Wakinamama wanaolea watoto bila baba (single mothers): Sababu, athari kwa mtoto, changamoto na mitazamo ya jamii

Wakinamama wanaolea watoto bila baba (single mothers): Sababu, athari kwa mtoto, changamoto na mitazamo ya jamii

Habarini watu wa Mungu

Utangulizi:
Kuna kaka yangu alioa (miaka kama mitano iliyopita) mwanamke aliyezaa na mwanaume tofauti na yeye hawajafunga ndoa na pia hawaishi pamoja kutokana na mambo ya kazi kwa pande zote mbili walishatambulishana kwa wazazi pande zote mbili na mahusiano yao ni ya uwazi na jamii inajua.

Pia mwanamke anaishi na mtoto aliyezaa na mwanaume kabla hajaanza kuishi na kaka na huyo mtoto anasoma darasa la 2 sasa(7yrs) kawaida kaka huenda kwa huyo mke kila ijumaa na kurudi jumapili jioni au jumatatu asubuhi sana na kupitiliza kazini kwake.

Tatizo lilipo
Ni kwamba mpaka leo mwanamke (shemeji) anawasiliana na mzazi wa mtoto wake (akiulizwa husema anawasiliana nae kwa sababu ya mtoto na kutuma matumizi na sio kimapenzi), na mara nyingine huja kumwona mwanae anapopata nafasi na kila anapokuja hamshirikishi kaka na akimuuliza hujibu tu alikuja bila taarifa kumwona mwanae na kwasababu anaishi mikoa ya mbali lazima alale hata siku 2 au 3 na akimuuliza analalaje hapo na ataaminije kuwa hawafanyi mapenzi? shemeji husema analala chumba cha housegirl na yeye analala na h/g.

Nimeandika hivi kwa sababu bro hii wiki hajaenda kwa mke kwa sababu kasikia yupo mzazi mwenzie na mke wake, na anakosaga sana amani, wikiendi yote kaishia kulewa tu mpaka sasa mwanaume bado yupo na kaka akitaka kuongea na mwanamke hana shida anaongea nae kwa uhuru lakini mi naona ni maigizo.

Kaniomba jana ushauri na anampenda kweli, nimeshindwa kutoa jibu ila nimemwambia amwambie mwanamke ampeleke mtoto kwa baba yake ili hiyo shida iishe kasema alishamwambia lakini shemeji anadai mtoto wake hawezi kuishi kwa mama wa kambo na kaka mpaka sasa hajazaa nae.

Naombeni pia mawazo yenu, hali ya kaka sio nzuri kwa sasa

(Hanaga mpango na mitandao ya kijamii zaidi ya whatsapp so naamini hawezi kuona huu uzi).
I see kumbe duniani kuna watu wanaishi kinyonge sana eeeh?. Tena muda mwingine unyonge wa kujitakia. Mwanaume mwingine anakuja nyumbani kwangu alie na uhusiano na mke wangu. Halafu mwenye nyumba unaikimbia nyumba. Ushauri huyo mke anampenda huyo aliezaa nae,kwa kakaako amefuata ndoa tu,lakini mapenzi yote yako kwa mzazi mwenzie. Halafu kakaako ni dhaifu kwa,mkewe. Katawaliwa kifkra,ndio maana bila aibu kamleta mzazi mwenzie kwake na mumewe,na hivi tunavyoongea katundikwaa mimba ingine na huyo mwenye mtoto wa kwanza,lakini mtoto mtabambikiwa nyie . Mwisho hakuna namna mfungue kakaako huyo sio mke tena aachane nae leo hii,nisiwakute hapo
 
Huyo shemeji yako ni katili kwa kiwango hakisemeki!

hakuna mahali mwanadamu anakuwa na huo ujasiri kama hana nia ya uuaji dhidi ya huyo anayemfanyia!

Swala sio m toto kwenda kwa babake!
Swala ni kakako soon atajifia au kuuwawa!
HAKUNA MTU HAPO!
 
