Wakili Mwabukusi, Emmanuel Masonga na Mdude Nyagali wakamatwa na Polisi Mikumi wakiwa safarini kuelekea Dar es Salaam

Wakili Mwabukusi, Emmanuel Masonga na Mdude Nyagali wakamatwa na Polisi Mikumi wakiwa safarini kuelekea Dar es Salaam

CDM acheni uchochezi jmn - kwa nn mnakuwa hivyo jmn!!!!
Serikali ya CCM ina ustarabu sana ndiyo maana mnadeka sana
 
Miye nawalaumu tuu kujipakiza gari moja, hapo mwingine angekwea mwewe, mwingine treni, na mwingine angepanda basi hadi iringa akatokea Dodoma zen akarudi Dar. Umafya umafya tuu maisha kuwindani km nyati na simba porini.
 
Hii ndio Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi hilo , Kamanda Misiime , Shukrani nyingi sana kwa Wananchi kwa kupaza sauti kuu , maana mngenyamaza watu hawa wangeweza kupotea kama Ben Saanane .

Kamanda Misiime amedai kwamba , watu hao wamekamatwa kwa tuhuma za Uchochezi , na kwamba kuna watu wengine bado wanasakwa ili waunganishwe nao.

======
Bali kwa Tafsiri ya wananchi , wanaoitwa wachochezi ni wale wote wanaopinga Mkataba duni wa kudhalilisha wa milele wa Bandari za Tanganyika tu (siyo za Zanzibar) na DP WORLD ya Waarabu wa Dubai , kwahiyo tunatarajia watu wengi zaidi kukamatwa kwa tuhuma hizi , wakiwemo wanasiasa , wanaharakati na Viongozi wa dini wanaopinga uwekezaji huu wa kitumwa .

Lengo la yote haya ni kuwatisha wananchi ili wamuachie Mwarabu Bandari zetu .

Je lengo hili litafanikiwa ?
Samia anafanya kitu kibaya sana tena sana. Muda ni mwalimu mzuri!
 
Polisi wana taarifa za kiintelijensia na bado mtatafutwa wote mpaka mpatikane si umemsikia kamanda wa polisi katika press. Hao wakina Mwambuzi na mdude wanatumwa tu serikali inataka wale waliojificha nyuma yao.
Hilo jeshi la polisi analogia linalosubiri kutumwa na viongozi CCM wana intelligence gani? Hilo jeshi bado sana, wao hutumia nguvu tu na akili kidogo sana.
 
Muda mnaotumia kuwapigania ambao hawajawatuma mngetumia kwa mambo yenu, ndo yale yale ya unakufa unaacha watoto wanateseka kisa siasa
Kwani hao wanaokufa kwenye ajali huwa watoto wao wanaishi kwa raha? Je umewahi kuona watu wanaacha kusafiri kisa wanaweza kupata ajali? Kufa ni lazima, kuishi majaliwa boss. Hivyo acha kufundisha wanaume uoga.
 
Tunaishi kwa aman sasa akitokea panya mmoja na kutaka kuhalibu aman azibitiwe tafadhali
🤣 Amani kweli ipo mkuu, ila sidhani kama watu wanafurahishwa na hii Amani ya wezi na mafisadi kula bila kusaza ilihali wananchi wanapuuzwa na kuteswa na umaskini uliokithiri.
 
Hii ndio Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi hilo , Kamanda Misiime , Shukrani nyingi sana kwa Wananchi kwa kupaza sauti kuu , maana mngenyamaza watu hawa wangeweza kupotea kama Ben Saanane .

Kamanda Misiime amedai kwamba , watu hao wamekamatwa kwa tuhuma za Uchochezi , na kwamba kuna watu wengine bado wanasakwa ili waunganishwe nao.

======
Bali kwa Tafsiri ya wananchi , wanaoitwa wachochezi ni wale wote wanaopinga Mkataba duni wa kudhalilisha wa milele wa Bandari za Tanganyika tu (siyo za Zanzibar) na DP WORLD ya Waarabu wa Dubai , kwahiyo tunatarajia watu wengi zaidi kukamatwa kwa tuhuma hizi , wakiwemo wanasiasa , wanaharakati na Viongozi wa dini wanaopinga uwekezaji huu wa kitumwa .

Lengo la yote haya ni kuwatisha wananchi ili wamuachie Mwarabu Bandari zetu .

Je lengo hili litafanikiwa ?
Dah!!

Hata mkoloni hakuwa na upumbavu kiasi hiki aisee..
 
Back
Top Bottom