Wakili Sweetbert Nkuba kupinga ushinda wa Wakili Boniface Mwabukusi kuwa Rais wa TLS

Wakili Sweetbert Nkuba kupinga ushinda wa Wakili Boniface Mwabukusi kuwa Rais wa TLS

Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Rais wa chama cha Wanasheria nchini TLS, Wakili Sweetbert Nkuba amekataa kutambua ushindi alioupata mpinzani wake wa karibu Mwabukusi kwa madai ya ukiukaji wa mwenendo wa uchaguzi.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Nkuba amesema ameshawasiliana na wanasheria wake ili kwenda kupinga ushindi wa Mwabukusi mahakamani.

"Mojawapo ni kuona karatasi za kupigia kura kuisha na kwenda kuchapishwa zingine, kufanyiwa vurugu na kusambaa taarifa mitandaoni ushindi wa mpinzani wangu kabla ya kutangazwa na msimamizi wa uchaguzi," amesema Nkuba

Katika uchaguzi huo uliofanyika Jana na matokeo yake kutangazwa usiku, Wakili Nkuba alizidiwa zaidi ya kura 400 na mpinzani wake Wakili Mwabukusi ambaye alitangazwa kuwa mshindi.

View attachment 3060290
Nkuba atulie Mbona inamuuma Sanaa akubali kushindwa asubirie next time
 
Kura zilkuwa zimeshahesabiwa usisahau Msimamizi wa mwabukusi Alikuwa Adv jebra ambaye alikuwa ndani Ya sehemu ya kuhesabia kura na alikuwa nyuma ya Jaji anayetangaza kura..
Ni uhuni tu umefanyika pale.
 
Ni uhuni tu umefanyika pale.
Hata wakirudia uchaguzi atashindwa Tena nilikuwepo sehemu ya Tukio nilishuhudia pia
20240803_001827.jpg
 
Na waliotangaza ushindi kwa kura kabisa kabla ya uchaguzi kufanyika unazungumziaje??
Hakuna aliyetangaza Ushindi wa kura kabla ya Uchaguzi..

Kura zimeanza kutangazwa idadi kuanzia saa mbili usiku hiyo ni baada ya kukamilika kwa kuhesabiwa kwa Kura saa moja jioni
 
Back
Top Bottom