Superb2014
JF-Expert Member
- Jul 29, 2017
- 9,266
- 7,426
Huyo Kaka yako anatakiwa kuwa na msimamo kama huyo Mwanamke bado anaendelea na mahusiano na huyo Mwanaume aliyezaa nae ni bora Kaka yako aachane nae atafute Mwanamke mwingine.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Inawezekana kalogwa coz mwanamke yule ana maamuzi na ni mbabe.Hapo Shemeji anakosea sana kumkaribisha huyu mzazi mwenzie mpaka anapoishi!
Ni hivi mwambie brother aachane naye, kama huyu dada atakaa kumrudisha mtoto kwa baba yake.
Pia inawezekana huyu dada kmloga kaka yako, sio kawaida kwa mwanaume kuvumilia ujinga kama huo!
Kama kalogwa kuna uwezekano wa kumsaidia? Nilishaliwaza sana hiliHapo Shemeji anakosea sana kumkaribisha huyu mzazi mwenzie mpaka anapoishi!
Ni hivi mwambie brother aachane naye, kama huyu dada atakaa kumrudisha mtoto kwa baba yake.
Pia inawezekana huyu dada kmloga kaka yako, sio kawaida kwa mwanaume kuvumilia ujinga kama huo!
kamata, peleka kanisani, msikitini au kwa waganga wazuri wa kienyeji.. Sio kawaida hiiKama kalogwa kuna uwezekano wa kumsaidia? Nilishaliwaza sana hili
Hahaha, ume nifurahisha sana mkuu eti ni sawa na kubusu miguu ya nyuma ya punda..,Kuoa demu mwenye mtoto ilhali baba mtoto yuko chai, ni sasa na kubusu miguu ya Nyumba ya punda.
Mwambie aendelee kulia mpaka pale atakapo kua na kutengemaa kwa afya ya akili yake.Habarini watu wa Mungu
Utangulizi:
Kuna kaka yangu alioa (miaka kama mitano iliyopita) mwanamke aliyezaa na mwanaume tofauti na yeye. Hawajafunga ndoa na pia hawaishi pamoja kutokana na mambo ya kazi kwa pande zote mbili. Walishatambulishana kwa wazazi pande zote mbili na mahusiano yao ni ya uwazi na jamii inajua. Pia mwanamke anaishi na mtoto aliyezaa na mwanaume kabla hajaanza kuishi na kaka.... na huyo mtoto anasoma darasa la 2 sasa(7yrs). Kawaida br huenda kwa huyo mke kila ijumaa na kurudi jumapili jioni au jumatatu asubuhi sana na kupitiliza kazini kwake.
Tatizo lilipo
Ni kwamba mpaka leo mwanamke (shemeji) anawasiliana na mzazi wa mtoto wake (akiulizwa husema anawasiliana nae kwa sababu ya mtoto na kutuma matumizi na sio kimapenzi), na mara nyingine huja kumwona mwanae anapopata nafasi. Na kila anapokuja hamshirikishi kaka na akimuuliza hujibu tu alikuja bila taarifa kumwona mwanae na kwasababu anaishi mikoa ya mbali lazima alale hata siku 2 au 3. Na akimuuliza analalaje hapo na ataaminije kuwa hawafanyi mapenzi? Shemeji husema analala chumba cha housegirl na yeye analala na h/g.
Nimeandika hivi kwa sababu bro hii wiki hajaenda kwa mke kwa sababu kasikia yupo mzazi mwenzie na mke wake, na anakosaga sana amani, wikiendi yote kaishia kulewa tu. Mpaka sasa mwanaume bado yupo na br akitaka kuongea na mwanamke hana shida anaongea nae kwa uhuru lakini mi naona ni maigizo.
Kaniomba jana ushauri na anampenda kweli, nimeshindwa kutoa jibu ila nimemwambia amwambie mwanamke ampeleke mtoto kwa baba yake ili hiyo shida iishe kasema alishamwambia lakini shemeji anadai mtoto wake hawez kuishi kwa mama wa kambo. Na br mpaka sasa hajazaa nae.
Naombeni pia mawazo yenu, hali ya br sio nzuri kwa sasa
(Hanaga mpango na mitandao ya kijamii zaidi ya whatsapp so naamini hawezi kuona huu uzi).
.."amekunywa sumu, sasa ya nini kuombewa"Hauna kilio msiba wa kujitakia...!!!
Huyo bro bakora zinamhusuKaka ako nae anazingua kwa hiyo kaogopa kuenda kisa eti jamaa yupo seriously? Halafu anamruhusu vip huyo mwanamke amlaze kidume mwingine ndani kwake kwa nini asiende kulala lodge? Wanaume wengine wanaboa unaweza jikuta umemchapa bro ako vibao!.
majuto huja baadaeMwambie Kaka asione wivu wala roho kuuma sababu yeye pia hajaoa,afadhali aji sort mapema tena ana bahati kua ameshajua ni mwanamke wa aina gani,atafute mwanamke anae jielewa huyo amejua tabia zake na hata akioa huyo jamaa atakuja na wataonana na huyo mzazi mwenzie na ndio atamchefua zaidi, ajikaze kiume atafute mwengine maisha yaendele.
namba mojaNionavuo mimi,
1. Mtoto arudishwe kwa baba ake, au
2. Bro ako akubali kumlea Mtoto wake wankifikia ili jamaa azuiliwe kuja kwa kesi ya mtoto mara kwa mara, au
3. Aachane na huyo mwanamke
Kinyume na hapo, bro ataendelea kulia machozi ya samaki.