Wakinamama wanaolea watoto bila baba (single mothers): Sababu, athari kwa mtoto, changamoto na mitazamo ya jamii

Wakinamama wanaolea watoto bila baba (single mothers): Sababu, athari kwa mtoto, changamoto na mitazamo ya jamii

Usitawaliwe na 50/50 boss,
Ulishasikia kuna mwanamke amekataa kuolewa na mwanaume mwenye mtoto wa nje?

Ila mwanamke, kuwa naye mmoja tu! Utakuwa Topic mtaa mzima na unaweza kupishana na bahati nyingi za kuolewa.
Siyo 50/50 bali huo ndiyo ukweli,, lakini kwa vile watu mmekengeuka badala ya kufuata maandiko ya Mungu mnafuata mitazamo ya jamii na ndiyo hapo mnapojikuta mnalazimisha utofauti wa hizi jinsia mbili hadi kwenye dhambi..

Kwamba eti jinsia moja inaruhusiwa kutenda dhambi hii lakini jinsia nyingine hairuhusiwi kutenda dhambi hii ukiuliza kwanini eti ndivyo tamaduni zilivyokuwa tangu enzi na enzi kwahiyo jamii ndiyo inaona hivyo kwani what is jamii?? Kwani jamii ndiyo iliyokuumba na je aliyekuumba ndivyo anavyotaka hivyo??

Halafu hawa watu wanaofuata mitazamo ya jamii ndiyo wale unakuta mwanamke kafikisha miaka 26 tu hajaolewa anaanza kuhangaika kwa waganga kwa kujiona ana mikosi eti kwa sababu tu jamii imemnyooshea vidole kwamba kwanini hajaolewa!! Na ninashindwa kuelewa kwanini jamii iwe na mitazamo ya ajabu kiasi hicho tena mitazamo iliyo kinyume na matakwa ya Mungu!!

Yaani napata wakati mgumu kuelewa inakuwaje mtu anaruhusu jamii imuamulie maisha yake tena jamii hiyo hiyo ambayo nayo ina maovu mengi na ina matatizo mengi tu eti ndiyo iwe hakimu wa maisha yake kiasi cha huyo mtu kushindwa kuishi kwa amani kwa sababu ya kufanya vile inavyotaka jamii na ndiyo maana hata ndoa nyingi za siku hizi hazidumu maana unakuta mwanamke hajaolewa kwa sababu yuko tayari bali kaolewa kwa sababu ya kuhofia umri kuenda na kukosa mume na yote hiyo inatokana na nini?? MITAZAMO YA JAMII!!
 
Nyie hamjawahi kujitambua hata siku moja. Ni reheme za Mungu ndio zinawalinda tu.

BR
Uduzungwa.
Halafu wanaume mnaotoaga kauli kama hizi tukija kuangalia maisha yenu tunakuta ndiyo wale wale tu
 
What other reputation do you have??
Nyingi tuu nikiianza kuelezea ntajaza server za humu

Ila ndo hvyo Yule jamaa hayuko peke ake na wengi tunamuunga mkono sasa wewe endelea kuuliza maswali yako nyinyi Kama Nani
 
mie sijaisoma yote,lol

mie kuna kitu kinanishangaza kuhusu hizi topics za single mothers...

utasikia hatuoi single mothers..huu ndio msimamo wetu mabaharia...

na huu msimamo unajulikana,

sasa hizi topic za single mothers ni nyingi sana...

sasa jibu ni lile lile

nachowauliza hamchoki ??

kutoa jibu hilo hilo…??

clearly mabaharia hamna umoja😉😉😂😂😂

mabaharia wengine hawaelewi somo😂😂
Mabaharia tunarudia rudia hii....
kama vile tunavyorudia rudia kuvuta bangi....
tunamaanisha
 
Huyo mwanamke hajielewi ndio maana jamaa alizaa nae akamwacha
Na sasa anelekea kuachwa tena wala huyo baba watoto wake wa zamani hatamuoa.

Kama huyo ex wake ameweza kumshawishi na akamhurumia na kuamua kumwacha mume basi anaweza kumkubali mwanaume mwingine yeyote pia.... huyu baada ya muda atakua single tena
Yaa atakuwa loos ball....
looser to pay winner to stay
 
nimesema hiviiiiiiii

Nikikupenda wewe mwanamke uliyezaa na mwanaume mwingine

Nakupenda wewe na mwanao HUDUMA zote muhimu za mtoto nabeba mwenyewe

Sitaki kusikia wewe mwanamke unapokea hata sent kwa mwanaume Aliyekuzalisha (sitaki kusaidiwa majukumu)

Alikuacha mwenyewe so akuache hivyo hivyo milele

Nisiskie fyoko wala fyoko hela ya mtumizi ya mwanangu hiiii hapa (akitaka amchukue mwanae akamlee huko)

nikiwa na mahusiano na mwanamke aliezalishwa MARUFUKU kwangu kuona mnawasiliana na mzazi mwenzio
 
Nimekuelewa sana apa.
Ni umalaya tu. Mtu kakutelekeza na watoto wawili, then umepata mtu wa kukuchukua pamoja na majukumu hayo ( watoto wawili). Then unataka kuvunja ndoa kwa ajili ya aliye kutelekeza?

Nilisoma sehemu flani, unapoingia kwenye ndoa sio kwamba hautapenda tena au kutamani tena, bali unatakiwa kuheshimu kiapo chako kwa mwenza wako.
 
