Wakinamama wanaolea watoto bila baba (single mothers): Sababu, athari kwa mtoto, changamoto na mitazamo ya jamii

Wakinamama wanaolea watoto bila baba (single mothers): Sababu, athari kwa mtoto, changamoto na mitazamo ya jamii

Sasa ni andiko lipi linalosema wanawake ndiyo wawasaidie wanaume kuishinda tamaa yao?? Na nimeshakuambia kwamba vishawishi vipo na vitaendelea kuwepo sababu ndiyo vinavyopima imani na matendo ya wanadamu!!

Yaani ukisema eti wanawake waache kukaa uchi ni sawa na kusema Shetani aache kutujaribu wanadamu ili atupunguzie mzigo wa kutenda dhambi wakati Mungu ndiye kamruhusu lakini akatupa uwezo wa kumshinda ili kwamba kwenye hukumu kusiwe na watu watakaotoa visingizio vya kwamba eti shetani aliwapitia
Hapo umesema kweli, wanawake wamegeuka mawakala wa shetani. Ndio wanaotumika kumjaribu mwanamume, wakitoswa wanaliiiia wakati walikuwa wanatumikia matakwa ya bwana wao.

Andiko? Hili hapa:

1 Timotheo 2
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁹ Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;
¹⁰ bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.
 
Basi kama ambavyo siyo wanaume wote ni wacha Mungu pia vile vile siyo wanawake wote ni wacha Mungu sasa msiwashutumu wanawake wasio wacha Mungu tu na kuwaacha wanaume wasio wacha Mungu kana kwamba kumcha Mungu ni jukumu la mwanamke tu na siyo mwanaume
Mwanamke mcha Mungu na asiye mcha Mungu wote wana bikira. Wakiteleza tu kwenye uzinzi wataingia kwenye daraja ya single mother, hawatafaa kwa ndoa
 
Thatdumbgirl,

Ndugu mimi sio wa mtazamo finyu hivyo. Kwanza fanya toba, Mariamu mama wa Yesu hakuwahi kuwa single mother kiasi cha kuhitaji rehema za Mungu. Ni neno baya kabisa kuwahi kulisikia.

Kukemea dhambi hakuhitaji kubembeleza, ni neno moja kwa moja. Sipo hapa kukufurahisha, nipo kuisema kweli na kama unadhani unazo hoja za msingi, jibu kwa hoja sio maneno ya ujumla tu. Na hapa tambua sijashawishi mtu, nimeeleza matokeo ya mahusiano hayo. Ukipenda chukua ukipenda acha. Ni vema binti zetu kuepuka zinaa na kujizuia kww ajili ya ndoa, hiyo injili jumuishi piga wewe, mimi nasema kweli ya Mungu tu.

Halafu unasema ninayemhukumu ni mtoto, mimi nahukumu? Nimesema madhara ya kuoa single mother kwa vijana, sijaongelea mtoto. Mungu ameagiza tujitunze mpaka ndoa, sasa binti akiruhusu kuzalishwa nje ya ndoa atalipa gharama kubwa, upende usipende. Ukweli utawaweka huru, na ndio njia pekee ya kukinusuru kizazi kinachopotea.
 
Nyenyere, Kama ulivyoniletea hili andiko niletee na andiko lililosema mwanamke ndiye anayetakiwa ajitunze ili kumuokoa mwanaume, nasubiri.
 
Huna ujualo, unabaki kulalama tu
Wewe ndiyo hauna ujualo kwa sababu wewe mwenyewe umesema unaongea kweli ya Mungu tu ila nikikuambia uniletee andiko linalothibitisha hayo yote unayoyasema hauleti sasa hauoni kama hayo yanabaki kuwa maneno yako ya kutunga tu?? Labda utuambie unaongea kweli ya mungu yupi maana miungu iko mingi!!
 
Laana right?? Vipi na wale single mothers wanaohangaika na watoto peke yao hadi mwisho wa siku watoto wao wanakuja kufanikiwa kielimu na kiuchumi??

Halafu tusingewaona wanafiki kama mngekuwa mnawashutumu na hao wanaume wanaosababisha uwepo wa single mothers kwa sababu za kipumbavu
Na wakifanikiwa hao wanaume ndiyo wakwanza kupeleka videvu vyao kulia lia kwa watoto nakusema mama yake kamlisha sumu asinikumbuke Mimi Baba yake,huwa najiuliza hivi Baba anayejitambua anahitaji kujitambulisha kwa mtoto? Au mtoto anakuona Baba kwa matendo na kujua huyu ndiye Baba! Shida sana hii dunia
 
Na wakifanikiwa hao wanaume ndiyo wakwanza kupeleka videvu vyao kulia lia kwa watoto nakusema mama yake kamlisha sumu asinikumbuke Mimi Baba yake,huwa najiuliza hivi Baba anayejitambua anahitaji kujitambulisha kwa mtoto? Au mtoto anakuona Baba kwa matendo na kujua huyu ndiye Baba! Shida sana hii dunia
Wanaume huwa wanajiona wako innocent kwenye kila kitu yaani wao hawakosei kabisa na hiyo ndiyo shida yao kubwa
 
Back
Top Bottom