Wakristo na waislamu katika hili nani ni mkweli kati yenu?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,982
Reaction score
51,157
Wakristo wanasema Yesu alisulubiwa akafa akazikwa akafufuka akapaa mbinguni.

Lakini Waislamu wanasema Yesu hakusulubiwa hakufa hivyo hakufufuka. Wakati waislamu wanasema Yesu si Mungu wala mwana wa Mungu wakristo wanaamini vinginevyo.

Ukisikiliza stori zao kuhusu Ibrahimu Bado zinapishana pakubwa Sana. Nani ni mkweli kati yao?
 
Ukisikiliza stori zao kuhusu Ibrahimu Bado zinapishana pakubwa Sana. Nani ni wakweli kati yao?
Yesu wa Wakristo sio Issa wa Waislamu.
Upo ushahidi kadhaa wa historia nje ya biblia unamzungumzia kusulibishwa na kufa kwa Yesu Kristo.
 
Uislamu na Quran vimefanya Hila nyingi sana juu ya ukristo na Bible kwa ujumla. Kuna member mmoja humu aliandika thread "uislamu hausimami bila propaganda" nadhani anaitwa hamis77

Kuna namna waandishi wa Quran walifanya hila nyingi sana juu ya Biblia.

Mfano katika hili la kusulibiwa kwa Yesu na kufa acha habari za kufufuka kwake waliogopa kuliweka wazi kwa sababu Quran ingeingia huo mtego ingekubali Msalaba ambao ndiyo msingi wa ukristo.

Ukristo hausimami bila Msalaba. Huo ndiyo ukweli. Hakuna ukristo bila yesu kusulibiwa,kufa na kisha kufufuka.

Ukisoma maelezo ya Quran ni kama Mungu wa kwenye quran aliogopa yesu asiteswe na hatimaye akamnyakua kumuepusha na matukio yote ambayo Biblia iliendelea nayo hadi kifo na hatimaye kufufuka.

Hata tukio la nani Ibrahim alitaka kumtoa kama dhabihu ukisoma Biblia na Torah ya wayahudi unaona Mungu alitaka kumjaribu Ibrahim kwa mtoto wa pekee na mkewe Sara (mke halali) ambaye Ibrahim alimpenda kuliko chochote. lakini inapokuja simulizi za Quran katika hilo hilo la kuchinja unaona anayetolewa kafara ni mtoto wa nje ya ndoa Ambae kwenye Mila za kiyahudi naashariki ya kati kwa ujumla mtoto wa nje ya ndoa anaonekana kama Hana thamani.

Hapa ukweli halisi upo kwenye kitabu cha kale zaidi ambacho ni Torah ya wayahudi dini ambayo yesu aliikuta na kisha Biblia ambazo zote zinasimulia aliyetolewa dhabihu/kafara/kuchinjwa ni mtoto wa Sara na si Ishmael(Ismail) mtoto wa nje.

Quran imeweka propaganda kwa sababu ilijua mwendelezo wa uzao wa yule mtoto wa nje ya ndoa ilikuwa ni waarabu. Ikajimegea minyama.

Uwepo wa vile Quran ilivyoandikwa Biblia na Torah ya Jews vimechangia kwa kiwango kikubwa sana.

Mbaya zaidi wale wale Wana wa ukoo wa Yuda(wayahudi) ambao wametoa manavio wengi,Quran imekuja kuwasema kama ni waislamu.

Hii ni hila ya waziwazi kwa dini ya uyahudi na kisha mtoto aliyetoka ubavuni mwa uyahudi wambae ni ukristo.

Wayahudi wao walikubali hili tukio la yesu ila wakasema wanafunzi wake walimwiba. Hajafufuka kama ilivyosemekana.
 
Wakristo wanasema Yesu alisulubiwa akafa akazikwa akafufuka akapaa mbinguni.

Lakini Waislamu wanasema Yesu hakusulubiwa hakufa hivyo hakufufuka. Wakati waislamu wanasema Yesu si Mungu wala mwana wa Mungu wakristo wanaamini vinginevyo.

Ukisikiliza stori zao kuhusu Ibrahimu Bado zinapishana pakubwa Sana. Nani ni wakweli kati yao?
NIMEJISIMIKA RASMI UUNGU. KWAANZIA LEO MIMI NI MUNGU WENU LAZIMA MNIABUDU. HAYA INAMISHENI MIBICHWA YENU CHINI NA VIJAMBIO VYENU JUU NA MSEME KWA PAMOJA LOOSE NUT AKBAR!

