KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Mungu mwenyewe siku zote anachekwa, anadhihakiwa na mambo chungu nzima!Ipo clip iddy anacheka mpk chozi Linamtoka
Mpaka anataka kuanguka kwa kucheko
Nahs Hali Ile imeonesha kama Ana mdhiaki rais
Na kwa. Kitendo kile lazima apate dhoruba
Na akitoka sijui kama atarudia
Ova
Sent using Jamii Forums mobile app
Hii habari ya "kumdhalilisha Mkuu wa Nchi" ni habari za Ujima tu.Nimeangalia ile sio commedy, alilenga kumdhalilisha Mkuu wa Nchi lazima achunguzwe huwenda kuna mtu anamtumia nyuma ya pazia
Bado sioni kosa la "kuwekwa rumande bila dhamana" kwenye hali hiyo uliyoielezea hapo; na bado nakushangaa kabisa umepatwa na mkasa gani kuyashangilia haya.
Seriously! Yaani ni kosa kumcheka Rais? Tena picha ya mtu aliekuja kuwa Rais!!! Seriously?
AiseKwa nini asimcheke Baba ake Mzazi?
Mi Naona tu Idris anyongwe kwa kweli he is too much
Sent from my iPhone using JamiiForums
I ddnt see this long shit coming
Wewe hujui kitu unaropoka. Wakili alishaongea kuwa ni shitaka la kumdhalilisha rais. Wewe una bisha kitu gani? Uwe na uhakika wa unachosema kabla hujaandika utumbo wako hapa. Hata kama umetumwa na Polepole basi uwe unatumia akili kiidogo.
Hii habari ya "kumdhalilisha Mkuu wa Nchi" ni habari za Ujima tu.
Nchi zilizoendelea kama Marekani na Uingereza, rais Donald Trump, Malkia Elizabeth, Waziri Mkuu Johnson wanakuwa caricatured kila siku, na hakuna mtu anayefungwa kwa hilo.
Ni ushamba fulani unaochangia tuwe masikini.
Tunaheshimu sana watu fulani kuliko hata mifumo na uhuru.
Yani comedian kufanya comedy kwa rais ishakuwa shida?
Ushawahi kuona kipindi kinaitwa "Saturday Night Live" ?
Mchekeshaji Idriss Sultan wa Tanzania anashikiliwa na polisi tangu Jumanne wiki hii.
Wakili wa mchekeshaji maarufu nchini Tanzania Idriss Sultan ameiambia BBC kuwa msanii huyo anahojiwa na polisi juu ya 'kuicheka picha ya Rais John Pombe Magufuli'.
Kwa mujibu wa wakili Benedict Ishabakaki, japo bwana Sultan hajafunguliwa mashtaka rasmi na polisi, maswali anayohojiwa kufikia sasa yanahusiana na mkanda wa video aliotuma mitandaoni hivi karibuni akionekana akiicheka picha ya zamani ya rais Magufuli.
"Hawajamwambia mpaka sasa kama amevunja kifungu chochote cha sheria...lakini mwenendo wao wa maswali ni kuhusiana na ile video," wakili Ishabakaki ameiambia BBC.
Bw Sultan anashikiliwa na polisi toka Jumanne mchana punde tu alipoitikia wito wa kuripoti kituo cha polisi na mpaka sasa bado hajapatiwa dhamana wala kupandishwa kizimbani.
Wakili wake pia ameiambia BBC kuwa Jumatano jioni polisi walienda kufanya upekuzi nyumbani kwa mteja wake.
"Tunataraji anaweza kuachiwa kwa dhamana hii leo...masharti tuliyopewa ni awe na wadhamini wawili wanaotambuliwa na serikali ya mtaa," amesema wakili Ishabakaki.
Kumekuwa na kampeni katika mitandao ya kijamii nchini Tanzania ambapo watu kadhaa wakiwemo wanasiasa wa upinzani wa wanaharakati wanatuma ujumbe wa kutaka msanii huyo kuachiwa huru.
Kampeni hiyo inaendeshwa kwa kutumia anuani maalumu ya mtandao ya #FreeIdrisSultan.
Jamii zenye maendeleo ya kiuchumi (mfano Marekani na Uingereza) ni jamii zilizojengwa katika misingi ya uhuru wa watu kujieleza na kuishi bila hofu, kiasi kwamba watu wanamkejeli na kumtukana rais au Malkia bila woga.
Huyo kijana wamwache akae huko ajifunze
Imagine ingekuwa mzazi wako anadhihakiwa kwa jinsi hiyo. Sometimes tunakosa kuwa na values sijui ni malezi au? Yet bado watu hawaoni kama ni kosa lile, iko wapi value kwenye jamii yetu? Respect is earned, kama huwezi heshimu hata mamlaka utamheshimu nani? Vijana wanapotoka sana...Mh. amsamehe tu kwakua ni mzaziAcheni siasa, ile ni dhihaka na sio vinginevyo. Tupingane na Rais katika mambo ya msingi ila sio kumdhihaki.
Sent from my iPhone using JamiiForums
I tend to differ. America ina values zake. Leta na sisi vitabu vya culture yetu uone kama utakuta kejeli kama hizi. Hii pia inaonyesha kiwango cha utegemezi wa fikra. Africa ina value zake kama kuheshimu wakubwa na kuna sababu za msingi tu pengine ndiyo maana zile ancient empires kama Mali zilikuwa na maendeleo makubwa enzi hizo. Pengine dunia Inge evolve kuwa ya kistaarabu zaidi kama African values ndizo zingeiongoza maendeleo na ustaarabu wa dunia; lakini kwakua hatupendi kufikiri nje ya box, kila tulichowekewa kwenye box na weupe ndicho tunachokiona kinafaa pamoja na kuwa hakina mbadala.Jamii zenye maendeleo ya kiuchumi (mfano Marekani na Uingereza) ni jamii zilizojengwa katika misingi ya uhuru wa watu kujieleza na kuishi bila hofu, kiasi kwamba watu wanamkejeli na kumtukana rais au Malkia bila woga.
Si kwamba ukimtukana rais unakuwa tajiri.
Hicho ni kipimo tu cha level ya tolerance for free speech and free thought iliyo katika jamii.
Jamii zenye free speech na freedom of thought, zina misingi ya maendeleo makubwa ya kiuchumi kuliko jamii zinazobana watu wake hata kumkejeli rais.
Kwa maelezo zaidi kwenye habari hizi, kama hujasoma, tafuta kitabu kinaitwa "Why Nations Fail: The Origins of Power, Prosperity, and Poverty" by Armenian-American economist Daron Acemoglu from the Massachusetts Institute of Technology and British political scientist James A. Robinson from the University of Chicago.
Nchi inayokataza rais kukejeliwa, ina uwezo mkubwa wa kuminya watu wenye mawazo mazuri wanaotofautiana na rais kumshauri rais afanye hayo mambo mazuri.
Kwa sababu, huyo rais kafanywa kuwa Mungu mtu, hawezi hata kudhihakiwa.
Si mtu tena!
Kusema kweli inachekesha lakini si unajua tena mkubwa hachekwi? Wengine tulicheka kimyakimya yakaisha, ila yeye kiherehere ndio kinamponza.
Sent from my iPhone using JamiiForums
Huyo kijana wamwache akae huko ajifunze