Oa single mothers mwenye sifa zifuatazo :
1. Aliye zaa nae awe amekufa,na uhskikidhe hilo sio kwa kuambiwa tu.

2. Au alie zaa nae awe chizi/kichaa/mwendawazimu asie weza kupona leo wala kesho na uhakikishe hilo toka kwa daktari unae muamini.

3. Kadhalika usiishi na watoto baada ya kubaleghe,wakiwa chini miaka mitano unaweza kuishi nao,ila kinyume na hapo utajua mwenyewe.

Nipo ....
 
  • Thanks
Reactions: amu
nimesema hiviiiiiiii

Nikikupenda wewe mwanamke uliyezaa na mwanaume mwingine

Nakupenda wewe na mwanao HUDUMA zote muhimu za mtoto nabeba mwenyewe

Sitaki kusikia wewe mwanamke unapokea hata sent kwa mwanaume Aliyekuzalisha (sitaki kusaidiwa majukumu)

Alikuacha mwenyewe so akuache hivyo hivyo milele

Nisiskie fyoko wala fyoko hela ya mtumizi ya mwanangu hiiii hapa (akitaka amchukue mwanae akamlee huko)

nikiwa na mahusiano na mwanamke aliezalishwa MARUFUKU kwangu kuona mnawasiliana na mzazi mwenzio
Wanawake wa ajabu....
utakapo mzuia na yy ndio ataongeza bidii ya mawasiliano.....kwa kificho...
utajua hujui....
creatures wa ajabu sana hao
 
Nilikuwa najiuliza mbona humu Jf wanawananga sana single mother kuwa hawaachani na baba wa watoto wao,nikafikiria kwa msimamo tulionao wanawake tukiacha tunaacha kweli ,wanatusingizia

Lakini kwa nilichoshuhudia kwa macho na masikio yangu,sijui wanakwama wapi hawa wanawake wenzangu jamani

Ni mama wa watoto wawili aliyezaa wakati anasoma chuo fulani na mwanaume fulani kipindi hicho akiwa chuo,mtoto wa kwanza alimzaa akiwa mwaka wa kwanza na wa pili alimzaa wakati anahitimu chuo,na kwa bahati nzuri akapata kazi kwenye kampuni fulani na kwa jeuri yule mwanaume aliyekuwa naye chuo alimuacha katika mazingira ya kutatanisha na mawasiliano yakawa yamekatika kipindi wamehitimu chuo

Baada ya mwaka 1 huyu mdada akawa amepata mwanaume mwingine akamuoa tu vizuri kwa harusi kubwa tu

Cha ajabu wiki kama 4 zimepita yule kaka aliyezaa naye watoto wawili akaibuka,akamtafuta,wakagombana na wakabembelezana wakakubaliana huyo kaka atakuwa anamtumia hela mdada ya kuwahudumia watoto muda huo akijiandaa kumwambia mume wake kuhusu hao watoto awarudishe kwa baba yao

Wakakubaliana kuwa siku fulani watakutana hoteli fulani atawapeleka watoto wakamsalimie baba yao,bila mume wake kujua

Siku ya siku mdada akawapeleka hotel nje kidogo ya mji,basi wakakutana,ila mdada akawa na msimamo kuwa endapo ex atajaribu kuleta ushawishi hatakubali hata siku moja,bahati mbaya mtoto wao wa kwanza akawa anaongea maneno kwa baba na mama ya kuwaleta pamoja hadi mdada akawa na huruma kwa ex wake akajikuta anataka avunje ndoa arudi kwa ex wake na huku ex wake ana mke na mtoto 1

Juzi mume wa ndoa anapata mchezo mzima,anamuuliza mke wake anasema ni kweli anadai talaka arudi kwa baba watoto wake

Nimeamini wanawake muda mwingine hatutumii akili

Alikutelekeza,akakuacha mwenyewe ukatunza watoto mwenyewe,from no where mnarudiana kisa maneno ya mtoto wao wa kwanza yamemfanya alie,amhurumie na amrudie ex wake
Yaani siyo suala la kuzaa tu... mwanamke aliyefanya mapenzi na mwanaume (katika category hii siingizi wanawake dada poa wale ambao mwanaume anapiga na kusepa) huwa mara nyingi hana ujanja kwa huyo mwanaume huyo. Inaawezekana wapo wasiokumbukana lkn hao wanaweza kuwa kwenye kundi la hit and run. Lakini nakwambia wale ambao walikuwa wapenzi kwa maana ya wapenzi wakaja kuseparate wakikutana huongea lugha nzuri kabisa na mwanaume akitaka kukumbushia kwa mwanamke huyo inawezekana kabisa. Sasa hiki ninachokieleza kipo chini ya kiwango linapokuja suala la wazazi (tena mtoa mada kakoa mfano mzuri kabisa kuwa mdada alizaa na jamaa watoto wawili then akaolewa na mwingine) maana hawa wana mengi ya kushare kuhusu mtoto wao lakini wamechanganya na damu kabisa hawa. Hivyo basi watu hawa kuachana kabisa inatakiwa mmoja wao (si wote kwa maana hicho ni kipaji anachokuwa nacho mtu mmoja mmoja) kuwa na moyo mkuu wa kukataa kuyarudia baada ya kuvunjika.

Wapo wanawake wachache wanaoweza kuanzisha mahusiano na wenza wapya baada ya kuachana na wazazi wenzao.
 
Back
Top Bottom