KENGE NYIE

adriz
 
Ndugu mabishano ya kidini hayanaga muafaka hasa zinapokutana hizo dini mbili
Ukitaka kujua Yesu na Issa ni watu wawili tofauti muulize muislamu yoyote yule
1. Yesu ni Issa?
2. Nitajie wafuasi (wanafunzi) wa Issa?
Majibu yote utakayoyapata kutoka kwa muislamu yatakuwa kutoka kwenye Biblia na siyo Quran. Hapo hapo muislamu anaamini Biblia imechakachuliwa ila ataitumia hiyo hiyo Biblia kukuelezea kuhusu Issa
 
Wakristo wanasema Yesu alisulubiwa akafa akazikwa akafufuka akapaa mbinguni.
Wakristo wanaweza kuwa Wakweli kwani Stori Yao imesukwa tangu mwanzo ikilenga mwisho(target) kama ni uongo tunasema uongo wenye mashiko au uliokubalika.

Waislam kwenye kipengele hiki Stori Yao inaning'inia na haina msuko wa uhakika.

Lakini Waislamu wanasema Yesu hakusulubiwa hakufa hivyo hakufufuka. Wakati waislamu wanasema Yesu si Mungu wala mwana wa Mungu wakristo wanaamini vinginevyo.

Ukisikiliza stori zao kuhusu Ibrahimu Bado zinapishana pakubwa Sana. Nani ni wakweli kati yao?

Waislam na Wakristo wote sio Wakweli.
Kwa sababu ni second na third-party.

Wayahudi hao ndio wakujadili
 
Biblia na Wakristo wanamjua Yesu. Jina hilo kwenye kiswahili lilitoholewa kutoka Yeshua au Yasoos kwa Kigiriki, au Gesu kwa Kirumi.
Quran ina Isa, jina tofauti kabisa. Hiyo inaonesha kuwa Isa wa Quran siyo Yeshua wa Biblia. Yesu wa Biblia, alikufa msalabani, alifufuka siku ya tatu, akapaa mbinguni akiwa mbele ya watu. Hizo ni accounts za mashuhuda wa omani ya Kikristo na wasip wakristo. Biblia inajitegemea, na wala haihitaji kulinganishwa na kitabu kingine chochote.
 
Uislamu na Quran vimefanya Hila nyingi sana juu ya ukristo na Bible kwa ujumla. Kuna member mmoja humu aliandika thread "uislamu hausimami bila propaganda" nadhani anaitwa hamis77

Kuna namna waandishi wa Quran walifanya hila nyingi sana juu ya Biblia.

Mfano katika hili la kusulibiwa kwa Yesu na kufa acha habari za kufufuka kwake waliogopa kuliweka wazi kwa sababu Quran ingeingia huo mtego ingekubali Msalaba ambao ndiyo msingi wa ukristo.
Watu walikua wakisulibiwa tu kabla hata yesu hajazaliwa na Maryam,na kanisa lilianza kutumia msalaba kama alama miaka 300 baada ya yesu kuondoka,usimtishie mchawi msalaba hauna chochote, msalaba upo kwenye maahua,madirisha
Ukristo hausimami bila Msalaba. Huo ndiyo ukweli. Hakuna ukristo bila yesu kusulibiwa,kufa na kisha kufufuka.

Ukisoma maelezo ya Quran ni kama Mungu wa kwenye quran aliogopa yesu asiteswe na hatimaye akamnyakua kumuepusha na matukio yote ambayo Biblia iliendelea nayo hadi kifo na hatimaye kufufuka.
Yesu si aliomba,baba ikiwezekana niepushe na kikombe hiki..na bible inadai yesu akiomba hakataliwi
Hata tukio la nani Ibrahim alitaka kumtoa kama dhabihu ukisoma Biblia na Torah ya wayahudi unaona Mungu alitaka kumjaribu Ibrahim kwa mtoto wa pekee na mkewe Sara (mke halali) ambaye Ibrahim alimpenda kuliko chochote. lakini inapokuja simulizi za Quran katika hilo hilo la kuchinja unaona anayetolewa kafara ni mtoto wa nje ya ndoa Ambae kwenye Mila za kiyahudi naashariki ya kati kwa ujumla mtoto wa nje ya ndoa anaonekana kama Hana thamani.
Isaka hawezi kuwa mtoto wa pekee wakati Ibrahim alikua na mtoto wa kwanza Ismail,tumia akili ndogo tu, Sheria hata ya kiislam inaruhusu kumfanya mtumwa wako kuwa mwana ndoa mwenzio..ndiyo maana bible inamtambua Ismail kama mwana wa Ibrahim na Mungu akaahidi kumbariki mwanao Ishmael
Hapa ukweli halisi upo kwenye kitabu cha kale zaidi ambacho ni Torah ya wayahudi dini ambayo yesu aliikuta na kisha Biblia ambazo zote zinasimulia aliyetolewa dhabihu/kafara/kuchinjwa ni mtoto wa Sara na si Ishmael(Ismail) mtoto wa nje.
Ibrahim hakuwa myahudi,hakufuata Sheria za kiyahudi,una uhakika hayo maandishi hayana ushawishi wa wivu waliokua nao upande wa isaka?
Quran imeweka propaganda kwa sababu ilijua mwendelezo wa uzao wa yule mtoto wa nje ya ndoa ilikuwa ni waarabu. Ikajimegea minyama.
Waarabu walikuwepo tu, Ibrahim ni mtu wa Iraq
Uwepo wa vile Quran ilivyoandikwa Biblia na Torah ya Jews vimechangia kwa kiwango kikubwa sana.

