Wakili Mwambukusi huenda akashidwa kwenye kura uchaguzi wa TLS

Wakili Mwambukusi huenda akashidwa kwenye kura uchaguzi wa TLS

Taasisi nyingi zilizokuwa independent, currently zimekuwa pro government kiasi kwamba haziwezi kutimiza wajibu wake mama
 
Acheni utoto hakuna uchaguzi unafanyika ili mtu flani asishinde
Kweli lengo la kila mgombea ni kushinda uchaguzi. Lakini fitina zinafanyika na watu fulani wanashindwaga unakubaliana na hilo?
 
Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) kinarajia kufanya uchaguzi wake mkuu hivi karibuni Jijini Dodoma kumchagua rais wa kuongoza chama hicho kwa kipindi cha mwaka mmoja

Wagombea halaii waliopitishwa kupigiwa kura kwenye nafsi hiyo ni sita kati ya hao Wakili machachari Boniface Mwambukusi ni mmoja wao

Habari za uhakika zinaonyesha kuwa kuna kapeni kubwa ndani na nje ya chama hicho ili Mwambukusi ashindwe kwenye boksi la kura kwenye uchaguzi huo

Lengo ni kuhakikisha kuwa wakili huyo msomi, machachari na mwenye msimamo mkali usiyoyumba kwa Serikali hashindi kwenye uchaguzi huo na kuingoza taasisi hiyo huru ya wanasheria nchini

Ikumbukwe kuwa awali wakili Mwambukusi alienguliwa na kamati ya uchaguzi ya TLS kugombea nafasi hiyo lakini alikwenda kufungua kesi mahakama kuu kupinga kuenguliwa kwake kugombea urais wa chama hicho

Katika kesi hiyo Mwambukusi alifanikiwa kushinda na mahakama kuamuru arejeshwe kuwa mmoja wa wagombea wa nafasi ya urais wa TLS

Mmoja wa mawakili ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema kuwa mawakili wengi wamejipanga kuhakikisha kuwa Mwambukusi hashindi kwenye uchaguzi huo

Inadai kwamba baada ya Mwambukusi kushinda kesi yake ya kuenguliwa kugombea uongozi TLS alikuwa akitoa maneno na kauli za kukiponda chama hicho kuwa hakijitambui na kimeshindwa kutimiza na kusimamia majukumu yake ya msingi na muhimu ambayo ni kuwatetea wananchi na kupinga uonevu na ukandamizaji nchini

Comasava
Basi atashinda, kama walipanga mipango miovu ya kumuengua na akarudishwa uwe na uhakika atashinda
 
Back
Top Bottom