaidi kwenye habari hizi, kama hujasoma, tafuta kitabu kinaitwa "Why Nations Fail: The Origins of Power, Prosperity, and Poverty" by Armenian-American economist Daron Acemoglu from the Massachusetts Institute of Technology and British political scientist James A. Robinson from the University of Chicago.

Nchi inayokataza rais kukejeliwa, ina uwezo mkubwa wa kuminya watu wenye mawazo mazuri wanaotofautiana na rais kumshauri rais afanye hayo mambo mazuri.

Kwa sababu, huyo rais kafanywa kuwa Mungu mtu, hawezi hata kudhihakiwa.

Si mtu tena!
I tend to differ. America ina values zake. Leta na sisi vitabu vya culture yetu uone kama utakuta kejeli kama hizi. Hii pia inaonyesha kiwango cha utegemezi wa fikra. Africa ina value zake kama kuheshimu wakubwa na kuna sababu za msingi tu pengine ndiyo maana zile ancient empires kama Mali zilikuwa na maendeleo makubwa enzi hizo. Pengine dunia Inge evolve kuwa ya kistaarabu zaidi kama African values ndizo zingeiongoza maendeleo na ustaarabu wa dunia; lakini kwakua hatupendi kufikiri nje ya box, kila tulichowekewa kwenye box na weupe ndicho tunachokiona kinafaa pamoja na kuwa hakina mbadala.

Itoshe kusema China inatuonyesha kuwa kuna mbadala wa fikira ambazo zinaweza kuwa bora kuliko hivi ambavyo tumezoea kulishwa pasipo kutathmini.
 
Sheria ya nchi gani inasema mkubwa hachekwi
Nikumbushe kifungu tafadhali

Vipi wale wanaomchora na komwe kwenye magazeti nao wakamatwe kwa kumdhihaki malaika?
Kusema kweli inachekesha lakini si unajua tena mkubwa hachekwi? Wengine tulicheka kimyakimya yakaisha, ila yeye kiherehere ndio kinamponza.

Sent from my iPhone using JamiiForums

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom