Wakinamama wanaolea watoto bila baba (single mothers): Sababu, athari kwa mtoto, changamoto na mitazamo ya jamii

Wakinamama wanaolea watoto bila baba (single mothers): Sababu, athari kwa mtoto, changamoto na mitazamo ya jamii

nimesema hiviiiiiiii

Nikikupenda wewe mwanamke uliyezaa na mwanaume mwingine

Nakupenda wewe na mwanao HUDUMA zote muhimu za mtoto nabeba mwenyewe

Sitaki kusikia wewe mwanamke unapokea hata sent kwa mwanaume Aliyekuzalisha (sitaki kusaidiwa majukumu)

Alikuacha mwenyewe so akuache hivyo hivyo milele

Nisiskie fyoko wala fyoko hela ya mtumizi ya mwanangu hiiii hapa (akitaka amchukue mwanae akamlee huko)

nikiwa na mahusiano na mwanamke aliezalishwa MARUFUKU kwangu kuona mnawasiliana na mzazi mwenzio
Mkuu CONTROLA haya nayaita maamuzi ya mwanaume.
Tena bila kusahau kuwa asili hao watoto wawe wako kabisa 😆
 
Mkuu CONTROLA haya nayaita maamuzi ya mwanaume.
Tena bila kusahau kuwa asili hao watoto wawe wako kabisa 😆
Asanteeeeee

Safi kabisa hicho ndio kikubwa cha kufanya

ushenzi shenzi wa kuruhusu watu wawasiliane kumbe wanamegana

Mwisho unaachiwa nyumba,unarudi hukuti mtu

Unauliza yuko wapi anakujibu bila AIBU (nipo kwa baba flani)
 
Huyo mwanamke hajielewi ndio maana jamaa alizaa nae akamwacha
Na sasa anelekea kuachwa tena wala huyo baba watoto wake wa zamani hatamuoa.

Kama huyo ex wake ameweza kumshawishi na akamhurumia na kuamua kumwacha mume basi anaweza kumkubali mwanaume mwingine yeyote pia.... huyu baada ya muda atakua single tena
Umeona ehh,huyo mwanamke kifupi ni kuwa hajitambui,wako wengi tu wa aina hiyo wanaorudia makando kando yao akiamni kuwa jamaa bado anampenda na mwisho wa siku wanaishia kutendwa tena.Umepata mwanaume anakuchukulia mapungufu yako,ukishaona vimetulia unamgeukia tena ex wako aliekwisha kukutenda,huo ni upuuzi uliopitiliza.Wasichotaka kujiuliza,kama ulikuwa mzuri kwake lakini hakukuoa,sasa hivi umebadilika nini mpaka akutake tena,ni series tu itaendelea atakupitia na hamu yake ikiisha utaachwa tena..
 
Nitaoa tu single maza kama aliyezaa naye alifariki na nimeoneshwa na kaburi.
Nilikuwa najiuliza mbona humu Jf wanawananga sana single mother kuwa hawaachani na baba wa watoto wao,nikafikiria kwa msimamo tulionao wanawake tukiacha tunaacha kweli ,wanatusingizia

Lakini kwa nilichoshuhudia kwa macho na masikio yangu,sijui wanakwama wapi hawa wanawake wenzangu jamani

Ni mama wa watoto wawili aliyezaa wakati anasoma chuo fulani na mwanaume fulani kipindi hicho akiwa chuo,mtoto wa kwanza alimzaa akiwa mwaka wa kwanza na wa pili alimzaa wakati anahitimu chuo,na kwa bahati nzuri akapata kazi kwenye kampuni fulani na kwa jeuri yule mwanaume aliyekuwa naye chuo alimuacha katika mazingira ya kutatanisha na mawasiliano yakawa yamekatika kipindi wamehitimu chuo

Baada ya mwaka 1 huyu mdada akawa amepata mwanaume mwingine akamuoa tu vizuri kwa harusi kubwa tu

Cha ajabu wiki kama 4 zimepita yule kaka aliyezaa naye watoto wawili akaibuka,akamtafuta,wakagombana na wakabembelezana wakakubaliana huyo kaka atakuwa anamtumia hela mdada ya kuwahudumia watoto muda huo akijiandaa kumwambia mume wake kuhusu hao watoto awarudishe kwa baba yao

Wakakubaliana kuwa siku fulani watakutana hoteli fulani atawapeleka watoto wakamsalimie baba yao,bila mume wake kujua

Siku ya siku mdada akawapeleka hotel nje kidogo ya mji,basi wakakutana,ila mdada akawa na msimamo kuwa endapo ex atajaribu kuleta ushawishi hatakubali hata siku moja,bahati mbaya mtoto wao wa kwanza akawa anaongea maneno kwa baba na mama ya kuwaleta pamoja hadi mdada akawa na huruma kwa ex wake akajikuta anataka avunje ndoa arudi kwa ex wake na huku ex wake ana mke na mtoto 1

