Wakristo tujitafakari upya taratibu zetu zote za mazishi. Kuna mambo hayako sawa

Hapana mkuu hayo huwa yanatokea sana ili kupunguza sooo, lakini hiyo haitakuwa Misa bali itakuwa ibada tu! Na hili huwa linatokea kwa mfano mtu aliyefiwa yeye ni mshiriki mzuri wa mambo ya Kanisa ila marehemu ndio hivyo alikuwa amejifungia masakramenti, sasa hapo baraza la walei linaona ni vyema ikaendeshwa ibada kwa ajili ya mfiwa. Hivyo ibada hiyo huwa fupi sana na haifuati ule utaratibu wa mazishi ya kawaida ya Kikristo.
 
Mkubwa humzika mkubwa mwenzake. Mdogo huzikwa na yeyote mwenye mamlaka ya kuzika.
 
Hakuna ubaya wowote. Siku ya kusimikwa kwa Askofu yeyote wa RC, imekuwa ni utamaduni kuona Rais wa nchi anahudhuria sherehe na misa hiyo. Sasa kwa heshima hiyo hiyo, Rais mstaafu wa nchi anazikwa na misa inayoongozwa na Askofu, tena si mmoja, hata wanne
 
Inategemeana na, Ntu na Ntu" Wenzetu wanazikwa hata na Sheikh Mkuu! Dah hii Dunia hii....
 
Ni mgawanyo tuu..
Askofu wa iringa aliongoza misa ya kawaida siku ya kwanza.
Misa maalumu ya kumuaga iliongozwa na askofu wa dar ruwaichi..
Pia misa ya mwisho kwao masasi iliongozwa na askofuu wake filbert mhasi ambaye ni askofu wa masasi pa1 na rais wa baraza la maaskofu katoliki tz
 
Peponi ndio wapi? Tuanzia hapo kwanza, binadamu ni kama mnyama au majani, jani likikauka na kuoza ni mbolea kwa mimea mingineyo.

Huko Peponi hakujai? Huo uwanja wa parapanda ikilia siupatii picha utakuwaje maana Tangia tuambiwe kuhusu akina Zinjanthropus mpaka kizazi hiki cha kina Lisu sipati picha wameishi binadamu wangapi.

Jiulize tu, Noah eti alitengeneza safina iliyobeba wanyama na viumbe wote kwa pair, Watu walimsusia akatengeneza yeye mwenyewe na Familly yake, huo uwanja walipolitegesha ilo safina from the scratch mpaka linaisha kwangu haimake sense, labda kuwe na story mbadala wake kama ile ya kula tunda mtaani tunaambiwa ni kugegedana.

Mafundisho mengi ni mind control tu hamna kitu. Sali sana utakufa tu, kuwa chinjachinja utakufa tu, toa sana sadaka bado utakufa tu. Jifunzeni wanyama pori mfano ambao nao ni viumbe wa Mungu, Simba anakula Swala na yeye akiotewa na manyamela kina fisi analiwa vizuri tu. Mungu tu ndio ataishi milele.

Usiniambie eti sisi ni bora kuliko wanyama, utakuwa umechanganyikiwa, kata miti na mimea yote itowayo Oxygen uone kama wewe ndio bora sana, ondoa nyuki uone kama wewe utatengeneza asali.

Far from mental slavery.
 
Kama vidole tu, havipo sawa. Hili halikwepeki. Si waona hata marais wakija hapa kwetu inavyokua....akija Bush/Obama/Trump na akija M7 au Kagame au Kenyatta....mapokezi huwa tofauti sana. Sifikiri kama umesahau baadhi ya barabara kupigwa deki....

But all in all, nakubaliana na hoja yako, ubaguzi upo na hautaisha...pengine hata wewe ungekuwa mfanya maamuzi, pengine usingeamua tofauti.......yaani Rais azikwe na katekista kama sie makapuku huku? Kweli? Hata ibadani kanisani tu, viongozi na wenye pesa wana sehemu zao!
 
