Habari wakuu,
Umri wangu ni miaka 27 na bado sijaoa wala sijafikiria kuoa nataka nianze kutafuta mwenza nikifika 30years, lakini hapa kilichonishtua ni wimbi kubwa la kina single mothers wadada kwa wamama wengi sana mitaani wana watoto na hawakai na wazazi wenza, asilimia 75 niliokutana nao hadi sasa ni single mothers, unakuta binti mrembo kafungasha rangi nzuri sura nzuri kidini mnaendana lakini kazalishwa na hana mume.
Mbaya zaidi hata ex wangu aliyenipaga kibuti alivyofika chuo kikuu sahivi na yeye ni single mother, yaani nimechanganyikiwa sijui pa kushika yaani naogopa sana kuoa single mother nahisi sitakuwa huru.
Mnishauri jamani namna ya kuishi na single mother ikitokea nimeangukia huko.