Nifah
JF-Expert Member
- Feb 12, 2014
- 34,020
- 79,098
Sijaona picha yoyote;lakini nashangaa sana hata wewe kuandika uliyoandika hapa.
Ameitemea mate, ameivunjavunja ama kuipaka matope na kuiharibu?
Kuna sheria yoyote inayozuia mtu kucheka? Na kama amecheka kwa kufurahia kuiona picha hiyo, ni kosa?
Halafu mkuu 'Nifah', unashangila kabisa mtu kuwekwa rumande, siku kadhaa, kweli huoni kasoro yoyote hapo?
Ndio, hata mimi sipendezwi rais au hata picha yake idhihakiwe. Kama kahisiwa kufanya kosa/kuvunja sheria, kumweka rumande kama adhabu yake ni kosa pia. Haya ndio tunayotakiwa kuyakataa.
"Dhihaka" ni kufanya nini?
Tunakwenda taratibu sana, lakini najua siku moja tutafika mahali na kushangaa watu walikuwa wanawekwa rumande kwa sababu za "kucheka"?
Yote uliyoyasema hapa hayana maana kama tu hujaiona picha, in fact alichokifanya Idriss ni kuunganisha picha ya Rais pamoja na video yake akiwa anacheka, niliiona punde tu alipoiweka kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Nakushauri utafute kwanza hiyo video ndipo tuuanze mjadala.
Sent from my iPhone using JamiiForums