Aaaaand!
Hiyo nyumba mlimkuta nayo shemeji?
Ni ya kupanga?
muulize bro nani analipa kodi?
MY DEAR KAMA KODI ANALIPA MWANAMKE, VERY LIKELY ANALIPA HUYO BABA WA MTOTO!
katika hali ya kawaida kabisa!
HUO UJASIRI UNA LA ZIADA!
nakataa kuwa ni swala la kawaida!
 
Ninachokiona, mwanaume hana sauti kwa mwanamke na hana anachotoa nyumbani zaidi ya kula kulala.

Mke hujazaa nae unaruhusu mwanaume mwingine alale kwako dah. Huyu jamaa ni bwege

Kwangu nilishapiga marufuku hakuna mwanamke kuingia kwangu nikiwa sipo labda kaka wa mke wangu tu. Yeyote atakaefika ninaconnec dots. Wakutane hukooo siyo kwangu . yaani utafuniwe mke na tena utafuniwe kwako??? Dah ha ha haaa
 
Hili nalo linahitaji kuomba ushauri,kila kitu kipo wazi hapo ukiona manyoya ujue kashaliwa
 
Mpe pole kaka ako na umwambie pombe sio suluuhu
Aongee na mwanamke wake juu ya hiyo tabia..tena aongee akiwa anamaanisha maana wanawake akili zetu tunazijuaga wenyewe hasa kama hatujitambui

Muda ufike wanawake tuache endekeza wanaume tuliozaa nao jamani..kama umeamua kumove on ...move on sio kuumiza mtoto wa mwanamke mwenzio kwa kwa kisingizio cha mnalea mtoto na mzazi mwenzio
Aongee naye kitu gani?
Piga chini endelea na maisha mengine.
Nikikuchumbia maana yake uachane na ya zamani tuanze upya.
Huyo baba Kama anataka mtoto amchukue akakae naye huko.
Yaani mtu kashatolewa mahari anafanya ujinga wa hivi!!
 
Inawezekana kalogwa coz mwanamke yule ana maamuzi na ni mbabe.
Mpelekeni akaombewe ili huo ujinga umtoke, huyo shemeji yenu kamuwahi kaka yenu sasa huko aliko kwanini asitafute mke akae kimya amwambie aendelee na huyu mzazi mwenzie
 
Kaka ako nae anazingua kwa hiyo kaogopa kuenda kisa eti jamaa yupo seriously? Halafu anamruhusu vip huyo mwanamke amlaze kidume mwingine ndani kwake kwa nini asiende kulala lodge? Wanaume wengine wanaboa unaweza jikuta umemchapa bro ako vibao!.
Huyo kaka naye duu wanawake wengi hivi wanatafuta ndoa yeye anahenyeshwa hivyo duu angekuwa kaka yangu nimgemburuza mpaka kanisani namwambia Mchungaji siondoki naye mpaka akili yake iwe umerudi
 
Mwambie aendelee kulia mpaka pale atakapo kua na kutengemaa kwa afya ya akili yake.
Ila umwambie ukweli kua katka kundi la wanaume yeye hayupo kwa sasa [emoji16]
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Hapo bro wako bado hajamuoa kwa ndoa ndio maana huyo mwanamke anamletea huyo mwanaume ndani, akitaka aheshimiwe afunge nae ndoa rasmi na atekeleze wajibu wake kama mume, hutasikia huyo baba wa mtoto akijitokeza, ndoa inaheshima yake bwana
Hakuna kitu kama hicho kama hamjaoana ndiyo kipindi inaweza ficha ujinga wote, lakini kwa huyo wala mie simtetei amuacha tu aendelee na jamaa yake
 
Mpe pole kaka ako na umwambie pombe sio suluuhu
Aongee na mwanamke wake juu ya hiyo tabia..tena aongee akiwa anamaanisha maana wanawake akili zetu tunazijuaga wenyewe hasa kama hatujitambui

Muda ufike wanawake tuache endekeza wanaume tuliozaa nao jamani..kama umeamua kumove on ...move on sio kuumiza mtoto wa mwanamke mwenzio kwa kwa kisingizio cha mnalea mtoto na mzazi mwenzio
Huyo ni kahaba, bado wanapendana kuachana hawawezi, yeye atafute tu mwingine, hivi unamme ka ex kweli katakusogelea jamani
 
Back
Top Bottom