Wakinamama wanaolea watoto bila baba (single mothers): Sababu, athari kwa mtoto, changamoto na mitazamo ya jamii

Kwasababu hawakujitia mimba

Kwasababu hamuwezi kupangia waowaji na waolewaji nini wanataka, nini wanapenda

Bado ni suala la mtu binafsi.
Hakuna anayepangiwa, wanashauriwa. Na tunashauri kutokana na experience. Na hakuna wa kunipangia nini cha kumshauri mtu, ni suala la mtu binafsi. Acha ushauri utembee, wa kufuata atafuata, wa kuacha aache lakini wameonywa.
 
Afanikiwe, asifanikiwe, ushauri kuhusu kuoa ndio huo nimeshautoa. Single mother hapana.
 
Huna cha kunifundisha mimi, tunabadilishana mitazamo tu.



Pole wewe, hocho unachokiamini huko ulaya na marekani kimeshondwa na sasa wengi wanafanya marekebisho
Na kwanini haujawahi kuwaambia wanawake wasiolewe na wanaume wenye watoto nje ya ndoa??
 
Na kwanini haujawahi kuwaambia wanawake wasiolewe na wanaume wenye watoto nje ya ndoa??
Kwa sababu mwanamke hachagui mke, bali anachaguliwa. Pia mwanamke haoi bali anaolewa. Kumbuka kwa baadhi ya imani mwqnamume aweza kuoa mke zaidi ya mmoja na ikahesabika sahihi mbele ya jamii, so mwanamke akiwa msaidizi anatolewa kwao kuja kumjenge mwanamume ukoo bila kujali ana mtoto ama la.

Ndoa ni ya mwanamume sio ya mwanamke na mwanamume, get the facts straight first.
 
Nakumbuka niilishawahi kukutolea mfano wa kule Eden kwamba Evah ndiye aliyemshawishi Adam kula tunda lakini wote walipewa adhabu!! Sasa kama kweli anayekubali kushawishika hana makosa kwanini naye alipewa adhabu kwanini adhabu asingepewa aliyeshawishi peke yake??

Maana yake ni nini?? Maana yake ni kwamba vishawishi vipo na ni jukumu lako na wajibu wako kuvishinda kwa sababu uwezo wa kuvishinda umepewa ila kwa vile wanaume mnajiona mmeumbwa na tamaa mnavikumbatia hivyo vishawishi halafu mnatafuta sababu za kujitetea na kujiona hamna makosa wakati aliyeshawishi na aliyekubali kushawishika wote wana makosa!!

Mind you hakuna andiko kwenye biblia limesema eti mwanamke anatakiwa amsaidie mwanaume kupunguza tamaa kila jinsia ina maovu yake na kila jinsia inatakiwa ipambane kivyake katika kuacha hayo maovu na siyo kusingizia kuwa eti jinsia fulani ndiyo na ndiyo inatakiwa hakuna kitu kama hiko

Kumbuka hata Mungu alimruhusu Shetani kuja kutujaribu hapa duniani na akatupa uwezo wa kumshinda na watakaoshindwa wakaanguka basi watahukumiwa naye kuenda motoni sasa usitegemee eti siku ya hukumu utaenda kumuambia Mungu kwamba Shetani ndiyo alikufanya ukatenda dhambi hiyo sababu na utahukumiwa wewe pamoja na huyo Shetani wako
 
Kwahiyo mwanaume kubaka ni sawa hata kama katengenezewa mazingira??
 
Umekwepa ukweli
 
mfano mimi na wewe tunapendana, nikikuomba unizalie unaweza nipa masharti gani?
Mimi binafsi siwezi kuzaa nje ya ndoa ila kumbuka udhaifu wa wanawake wengi ni kupenda kwa dhati na wanaume mkishajua mmependwa huwa kuna vitu mnafanya makusudi sababu mnajua hamuwezi kuachwa

Hivyo kuna wanaume wengine wanautumia huo udhaifu na wanawaambia wanawake wao wawazalie watoto ndiyo watawaoa na wakikataa basi wanaachana sasa kwa mwanamke ambaye kapenda kweli lazima akubali tu hata kama ni kishingo upande na shida ndiyo inaanzia hapo
 
Karma, Biblia inasema aliyedanganywa ni mwanamke na sio mwanamume. Shetani alimdanganya mwanamke, mwanamke akamdangaya mwamume.

Hata leo shetani anamdanganya mwanamke ajiweke uchi, ajipambe kikahaba kisha mwanamke anamdanganya mwanamume.

Ndio maana tunawaonya mrudi kwenye mstari mtuokoe, hata wachungaji wengi wameangushwa na wanawake
 
Kwa binti mwenye maadili, hawezi kuwa kwenye mazingira yatakayo mfanya awe target, hata wazazi wanaojali hawawezi kumweka binti yao kwenye mazingira kama hayo. Kumbuka umeongelea kijijini.
Kwahiyo mkuu wewe unadhani mwanaume kaumbwa na tamaa ila aje aitumie tamaa yake vizuri hapa duniani?? Kwamba hajapewa kabisa uwezo wa kuishinda hivyo hata akiitumia ni sawa tu si ndiyo??
 
Karma, Pia hapa siongelei dhambi ya zinaa, naongelea vijana kutokuoa single mothers. By the way kwa nini ukabadili ID toka Marianah!?
 
Wanawake wanaokubali ombi hili hawafai kuw wake wa ndoa. Ni wasio jitambua kabisa.
Yaani kwanza kabisa haujajibu swali langu halafu pili kwahiyo hao wanaume wanaowaomba wanawake wao wawazalie kabla ya ndoa wakati wanajua siyo vizuri ndiyo wako sahihi na wanafaa kuwa waume wa ndoa si ndiyo??
 
Afanikiwe, asifanikiwe, ushauri kuhusu kuoa ndio huo nimeshautoa. Single mother hapana.
Oohh sasa si ungesema tu tangu mwanzo kwamba huo ni mtazamo wako wewe na siyo uhalisia sasa unapomuingiza hadi Mungu kwenye haya maswala una maana gani?? Kuwa makini!!
 
Jukumu la mwanamke si kupenda bali kutii, mwanamume ndiye mwenye kupenda. Sasa wanawake wa mwendo kasi wanajipa majukumu ya wanaume, matokeo yake ni kupotea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…