Wakinamama wanaolea watoto bila baba (single mothers): Sababu, athari kwa mtoto, changamoto na mitazamo ya jamii

Wakinamama wanaolea watoto bila baba (single mothers): Sababu, athari kwa mtoto, changamoto na mitazamo ya jamii

Sasa hilo swali muulize muumba usiniulize mimi maana yeye ndiye aliyeruhusu hii dunia ya sasa kuwe na ndoa zenye waume waovu na wake wema na zinadumu na vile vile ndoa zenye waume wema na wake waovu na zinadumu!!

Unaonaje ukanijibu pia hili swali biblia inasema "mshahara wa dhambi ni mauti" si ndiyo haya je ni watu wote duniani wanaokufa wanakufa kwa ajili ya dhambi zao na je sisi tunaoendelea kuwa hai ni kwamba ni watakatifu hatuna dhambi??

Yaani Mungu ameruhusu? Duh, basi sawa.
Habari ya mshahara wa dhambi ni mauti ni habari nyingine hiyo. Nafsi itendayo dhambi hakika itakufa, ndivyo maandiko yalivyo. Sisi tunaoishi bado hatujafika mwisho wa mwezi tukapokee huo mshahara, usichanganye mada.
 
Sasa wewe Nyenyere unadhani watu wanatenda mema kwa ajili ya kuwafurahisha wanadamu?? Aise kama wapo watu wa aina hiyo basi nawapa pole mimi kama kuna sababu yoyote inayonifanya nisitende dhambi basi ni Mungu tu na si kitu kingine isingekuwa Mungu basi pengine saa hizi ningekuwa nina dhambi kama bahari mimi siishi kwa kufuata mitazamo ya watu wengine ambao hawawezi kunifanya kitu

Na hata siku moja siwezi kufungwa na tamaduni za kishenzi zilizotungwa na wanadamu kama mimi tena zinazonikandamiza nafungwa na maandiko tu kwa sababu maandiko ni ya aliyeniumba na hayanikandamizi sasa wewe unaposema hauongelei dhambi ina maana unataka watu wafanye vitu kuwafurahisha wanadamu na siyo Mungu?? Narudia tena hiyo jamii unayoiota haipo na haitakuwepo amka tu kutoka kwenye huo usingizi
Uko sahihi, mimi sijazungumzia dhambi. Msamaha ni kwa wanadamu wote bila kuchagua. Ila kwa mabinti ni heri wakatunza ubinti wao kuliko kujiingiza kwenye ngono za mapema na kuangukia kwenye kundi hili. Baadaye itakuja kuwa majuto kama inavyoonekana sasa
 
Hata siku moja mwanaume hawezi kusimama kwenye nafasi ya mwanamke na wala mwanamke hawezi kusimama kwenye nafasi ya mwanaume yaani kwamba hakuna anayeweza kusimama kwenye nafasi ya mwingine hivyo kila mtu asimame kwenye nafasi yake

Nikimaanisha mwanaume asimame kwenye nafasi yake na mwanamke asimame kwenye nafasi yake sasa ingekuwa vizuri kama hiyo sentensi yako ya mwisho ungewaambia wanaume wenzio ambao wao kubadilika wanasubiri eti hadi mwanamke abadilike imagine mtu anakwambia wanawake anzeni kubadilika wanaume watafuata seriously?? Kila jinsia inatakiwa ibadilike kwa nafasi yake huu ndiyo ukweli!!
Simama kwenye nafasi yako, umeelewa? Feminism imekupoteza hata huoni
 
Kwahiyo hapo mwanaume anakuwa hajafanya makosa anakuwa yuko sahihi kabisa??
Mwanamume anayemtoa bikra binti imempasa kumwoa, lakini kinachofanyika unanyofoana vichakani kwa kukidhi kiu ya wakati huo,ikifika wakati akili zimekaa sawa mwanamume hamwoni binti kama chaguo sahihi. Inabaki ni kilio na kusaga meno
 
Wewe unadhani kila ndoa iliyodumu imefuata hizo kanuni unazozijua wewe?? Na kwahiyo wazazi wanatakiwa wawalee vizuri watoto wa kike tu ila watoto wa kiume walelewe vibaya ili waje kurubuni watu siyo??
Nilijibu swali kufuatia mahitajio yake. Wewe unaleta feminism
 
Wapi nimeongelea dhambi? Uko negative ndio maana umejenga picha akili mwako ambayo wala haipo hapa.
Single mama wengi ni matokeo ya uzinzi ama uasherati. Kwani hii verse ulikuwa unamaanisha nini??? Uzinzi sio dhambi ni biskuti eti???[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Mzee tulishamalizana tukaelewana nini tena unaanza kushupaza shingo[emoji15][emoji15][emoji15][emoji15]
 
Eti kwa Mungu kugumu labda wewe ndiyo unaona hivyo mimi najua maandiko kuliko unavyofikiria na ninayoyaongea mimi kwa asilimia kubwa yanatokana na maandiko sasa wanaume kama ninyi msiokubali ukweli lazima mtuite majina kama feminist sijui nini mnajua wenyewe ila ukweli unauma

Si unaona hata wewe nimekupeleka kwenye maandiko ukaanza kusema oohh hii mada wanachangia hata non believers sijui nini haya ndiyo hao kina Kiranga sasa wamekuja kuchangia tukiwaunga mkono mnasema kwa Mungu kugumu hahahaha Mungu siyo mnafiki kama wewe aise soma maandiko yote na uyaelewe
Kama unataka maandiko, twende kazi. Hoja zako nyingi zina mwelekeo wa feminism
 
Moja, hakuna sehemu mimi nimeongelea dhambi. Hayo ya dhambi unajua mwenyewe ulikoyatoa. Na mimi sitakuja kuadvocate watu watende dhambi, sababu mshahara wake ni mzito. Mimi nimeongelea mshahara wa hiyo dhambi yenu ya kutelekezana.

