Mimi ni Shahidi na Mlalamikaji aliyetetewa na Wakili Msomi
Pascal Mayalla
Ilikuwa hivi, yaani nilipeleka Ng'ombe yangu ikapandwe kwa Ng'ombe Dume wa jirani yangu anayeishi kijiji jirani namimi pale Nkungulyabashashi...jirani akanifanyia uhuni wa mjini yaani Akanibadilishia Dume la Ng'ombe na kumpandisha Ng'ombe wangu kwa kadume kadhaifu ambako pia hamkuridhisha Ng'ombe wangu na sidhani kama aliingiza mbegu ndani
Nilipeleka malalamiko kwa Balozi na kwa Mwenyekiti wa kijiji, wakashindwa kesi nikapeleka kesi ofisi ya Kata...kisha Afisa Mtendaji akanishauri nikafungue jalada mahakamani na nimtafute Mwanasheria...
LA HAULA, Mungu si Athumani, nikakutana na Wakili Pascal Mayalla, naye akanishauri nisubiri ngombe ashike mimba na azae Mtoto kisha tuangalie kama atafanana na Dume lipi na hapo tutapata Ushahidi utaonipa nguvu ya kushinda kesi katika mahakama ya Wilaya alisisitiza
Ndugu yangu na Wakili
Pascal Mayalla nakushukuru sana Ngosha