Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Yule ameajiriwa. Kwani Yanga mtu hatakiwi kujiuzulu? Kalipa mishahara mitatu ya notisi, Kalipa hela alopewa kama manunuzi. Hataki kuchezea yanga. Uzuri yanga imekiri kwamba kaandika barua. Ulitaka afanyeje?Issue sio kuvunja mkataba, swala ni utaratibu wa kuvunja watu wana twist story mimi mwanzo nlikua upande wa Feisal ila nmefatilia nmegundua kuna sehemu haipo sawa
Iyo sheria ya FIFA ni kifungu gani kinachosema mpaka msimu uishe?huu ni msimu wa dirisha dogo TFF washatangaza timu zisajili.Utaratibu wa kuvunja mkataba haupo upande mmoja pia sheria za FIFA zinaruhusu kuvunja msimu ukiwa umeisha sio kati kati ya msimu hii kitu wasipo kaa kuongea Feisal hatacheza mpaka mwisho wa msimu
Wakishindwa hii wanaenda kumroga. AjipangeUto ukiachwa achika
Ikaja nne. EndeleaAwali ilikuwa point 8
Kwenye mkataba wa Yanga na fei toto. Yanga wameweka release clause ambayo inamtaka mchezaji kurudisha signing fee na mshahara wa miezi mitatuKwanza anapaswa aelewe kuwa Neymar hakuwalipa Barca gharama za pesa walizomsaini bali aliwalipa Barca pesa kulingana na thamani waliyomuwekea endapo kama kuna klabu itamuhitaji(release clause/buyout clause)
Any contract should have consideration. Sasa ukisema awarudishie halafu wataje tena hela yao huoni kama inakuwa siyo sahihiShwaini wengi wanajua pesa aliyorudisha fei ni yake kumbe ni kama anawarudishia Yanga pesa yao (signing fee),Yanga wakiridhia kupokea ile pesa basi itabidi wataje pesa yao kukubali kuvunja mkataba,kama ilivyo kwa wachezaji na makocha tunavyosikiaga fifa imewataka iwalipe kwa kuvunjiwa mikataba na ni hivyo kwa wachezaji,fei akae chini na Yanga wamtajie kiasi wanachotaka awalipe asepe sio aamke tu asubuhi akadeposit pesa kwenye acc ya Yanga eti ndio kavunja mkataba!
Ukoo wa Toto waganga!!!Wakishindwa hii wanaenda kumroga. Ajipange
Wewe una uhakika?Mwenye uhakika Fisal mwenyewe wengine ni ramli chonganishi.Ndio maana nimeanza inawezekana.Labda wewe ni mgeni Bongo.Kwanini unaongea vitu huna uhakika,?
Huyu jamaa anaonekana ni mweupe kabisa kichwan, yeye hajui Kama mchezaji anaweza kuvunja mkataba na timu yake akawa huru?? Then akatafuta timu yeye akiwa mchezaji huru?Kweli huijui sheria, na hata vipengele vya kisheria kwenye mikataba huvijui pia maana yake.
Hapo suala sio lazima mpaka viongozi wa Yanga SC wakae na Azam ndio waongee biashara, muhimu ni kama umeweka kipengele kwenye mkataba wa mchezaji wako kinachomruhusu kuondoka aki deposit kiasi fulani cha pesa, basi hapo umejibana mwenyewe.
Mchezaji ataondoka wakati wowote akiamua, muhimu aweke pesa mliyotaka kwenye akaunti yenu, hapa suala la Yanga SC kuongea na Azam linakuwa halina maana tena, halipo, kwasababu mchezaji ameshavunja mkataba na Yanga SC kwa kuweka mzigo kwenye akaunti, huyu sasa ni sawa na mchezaji huru.
Leo zitabaki 3Ikaja nne. Endelea
Basi na aende huko Azam fcFeisal yuko sahihi kwa 100% kisheria.
Ameamua kuvunja mkataba na Yanga kwa kulipa gharama yote inayotamkwa na mkataba wake. Hakuna tena suala la kukaa mezani, kukubaliana au kupatana. Mkataba wa Feisal imetamka yote na wote umefuatwa. Feisal kwa sasa ni mchezaji huru, ana uhuru wote wa kwenda klabu yoyote hata bure. Na Yanga kwa sasa hawahusiki chochote na Feisal.
Dejan akidai Simba Kuna vipengele wamekiukaBro ayo ni maoni yako, lakini kwani huonagi wachezaji wengi wakivunja mkataba na timu zao na kubaki wachezaji huru. Klabu inabidi iwe na ustadi wa kumbana mchezaji kwa kutokumpa uwezo wa kuuvunja mkataba kitu ambacho yanga wameshindwa kufanya. Mbona Dejan kavunja mkataba na simba akawa free agent saiv yuko tim nyngne. Ndomana yanga wanaitwa utopolo, hawana hata ustadi wa kutengeneza vizuri mikataba. Lakini shida hio sio kwa yanga tu hata tim nyngne bongo. Shida ni Elimuu!!!
Azam atapigwa mtamuhurumia leoLeo zitabaki 3
SawasawaKweli huijui sheria, na hata vipengele vya kisheria kwenye mikataba huvijui pia maana yake.
Hapo suala sio lazima mpaka viongozi wa Yanga SC wakae na Azam ndio waongee biashara, muhimu ni kama umeweka kipengele kwenye mkataba wa mchezaji wako kinachomruhusu kuondoka aki deposit kiasi fulani cha pesa, basi hapo umejibana mwenyewe.
Mchezaji ataondoka wakati wowote akiamua, muhimu aweke pesa mliyotaka kwenye akaunti yenu, hapa suala la Yanga SC kuongea na Azam linakuwa halina maana tena, halipo, kwasababu mchezaji ameshavunja mkataba na Yanga SC kwa kuweka mzigo kwenye akaunti, huyu sasa ni sawa na mchezaji huru.
Kiungo punda mzamiru anakula ngapi!?Yaani 12 ni mishahara mitatu. Wakati kuna watu wako bench huo ni mshahara mmoja. Daaa inasikitisha