Mbili, jiulize mwenyewe kwa umri ulionao, umeshawahi kusikia MWANAUME AMEZAA SANA MPAKA AMECHAKAA HATAMANIKI? Ukipata majibu, utaacha kushindana na nature na utajiweka mahala salama.

Shida yako ni kutanguliza hisia za kuwa unaonewa to an extent huoni ukweli. Ukweli ni huu: Dunia ina watu wengi wabaya kwa tabia. Kwa kuwa ni wengi, na wewe hupendi watu wabaya, jambo rahisi kwako ni wewe kuifunda nafsi yako iwaepuke watu wabaya kuliko kutaka kuibadili dunia kwa hisia.

Hamna sehemu mimi nimesema wanaume wanaozalisha wanawake na kuwatelekeza wanafanya vyema, kama umenifuatilia vizuri nilikueleza kuwa hao sio wanaume, ni mabrazameni wasiojua majukumu ya mwanaume. Lakini kwa kuwa hawawabaki, huwa mnaenda huko wenyewe na akili zenu za kushikiwa, cha muhimu ni nyie waathirika kuanza kuwaza kwa kutumia ubongo badala ya moyo ili msitujazie nchi na vitoto visivyoishi na baba zao. Kama mpaka hapa hujanielewa basi atakuelewesha brazameni, maana wao huwa wana lugha mnazozielewa
Tatizo lililopo mkuu ni kuwa watu hawa wamejenga mtazamo fulani vichwani, hivyo wanauleta humu wakidhani ndicho kilichoandikwa
 
Sasa uliona wapi mchungaji anakemea uzinzi na uasherati kwa wanawake tu na kuwaacha wanaume?? Huyo mchungaji si atakuwa mnafiki biblia inakataza uzinzi na uasherati kwa jinsia zote haijasema sijui nani anapata madhara nani hapati madhara hapana imesema tu kwamba uzinzi na uasherati ni dhambi

Na hicho ndicho kinachotakiwa kihubiriwe kwa watu wote wa mataifa tofauti na hapo huo ni unafiki na hata biblia hiyo hiyo imemuita mnafiki mtu ambaye anatoa boriti kwenye jicho la mwingine kabla ya kutoa kibanzi kwenye jicho lake mwenyewe sasa wewe tukikuita mnafiki unasema sijui sindano zinauma mara hatupendi ukweli sasa kati ya sisi na wewe nani hapendi ukweli??
Pia hakuna sehemu nimehukumu dhambi, mimi ni mkristo, nimesem aawazi kwenye comments nyingi tu huko juu, msamaha wa dhambi upo. Hao ni kwa wanaoaminikatika Mungu. Repentence is a U-turn process. Kama uliutia mwili addiction fulani, unahitaji neema kubwa kuiacha, si kufumba na kufumbua.

Pia kukemea dhambi kama uasherati si kuhukumu hata kidogo, ni wajibu. Tatizo la makanisa ya siku hizi yamegeuka "feel good churches," yaani mtu anakwenda kufarijiwa ili ajihisi vizuri na si kukemewa kuacha dhambi. Kumbe Munguhahitaji watu wengi, anahitaji watu waliotubu. Kukemea uasherati sio kuhukumu ndugu yangu
 
Kwa maneno ya jamaa Mwanamke akiolewa akiachika anafaa kuolewa kabisaa huyo Sio single mama hata kama ana watoto..[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] maana alifunga ndoa. Na Hajui ndoa zenye misukosuko ni za aina hiyo ambapo wanaume waliowazalisha wanawake baada ya kufunga ndoa na kuachana nao wanakuwa bado wapo hai. Mwanamke ambae mwanaume aliemzalisha either kwa ndoa au bila ndoa alifariki, wengi wao huwaga hawana shida na ndoa zao mpya na wengine huamua kutulia wasiolewe kabisa.
Mbona jamaa kaongea vizuri tu sema wewe unauchukulia personal usingle mother wako. Jamaa alisema wale waliofiwa na wame Tao wanaweza kuolewa kwasababu kiapo cha ndoa kinakuwa hakipo tena. Sasa ukiachika na kuolewa wewe ni mzinifu tu na hakuna namna nyingine. Tukubali maonyo yanapotujia.
 
Mimi kuna mtoto wa mama Mkubwa wangu alidanganywa na mwanaume kuwa anataka Kumuoaa yule dada akasema bhasi tufunge ndoa kabla ya yote mwanaume akasema Nahitaji kukujua kwanza kiti ambacho kimekuwa common sana kwenye Jamii ya sasa hakuna mtu anataka aoe alafu baadae story za mtoto iwe vita... Duuh cster akabeba mimba huku mipango ya Sendoff na ndoa ishaanza na michango pia aisee Kuja kujuaa yule mzee ana Familia yake ya Watoto watatu[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24] Can you imagine jambo kama hili limkute dada yako???? Yani yule dada isingekuwa kumuwahi tusingekuwa nae duniani aliona bora afe...lakini wazazi wakamtuliza mwisho wa siku akabaki kuwa Single mama wakati alikuwa dada mwenye maadili mazuri sana na msomi. So mwanaume asipoleta zengwe na kumkataa mwanamke hakuna SINGLE MAMA duniani tatizo wanaume minyege ikituzidi huwaga tunasahau kabisa kuwa kuna mimba kifatacho sasa ndo Single mama na watoto wa mtaani.
 
Back
Top Bottom