Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Rais wa chama cha Wanasheria nchini TLS, Wakili Sweetbert Nkuba amekataa kutambua ushindi alioupata mpinzani wake wa karibu Mwabukusi kwa madai ya ukiukaji wa mwenendo wa uchaguzi.
Pia soma: Uchaguzi wa TLS 2024: Boniface Mwabukusi ashinda Urais, apata kura 1274
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Nkuba amesema ameshawasiliana na wanasheria wake ili kwenda kupinga ushindi wa Mwabukusi mahakamani.
"Mojawapo ni kuona karatasi za kupigia kura kuisha na kwenda kuchapishwa zingine, kufanyiwa vurugu na kusambaa taarifa mitandaoni ushindi wa mpinzani wangu kabla ya kutangazwa na msimamizi wa uchaguzi," amesema Nkuba
Katika uchaguzi huo uliofanyika Jana na matokeo yake kutangazwa usiku, Wakili Nkuba alizidiwa zaidi ya kura 400 na mpinzani wake Wakili Mwabukusi ambaye alitangazwa kuwa mshindi.