Let's talk as mature people and look into the bigger picture. Sidhani kama kuitwa single mom au kukataliwa is such a big deal compared na effects anazopata mtoto. If you are a responsible man who was raised well and knows the value of a family; being a single dad isn't something you would wish even if no one is going to point a finger at you. Kwa sababu katika yote hata mwisho wa siku victim mkuu hapa ni mtoto. Baba unaweza kuoa; mama anaweza kuolewa lakini kwa mtoto kuna vitu tu vitamfuata kwa sababu tu ni mtoto wa nje.
Afu huku kwetu co-parenting sio rahisi sana; lazima utaishia kustick na watoto wa ndani; wa nje unabaki kuwa "seasonal parent". Ukioa/kuolewa mawasiliano na mzazi mwenzio inabidi yapungue haswa kama sio kukoma; kama unataka kuishi kwa amani na kuaminika kwa mwenzio. So mtoto ndo anayeumia hapa; lazima atampoteza mzazi mmoja; hatuna ile malezi 50/50 kwa wazazi wote.
Imagine wewe ni mtoto unaishi na mama ameolewa na ana watoto wa ndoa; there is a certain way tu utafeel like you don't belong there completely. Siku ukienda kwa Baba unamkuta na watoto wake wa ndoa; na huko kuna hali fulani tu ya kujiona kama unakosa umiliki 100%; kwa wazazi wote upo nje ndani. Wakija ndugu wa mzazi wa kambo; watakukumbusha tu kuwa wewe sio damu yao. Imagine watoto wa nje wanavyosuffer ikija kwenye issue za mirathi; hata kama ni haki yao bado wanaonekana kama ndo tatizo kwa familia.
Kama haitoshi watoto wengine wanapelekwa kulelewa kwa bibi sijui mama mkubwa etc; ili mzazi akaishi kwa amani kwenye ndoa yake; unaweza kuhisi ni nini kinajengeka kwenye akili ya huyu mtoto; yeye ni mbaya kwenye ndoa za wazazi wake ndo maana akaachwa kwa mlezi mwingine au ni vipi?
Narudia tena ukiwa mwanaume responsible na umelelewa vyema na wazazi wako; obviously utawish kufanya the same and more kwa mtoto wako. (Most of times; you can't give what you don't have). Imagine being a seasonal father kwa mwanao; kwa mwaka mnaonana mara moja au mbili au msionane kabisa; he/she is raised by someone else, another man matters the most to your child than you do; sijui kama haitokuumiza. So even if no woman is going to reject you; at least be responsible for the welfare of your children. Na hata kama hutokuwa rejected; how can you guarantee the welfare of your kid(s) kwa huyo mke utakayemuoa? Ni watoto wangapi wanasuffer kwenye mikono ya mama wa kambo/abusive step dads na wanashindwa hata kusema? Wapende wanao; waepushe na unnecessary complications