Juzi mume wa ndoa anapata mchezo mzima,anamuuliza mke wake anasema ni kweli anadai talaka arudi kwa baba watoto wake

Nimeamini wanawake muda mwingine hatutumii akili

Alikutelekeza,akakuacha mwenyewe ukatunza watoto mwenyewe,from no where mnarudiana kisa maneno ya mtoto wao wa kwanza yamemfanya alie,amhurumie na amrudie ex wake
 
Nyingi tuu nikiianza kuelezea ntajaza server za humu

Ila ndo hvyo Yule jamaa hayuko peke ake na wengi tunamuunga mkono sasa wewe endelea kuuliza maswali yako nyinyi Kama Nani
mwanaume ninaemuhunga mkono mwanaume mwenzangu Kwan kuna ulazima wa kujua mi ni nani haibadili ukweli
Nimewauliza hivyo ili nijue kwamba ninyi mkisema single mothers wasiolewe mnawaongezea nini au mnawapunguzia nini kwenye maisha yao ilihali wapo wanaume wenzenu wengi wanaojitambua wanawaoa kila iitwapo leo na ndoa zao zinadumu

Yaani ninyi wanaume wa humu JF na hizi kejeli zenu za kila siku kuhusu single mothers nilitegemea mkisema wanaume wasioe single mothers basi wanaume wote hapa bongo au kote duniani watafuata mitazamo yenu na pengine labda ipo siku single mothers wataacha kabisa kuolewa lakini wapi

Tatizo lenu wanaume huwa mnadhani Mungu ni wenu peke yenu na kwamba eti ndoa inapangwa na wanadamu!! Sasa kama anaruhusu wanaume wenye watoto waoe wanawake wasio na watoto kwanini asiruhusu wanawake wenye watoto waolewe na wanaume wasio na watoto??

Tena ukizingatia hao wala hawakujibebesha mimba wenyewe lakini mwanaume akizalisha bila ndoa anaoa vizuri tu ila mwanamke akizalishwa bila ndoa kuolewa ndiyo iwe kizaazaa?? Huwa nawaambia siku zote Mungu ni wa wote wanaume na wanawake na yeye ndiye anayepanga ndoa mtake msitake God is never unfair like humans na ndiyo maana haya malalamiko yenu hayajawahi kuisha humu mitandaoni wala huko mitaani na kamwe hayatakuja kuisha!!
 
Kuna muda huwa una points za maana.
Ni vile tu humu wanachekewa kukuoa.bibie.
Inawezekana ni kweli hajatumia akili kurudiana na baba watoto wake

Lakini kimsingi hakuna mwanamke mwenye akili timamu anayependa kuzaa na wanaume tofauti tofauti,halafu mapenzi yana nguvu kuliko akili
 
Kwa hiyo single mother hapo ni wewe au huyo shoga yako au ex wake au mume wake au watoto? Naombeni ufafanuzi kuhusu single mother.
 
Weekend tulivu kabisa ikianza.
Pia poleni na shughuli za week nzima.

Kuna watu waajabu sana ambao ukiwatazama unabaki kushangaa. Hivi unapata wapi ujasiri wa kumtukana/kushambulia single mother?

Jaribu kufanya utafiti binafsi usio rasmi kuchunguza huyo single mother anayesemwa kwenye mada na uhalisia uliopo.


Mwanamke huyu anapambana sana fahamu vizuri kuna jamaa kakimbia majukumu hapa na huyu mwanamke kayachukua kama yalivyo na kusonga nayo mbele.

Atapambana mwanae aishi vizuri kabisa na atajitahidi kwa hali na mali mtoto hasijisikie vibaya wala kuhisi kama hana baba.
Kama mtoto ataugua mwanamke huyu atapambana mtoto apate matibabu bora kabisa kwa gharama zozote zile.

Kama ni elimu, mtoto akifikisha umri wa shule atapelekwa vyema kabisa. Swala la sare na mahitaji ya mtoto ya kila siku atampambania mwanae.

Kama ni chakula na malazi, mtoto atapata vyote hivyo bila kupepesa macho japo mama anajikakamua kweli kweli maana kuna mbwa mmoja kakimbia majukumu.

Sasa wewe unaetoa maneno makali juu ya single mother hivi haya yote huwa unayaangalia kabla ya kumtukana na kumsimanga?

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni

Kumbuka kabla ya yote hayo kuna mtu aliona tayari kaharibu na hana alternative ndio maana kakimbia ila mwanamke huyu yeye kajifunga kilemba na kuanza kupambana na njia imeanza kuonekana wewe huku unakuja kutoa maneno machafu juu yake na kuwaanzishia nyuzi za kuwaandama.

Inaumiza sana kuwashambulia single mother kiasi hicho.
 
Back
Top Bottom