Kwanza unajua maana ya bikra?
Embu soma SEMANTIKI ili siku nyingine usijetia aibu humu ndani.
Siajabu nawe unakadigrii kako. Kweli elimu imeharibika.
Aina za Maana
Wataalam wengi mathalan Leech (1981) wanakubaliana kuwa kuna maana saba (7) kama ifuatavyo;
i. Maana ya Msingi
ii. Maana Dokezi
iii. Maana Mtindo
iv. Maana Hisia
v. Maana Tangamani
vi. Maana Mwangwi
vii. Maana Dhamira
MAANA YA MSINGI (DENOTATIVE MEANING)
Hii ndiyo maana kuu ya neno ambayo haibadiliki kutokana na mazingira.
Maana nyingine zote za ziada ambazo zinahusiana hutokana na maana hii ya msingi.aina hii ya maana huangaliwa na kufafanuliwa kwa kigezo cha kuwapo au kutokuwapo kwa sifa bainifu (distinction features) zinazokibainisha kitu hicho.
Sifa hizo baininifu katika taaluma ya semantiki huitwa vijenzi semantiki
Kwa mfano maana ya neno mwanamke linasheheni sifa bainifu zifuatazo::
+mtu
+mtu mzima
+ke
-me
Neno mwanamume nalo linasheheni sifa hizi bainifu:
+mtu
+mtu mzima
+me
-ke
MAANA DOKEZI (CONNOTATIVE MEANING)
Hii ni maana ambayo hudokezwa na kile kisemwacho na kuwakilishwa na kinachorejelewa na lugha.
Maana hii inapatikana kwa njia ya kitu fulani kuwakilisha au kudokeza kitu fulani kingine au hali nyingine.
Maana dokezi hutokana au huibuliwa.