Wakili Mwabukusi: Wapinzani hawana afadhali yoyote na CCM, ni wabaya kuliko hata CCM

Hapana. Lazima vyama vya upinzani viingie kwenye uchaguzi ili kupata nguvu ya kupambana na chama tawala. Mawazo na msimamo wa adv. Mwabukusi ni sahihi, lakini, si sahihi sana kwa wakati huu. Mapambano katika uwanja ya vita lazima kubadili mbinu za medani mara kwa mara kutokana na wakati na mazingira.
Nashauri vyama vya upinzani, ... Njoo vijijini kama Chadema walivyofanya huko kanda ya ziwa, Rukwa na kwingineko. Waelimisheni Watanzania juu ya hali yao na wanavyostahili kuwa. Wataelewa. Na baada ya hapo ingieni kwenye uchaguzi huku mkiimarisha usimamizi wa zoezi au mchakato mzima wa kura. Nendeni wilayani Nkasi mkajifunze Wananchi walifanyaje hadi Serikali na Chama tawala wakasalimu amri mwaka 2020 hata mwanamke, tena binti mdogo tuu Aidah Kenani akamgaragaza kwa aibu aliyekuwa mbunge machachari na maarufu Ally Kessy Mohamed. Inawezekana.
Kimsingi, Wananchi walikwishaichoka CCM na Serikali yake. Wanataka mabadiliko. Lakini, ni nani atakayewaongoza kuleta mabadiliko hayo? Ni Chama gani? Hawa hawa wachumia-tumbo Chadema, ACT, TLP, and the like?!
Anyway, vyama vya upinzani hamjachelewa bado, ingieni vijijini, "mwageni sumu" kwa Wananchi; wataelewa na kukisubiri CCM kwenye sanduku la kura.
Mwabheja sana!
 
Hivi hao 19 wamejipeleka hapo bungeni.

Mwabukusi anaendesha gari kwa gia ya reverse bila shaka atatumbukia mtaroni au kupata ajali ya kujitakia.
 
Ndio!!
CCM ni chama cha kihistoria tena historia iliyotukuka...

Na hata Chadema mnayo Historia inawayowatambulisha vizuri sana katika Jamii,
Mathalani kuwa na Mwenyekiti wa chama wa Maisha.

Lakini pia mna historia ya kutukana mno na mihemko kwa sana tu,

Mna historia ya sususia mambo mbalimbali kama vile chaguzi, baadhi ya mitandao ya simu na kadhalika, vitu ambavyo havijawahi kuwasaidia chochote Zaidi ya kuwaharibu na kudidimiza Zaidi.

Na kwasasa Chadema imevamiwa mathalani na mtu kama wewe, kutwa uchwao kulalamamika na kulaumu mara dipi weldi, mara tume ya uchaguzi, mara katiba mpya vitu ambavyo viko kwenye mipango na rada za serikli na itashughulika navyo kwa wakati wake kadiri itakavyona inafaa.

Nje ya hapo no consultation, no mobilization and engagements na wanachama uchaguzi unafika unashindwa then unakuja tena kulalamika unadai kuibiwa 😜

My friend,
Politics is science
Ukija kichwa kichwa unaliwa kichwa vizuri tu na kulaumu mpaka siku ya Mwisho....
 
Mwabukusi ana hoja ni vyema asikilizwe.
 
Si akaanzishe chama chake
 
Anaongea ukweli
 

Anataka Nini?. Mbona haishiriki chaguzi zozote?. Mwisho wa siku ataichukua kadi ya CCM maana janja yake imejulikana.
 
Namshauri aanzishe chama chake kuliko kila siku kulaumu wapinzani hasa akiilenga Chadema. Kama wapinzani wote wakisusia uchaguzi maana yake automatically nchi itakuwa imerudi kuwa ya chama kimoja na vyama vyote vitakosa kabisa platform ya kufanyia siasa na hili ndilo lengo la CCM. Heri kenda shika kuliko kumi nenda uje.
 
Kwa majira haya Lissu hakupaswa kuwa CHADEMA
Mbowe hana nia ya dhati kwasasa kuinua upinzani.

Bora hata Lema alimchana kuwa asiwaamini ccm
Vyama vya Upinzani vilivyosajiliwa vipo 19 kama sijakosea, WHY Chadema????

Ninachokiona hapa yeye (Mwabukusi) ndiye mwenye tamaa. Mnapokuwa vitani kwanini uanze kuwashambulia wenzako badala ya adui?? Yeye (Mwabukusi) ndiye anaetumiwa na wapenda madaraka wa CCM kuwashambulia Wapizani.

Chama Makini kama Chadema hakiwezi kuweka rehani maisha ya Watz kisa madaraka. Siku ikiwadia Watz wakaamua wenyewe kuyaweka maisha yao rehani kwa Ukombozi wa Nchi Yao sawa, hapo Chadema watakuwa tayari kuwaunga mkono.

Kingine ni kwamba siku Watz watakapoacha UNAFIKI basi wataweza kuwapata Viongozi wenye Mapinduzi ya FIKRA watakao waongoza kwenye Ukombozi wa kweli wa Nchi yao.
 

Yeye mwenyewe mwabukuzi ameona upinzani ulivyo mgumu, kashindwa kufanya maanadamano. Nadhani anapanic kwa ugumu uliopo.
 
Anataka vyama vya siasa vifuate matakwa yake yeye.

Ndoto yake ya kisiasa anaweza kupigania yeye binafsi na siyo kupitia migongo ya wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…