Habari za jumapili ndugu zangu.
Kumekuwa na wimbi kubwa la kutokuolewa wanawake waliozalishwa na kukimbiwa na wanaume kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na wanaume wenyewe walowazalisha wanawake hao kuogopa majukumu ya kulea.
Kutokana na observation yangu niliyofanya nimegundua kwamba single mother wanazo sifa karibu zote za kuolewa ukilinganisha na wale ambao hawana watoto, nadhani hii ni kutokana na experience waliyoipata baada ya kuzalishwa hivyo automatically akili zao zinatulia,ila sasa kuna sababu kuu mbili ambazo nadhani ndizo zinazofanya washindwe kuolewa.
Nambari moja ni kwamba wanaume wanaogopa kwamba akioa single mother ipo siku atasalitiwa. Pili,Jamii inamchukulia single mother kama mwanamke malaya asiyejielewa au kujiheshimu, hii hupelekea wanaume wengi kuacha kuoa single mother kwa kuogopwa kusemwa na watu.
My take. Tuwaheshimu single mother, hatujui waliyopitia.