Wakinamama wanaolea watoto bila baba (single mothers): Sababu, athari kwa mtoto, changamoto na mitazamo ya jamii

Mkuu CONTROLA haya nayaita maamuzi ya mwanaume.
Tena bila kusahau kuwa asili hao watoto wawe wako kabisa 😆
 
Mkuu CONTROLA haya nayaita maamuzi ya mwanaume.
Tena bila kusahau kuwa asili hao watoto wawe wako kabisa 😆
Asanteeeeee

Safi kabisa hicho ndio kikubwa cha kufanya

ushenzi shenzi wa kuruhusu watu wawasiliane kumbe wanamegana

Mwisho unaachiwa nyumba,unarudi hukuti mtu

Unauliza yuko wapi anakujibu bila AIBU (nipo kwa baba flani)
 
Umeona ehh,huyo mwanamke kifupi ni kuwa hajitambui,wako wengi tu wa aina hiyo wanaorudia makando kando yao akiamni kuwa jamaa bado anampenda na mwisho wa siku wanaishia kutendwa tena.Umepata mwanaume anakuchukulia mapungufu yako,ukishaona vimetulia unamgeukia tena ex wako aliekwisha kukutenda,huo ni upuuzi uliopitiliza.Wasichotaka kujiuliza,kama ulikuwa mzuri kwake lakini hakukuoa,sasa hivi umebadilika nini mpaka akutake tena,ni series tu itaendelea atakupitia na hamu yake ikiisha utaachwa tena..
 
Nitaoa tu single maza kama aliyezaa naye alifariki na nimeoneshwa na kaburi.
 
Nyingi tuu nikiianza kuelezea ntajaza server za humu

Ila ndo hvyo Yule jamaa hayuko peke ake na wengi tunamuunga mkono sasa wewe endelea kuuliza maswali yako nyinyi Kama Nani
mwanaume ninaemuhunga mkono mwanaume mwenzangu Kwan kuna ulazima wa kujua mi ni nani haibadili ukweli
Nimewauliza hivyo ili nijue kwamba ninyi mkisema single mothers wasiolewe mnawaongezea nini au mnawapunguzia nini kwenye maisha yao ilihali wapo wanaume wenzenu wengi wanaojitambua wanawaoa kila iitwapo leo na ndoa zao zinadumu

Yaani ninyi wanaume wa humu JF na hizi kejeli zenu za kila siku kuhusu single mothers nilitegemea mkisema wanaume wasioe single mothers basi wanaume wote hapa bongo au kote duniani watafuata mitazamo yenu na pengine labda ipo siku single mothers wataacha kabisa kuolewa lakini wapi

Tatizo lenu wanaume huwa mnadhani Mungu ni wenu peke yenu na kwamba eti ndoa inapangwa na wanadamu!! Sasa kama anaruhusu wanaume wenye watoto waoe wanawake wasio na watoto kwanini asiruhusu wanawake wenye watoto waolewe na wanaume wasio na watoto??

Tena ukizingatia hao wala hawakujibebesha mimba wenyewe lakini mwanaume akizalisha bila ndoa anaoa vizuri tu ila mwanamke akizalishwa bila ndoa kuolewa ndiyo iwe kizaazaa?? Huwa nawaambia siku zote Mungu ni wa wote wanaume na wanawake na yeye ndiye anayepanga ndoa mtake msitake God is never unfair like humans na ndiyo maana haya malalamiko yenu hayajawahi kuisha humu mitandaoni wala huko mitaani na kamwe hayatakuja kuisha!!
 
Kuna muda huwa una points za maana.
Ni vile tu humu wanachekewa kukuoa.bibie.
Inawezekana ni kweli hajatumia akili kurudiana na baba watoto wake

Lakini kimsingi hakuna mwanamke mwenye akili timamu anayependa kuzaa na wanaume tofauti tofauti,halafu mapenzi yana nguvu kuliko akili
 
Kwa hiyo single mother hapo ni wewe au huyo shoga yako au ex wake au mume wake au watoto? Naombeni ufafanuzi kuhusu single mother.
 
Weekend tulivu kabisa ikianza.
Pia poleni na shughuli za week nzima.

Kuna watu waajabu sana ambao ukiwatazama unabaki kushangaa. Hivi unapata wapi ujasiri wa kumtukana/kushambulia single mother?

Jaribu kufanya utafiti binafsi usio rasmi kuchunguza huyo single mother anayesemwa kwenye mada na uhalisia uliopo.


Mwanamke huyu anapambana sana fahamu vizuri kuna jamaa kakimbia majukumu hapa na huyu mwanamke kayachukua kama yalivyo na kusonga nayo mbele.

Atapambana mwanae aishi vizuri kabisa na atajitahidi kwa hali na mali mtoto hasijisikie vibaya wala kuhisi kama hana baba.
Kama mtoto ataugua mwanamke huyu atapambana mtoto apate matibabu bora kabisa kwa gharama zozote zile.

Kama ni elimu, mtoto akifikisha umri wa shule atapelekwa vyema kabisa. Swala la sare na mahitaji ya mtoto ya kila siku atampambania mwanae.

Kama ni chakula na malazi, mtoto atapata vyote hivyo bila kupepesa macho japo mama anajikakamua kweli kweli maana kuna mbwa mmoja kakimbia majukumu.

Sasa wewe unaetoa maneno makali juu ya single mother hivi haya yote huwa unayaangalia kabla ya kumtukana na kumsimanga?

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni

Kumbuka kabla ya yote hayo kuna mtu aliona tayari kaharibu na hana alternative ndio maana kakimbia ila mwanamke huyu yeye kajifunga kilemba na kuanza kupambana na njia imeanza kuonekana wewe huku unakuja kutoa maneno machafu juu yake na kuwaanzishia nyuzi za kuwaandama.

Inaumiza sana kuwashambulia single mother kiasi hicho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…