Dada habari Kwa majina naitwa ..... toka mbeya,mimi ni mzambia toka Lusaka kaka mimi dreva wa magari makubwa malori mimi nilioa binti yuko na mtoto kaka nimelea yule mtoto kama wangu pia na kumuanzisha shule na yule mtoto baba yake namfahamu
Sasa siku za karibuni hapa mimi nilirudi nyumbani pasipo kufanya mawasiliano na mwenzangu nilirudi nyumbani ghafla tu aliona sasa nikamkuta baba wa yule mtoto nikamuliza mwenzangu huyu kafwata nini alinijibu kwahiyo asije kumsalimu mwanae?
Mimi nikamuuliza mbona amuhudumii akanijibu hayakuhusu basi mimi nikaondoka maana niliwakuta mazingira sio mazuri wametoka kufanya tendo na mpaka niliamini tendo limefanyika nilimkuta kajifunika taulo langu yule mwanaume na mwanamke kavaa night dresses mimi nimeondoka wala sijamfanya kitu, nikachukua vitu vyangu vya muhimu nikaondoka vyombo nilimuachia kila kitu nilivyo beba vyeti vyangu na nguo zangu basi.