Afadhali umesema Baraza la Walei. Uzuri katiba ya Walei (matoleo yote) imeweka wazi tafsiri ya Walei. Padri na Katekista wanaangukia katika kundi la Makleri (Clergy), hawa sio Walei (Laity) . Walei ni waumini ambao wanaongozwa na Kamati Tendaji inayoundwa na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu, Katibu Msaidizi na Mtunza Hazina wa ngazi yoyote kuanzia Taifa, Jimbo, Parokia na Jumuiya
 
Kuna wakatoriki na Kuna walokole nk wote hao ni wakristo,
ila ulipomtaja padri kwa mazishi ya kapuku then ukataja askofu kwa mazishi ya kibosile basi nkajua ulikuwa Lupaso wewe 😂😂

Hapo kanisa catholic limehusika ni utaratibu wao kiongozi mkuu wa kanisa kuendesha mazishi,
ila kwa upande wa makanisa ya kulokole ama yale yanayofuata injili halisi ya yesu Kristo hayanaga huo ubaguzi ktk mazishi.
 
Una hoja ya msingi
 
Mleta Maada ana hoja ya msingi sana, Muumini wa kawaida sana akifariki hata Padri unaweza usimuone kwenye ibada, akifa muumini aliekuwa ba jina basi Padri utamuona, akifa muumini mzito kabisa utamuona askofu.

Hii ni kwa makanisa yote ukitoa Waislam
Hata kwa taasisi zisizo za kidini huwa mambo yapo hivyo...
 
Shida yake ni kuzikosoa taratibu za kikatoliki tu... anasahau KAFA Rais tena mstaafu tumetangaza maombolezo wiki... wangapi wanakufa na tunapiga kimya kitaifa..!? Kafa Rais mstaafu wa TZ, LAKINI Kenya wamepandisha bendera nusu mlingoti...

Alikufa baba wa taifa mwaka 1999 Tuliomboleza mwezi mzima.. hajahoji....

Kijamii tuna madaraja ambayo tunayakubali na hakuna wa kulalama... wengine hapa hata kwenye bia, nikanunue bia moja 5,000/- wakati naweza nikakaa sisimizi bar na nikainywa bia hiyo hiyo kwa 1,500/- ..!! Na wala silalamiki kwanini mwingine anaenda huko wanakouza bia 5,000/-..!!
 
Unanikunbusha mbali kuna kipindi fln between 2006 hv kuna mtu ambae alikuwa mkurugenz wa halmashaur sas alipo fariki alikuja kuzikwa ama tuseme ibada iliendeshwa na mwinyilisiti watu wakawa wanaoji kwanin mwinyilisiti amzike mzee huyu badal ya askof Thoma laizer ..ikasemekana kwamba mkurugenzi Yule alikuwa cyo mtoaji kanisani kbsa hvyo alivyokufa wakamteuwa mwinjilist akazike. ...kwa kweli huna kitu pesa hudhaminiki hat ukiifa uwenda ukazikw na katekista
 
Tena wakati mwingine katekista anakatazwa...

Kuna wakati katekista anakwenda kuendesha ibada ya mazishi kutokana na Padre kutopatikana.. mfano kasafori.. au kahushuria msiba au jambo jingine.. na kuna Parokia zina vigango vingi.. huwezi mpeleka Padre kwenye kila kigango kufanya ibada ya mazishi, hivyo makatekista hufanya wao ibada hizo
 
Siyo utoaji pekee.. ni ushirili wa mambo ya kanisa.. kwa mfano, kwenye ukatoliki... mtu hushiriki jumuiya, hushiriki usafi wa kanisa wakati wa zamu yenu, hutoi zaka, hutoi sadaka, husali misa yoyote... ETC HALAFU UNATAKA UPEWE HUDUMA YA KIKANISA KAMA MSHIRIKI KAMILI...

Hivi nyumbani kwako mtoto mtukutu huwa unamfanya nini ..!? Unampa kila kitu sawa na mtoto mwema.
!? Hamkuwa mnapewa zawadi mkifaulu shuleni na wengine wakaachwa..!?

TUACHE UWONGO... hata wewe mtu anataka umsaidie lakini anakuja na matusi mateke na mangumi, utatoa msaada..!? TUWE WAKWELI WA NAFSI
 
Yule Ngalekumtwa wa Iringa ndo mkuu wa Baraza la maaskofu TEC ( Sijui anaitwa Rais wa TEC/mwenyekiti)

Kwa maana hiyo ndio kiongozi wa Maaskofu wote wa Katoliki Tanzania

Sio kweli
 
Wachangiaji wengi wa uzi huu hawajui lolote , wengi ni washabiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…