1. People are subjected to mistakes , kuna hili kundi wanapata mimba wakiwa bado wadogo kwasababu mbali mbali zinazowapelekea kuachwa solemba na waliowapa mimba. Mara nyingi hawa ni victims.
2. U poa poa, tuzae tuzae then what!
3.umalaya, mtu anajikuta amepata mimba na within fertility window alilala na 3 different men, akianza kuwashika mashati na akafanya kosa moja hawa wanaume wakagundua hakuna atakayekubali huyo mtoto (wanaume sio mafala kivile)
4. peer pressure, jamii imemuaminisha mwanamke lazima azae akifika umri fulani, wanawake wakiwa umri huo desperation level inakuwa juu sana. Wanaona kama sijaolewa ngoja tu nizae.
5. Kutembea na waume za watu, i swear ukitembea na mume wa mtu utaishia tu kuwa single mother, most men won’t leave their wives for mpango kando. Na hii ni sababu ya baadhi ya wanawake maisha yakiwashinda kitega uchumi pekee kisichohitaji investment ni kuzaa na mume wa mtu.
6. Women empowerment, Wanawake wakiwezeshwa wakaweza hawataweza kukaa kwenye ndoa za mateso, Hence wakiona wanateseka watavunja ndoa tu….
7. Umagharibi ; ile nazaa nitalea mwenyewe.
Katika haya yote kubwa ni mmomonyoko wa maadili, However wanawake tunatakiwa kubeba lawama katika hili, kwanza “most” of men hawapendi watoto (hawawezi kukiri) So watoto ni jukumu la mwanamke, Jitunze pata mume mzae muwajibike pamoja kulea watoto, Hakuna ubaya wowote katika kulea watoto katika complete family, kwanini tuopt fasheni nyingine ambayo imeprove tofauti? Usingo mother/father uwe kwa sababu ya majaliwa (kifo)
Waliotengeneza familia/ndoa kuwa taasisi-msingi kushinda taasisi zote hawakuwa wajinga, mkiwa ndoani/familiani mtawajibika tu hata kama hamtaki! Hence ustawi bora wa watoto.
Wanawake tukemeane kwenye hili, katika hili nisisikie adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzie blah blah . Jamii itageuka ya ajabu na hapa bado!