R-K-O
JF-Expert Member
- Jun 27, 2023
- 482
- 2,178
Kuvunja ndoa ya kikristo ni mpaka kifo ama kuchepuka, Kwanini wakristo hawatii sheria zao wanakimbilia mahakamani kuvunja ndoa kwa sababu zingine?
-Mke au mume wako ni mwema kabisa tabia njema wala hana tatizo, mara paap! Kapata kazi huko Marekani, likizo yake ya kurudi ni wiki 2 tu mwaka mzima,
- Mke au mume wako ni mwema kabisa tabia njema, mmeoana mkiwa vijana wadogo, baada ya siku kadhaa mwenzako kakamatwa kwa kesi ya mchongo anahukumiwa jela kifungo cha maisha,
- Mke anakunyima unyumba mwaka mzma, ulikula kiapo muishi wote no mara waaaa! Hakuna kiapo kilisema muachane kisa tamaa yako ya kufanya mapenzi imekuzidi, kwanini msivumiliane mpaka kifo
- Maningia kwenye ndoa unakuja kupata habari mke wako alishatoa mimba tano, mmekaa miaka sita hakuna mtoto, kwanini msivumiliane mpaka kifo
- Mke anachukia ndugu na mama wa mme wake, anamtukana mama yako, uliapa kwamba mtaachana hadi kifo, kwanini msivumiliane mpaka kifo
Na kama kuna kanisa linavunja ndoa nje ya hizo sababu basi ni wazi hawaheshimu dini yao.
Huko mahakamani kumekuwa kimbilio la kwaristo wengi kuvunja ndoa kwa sababu zingine kabisa nje ya hizo mbili.