Nilikuwa najiuliza mbona humu Jf wanawananga sana single mother kuwa hawaachani na baba wa watoto wao,nikafikiria kwa msimamo tulionao wanawake tukiacha tunaacha kweli ,wanatusingizia
Lakini kwa nilichoshuhudia kwa macho na masikio yangu,sijui wanakwama wapi hawa wanawake wenzangu jamani
Ni mama wa watoto wawili aliyezaa wakati anasoma chuo fulani na mwanaume fulani kipindi hicho akiwa chuo,mtoto wa kwanza alimzaa akiwa mwaka wa kwanza na wa pili alimzaa wakati anahitimu chuo,na kwa bahati nzuri akapata kazi kwenye kampuni fulani na kwa jeuri yule mwanaume aliyekuwa naye chuo alimuacha katika mazingira ya kutatanisha na mawasiliano yakawa yamekatika kipindi wamehitimu chuo
Baada ya mwaka 1 huyu mdada akawa amepata mwanaume mwingine akamuoa tu vizuri kwa harusi kubwa tu
Cha ajabu wiki kama 4 zimepita yule kaka aliyezaa naye watoto wawili akaibuka,akamtafuta,wakagombana na wakabembelezana wakakubaliana huyo kaka atakuwa anamtumia hela mdada ya kuwahudumia watoto muda huo akijiandaa kumwambia mume wake kuhusu hao watoto awarudishe kwa baba yao
Wakakubaliana kuwa siku fulani watakutana hoteli fulani atawapeleka watoto wakamsalimie baba yao,bila mume wake kujua
Siku ya siku mdada akawapeleka hotel nje kidogo ya mji,basi wakakutana,ila mdada akawa na msimamo kuwa endapo ex atajaribu kuleta ushawishi hatakubali hata siku moja,bahati mbaya mtoto wao wa kwanza akawa anaongea maneno kwa baba na mama ya kuwaleta pamoja hadi mdada akawa na huruma kwa ex wake akajikuta anataka avunje ndoa arudi kwa ex wake na huku ex wake ana mke na mtoto 1
Juzi mume wa ndoa anapata mchezo mzima,anamuuliza mke wake anasema ni kweli anadai talaka arudi kwa baba watoto wake
Nimeamini wanawake muda mwingine hatutumii akili
Alikutelekeza,akakuacha mwenyewe ukatunza watoto mwenyewe,from no where mnarudiana kisa maneno ya mtoto wao wa kwanza yamemfanya alie,amhurumie na amrudie ex wake