Mbaya zaidi wale wale Wana wa ukoo wa Yuda(wayahudi) ambao wametoa manavio wengi,Quran imekuja kuwasema kama ni waislamu.
Uislam maana yake ni kujisalimisha kwa mwenyezi Mungu mmoja muumba wa kila kitu hafanani na chochote, ndiyo Mila ya Ibrahim
Hii ni hila ya waziwazi kwa dini ya uyahudi na kisha mtoto aliyetoka ubavuni mwa uyahudi wambae ni ukristo.
Yesu aliamini Mungu mmoja tu na yeye ni nabii tu
Wayahudi wao walikubali hili tukio la yesu ila wakasema wanafunzi wake walimwiba. Hajafufuka kama ilivyosemekana.
Quran haikatai tukio la mtu kusulubiwa bali inasema Allah aliwabadilishia mtu mwingine,so tukio lilikuwepo
 
Watu walikua wakisulibiwa tu kabla hata yesu hajazaliwa na Maryam,na kanisa lilianza kutumia msalaba kama alama miaka 300 baada ya yesu kuondoka,usimtishie mchawi msalaba hauna chochote, msalaba upo kwenye maahua,madirisha

Yesu si aliomba,baba ikiwezekana niepushe na kikombe hiki..na bible inadai yesu akiomba hakataliwi

Isaka hawezi kuwa mtoto wa pekee wakati Ibrahim alikua na mtoto wa kwanza Ismail,tumia akili ndogo tu, Sheria hata ya kiislam inaruhusu kumfanya mtumwa wako kuwa mwana ndoa mwenzio..ndiyo maana bible inamtambua Ismail kama mwana wa Ibrahim na Mungu akaahidi kumbariki mwanao Ishmael

Ibrahim hakuwa myahudi,hakufuata Sheria za kiyahudi,una uhakika hayo maandishi hayana ushawishi wa wivu waliokua nao upande wa isaka?

Waarabu walikuwepo tu, Ibrahim ni mtu wa Iraq

Uislam maana yake ni kujisalimisha kwa mwenyezi Mungu mmoja muumba wa kila kitu hafanani na chochote, ndiyo Mila ya Ibrahim

Yesu aliamini Mungu mmoja tu na yeye ni nabii tu

Quran haikatai tukio la mtu kusulubiwa bali inasema Allah aliwabadilishia mtu mwingine,so tukio lilikuwepo
Kutokana na maelezo yako Yesu siyo Issa. Eti Ishmael ha ha ha ha ha ha ha bila kujua lugha ya kiirabu wewe bado humjui Allah sasa ili uwe muislamu lazima ufuate nguzo za uislamu. Sasa huyo Ibrahimu na Ishmael walikuwa wanafuata nguzo gani? Allah anasikia lugha moja tu kiiarabu na lazima utumie kiarabu kusoma kitabu chake sasa Ibrahim alikuwa anatumia lugha gani?
1. Hivi Issa ni Myahudi au ni mpalestina?
2. Kwa nini Qurani haikatazi kutumia vitu na bidhaa za makafiri?
3. Nitajie wanafunzi au wafuasi wa Issa?
 
Wakristo wanasema Yesu alisulubiwa akafa akazikwa akafufuka akapaa mbinguni.

Lakini Waislamu wanasema Yesu hakusulubiwa hakufa hivyo hakufufuka. Wakati waislamu wanasema Yesu si Mungu wala mwana wa Mungu wakristo wanaamini vinginevyo.

Ukisikiliza stori zao kuhusu Ibrahimu Bado zinapishana pakubwa Sana. Nani ni mkweli kati yao?
Ukiamini Wakristu na Waislam hawaamini Mungu mmoja wala hutaona shida ya hizi tofauti.
 
Back
Top Bottom