Kina Kibatala na ule msimamo wao wa kutaka Adv. Mwabukusi arudishwe kugombea, lakini kusema wazi hawatampigia kura ulikuwa ni mpango mbovu.
Kama kura ni siri sikuona sababu kwanini watangaze machaguo yao hadharani, ile ilikuwa ni sawa na kuwafanyia kampeni wagombea wao kwa kivuli cha kutetea haki ya Adv. Mwabukusi, kwangu naona walikosea pakubwa.
Nasema walikosea pakubwa kwasababu kwa hiyo misimamo yao walijigeuza kuwa vibaraka wa watawala bila wao wenyewe kujua.
Hii pia inaweza kuwa ndio sababu ya Adv. Mwabukusi kushinda kesi yake ijumaa, kwasababu watawala walijua kumbe Adv. Mwabukusi hakubaliki miongoni mwa wapiga kura kama walivyokuwa wakihofia.