quran imenyooka kaisome usikubali kuambiwa kitu ukakibeba jujuu utaumbuka.Izo santanic verses qurani haina ujinga wenu huwo
nimesoma na kuelewa ndio maana nimeandika na sijasimuliwa na mtu yeyote hebu nikuulize ni kweli kwamba kuna Bbwawa au Ziwa la Moto ambapo jua huwa linazama?
Quran 18:86 "Hata alipofika machweo ya jua, alikuta linazama katika chemchemi yenye matope." Sasa kama sio uwongo kuna chem chem ya matope ambapo jua linazama?
Aisha aliripoti kuwa mbuzi (au kondoo) aliingia nyumbani kwake na kula kipande cha ngozi kilichoandikwa aya kuhusu kupiga mawe wazinzi na kunyonyesha watu wazima mara kumi. Hadithi hii imeandikwa katika
Sunan Ibn Majah na mara nyingi hutajwa katika mijadala kuhusu aya ambazo hazipo tena kwenye Qur'an:
"Aya ya kupiga mawe na ya kunyonyesha mtu mzima mara kumi iliteremshwa, na karatasi hiyo ilikuwa nami chini ya mto wangu. Alipofariki Mtume wa Mwenyezi Mungu, tulikuwa tukijishughulika na kifo chake, kisha mbuzi akaingia na kuila." Je Allah angekubali Quran yake iliwe na mfugo?
Kukusanywa na kuchomwa Quran kunatia Mashaka kwamba kwama Quran ya kwanza ilikua kamilifu je kipi kiliingiza uharibifu na je ipi ni sahihi ya zamani au mpya ? soma:
Wakati wa ukhalifa wa Uthman bin Affan, kulikuwa na wasiwasi kuhusu tofauti katika usomaji wa Qur'an miongoni mwa jamii za Waislamu. Ili kutatua tatizo hili, Uthman aliagiza kukusanywa kwa toleo lililoratibiwa kwa mujibu wa maandishi yaliyokuwa mikononi mwa Hafsah, mmoja wa wake wa Mtume Muhammad. Kisha akaamuru nakala zote zisizo rasmi na vipande vingine vyote vya Qur'an vichomwe moto ili kuzuia migogoro kuhusu maandishi hayo:
"Uthman alituma ujumbe kwa Hafsah akisema, 'Tutumie maandishi ya Qur'an ili tuweze kuyakusanya kuwa nakala kamilifu... na akaamuru kuwa nyenzo zote nyingine za Qur'an... zichomwe.'"
Inaripotiwa kuwa Khalifa wa pili, Umar ibn al-Khattab, aliwahi kukumbuka aya kuhusu kupiga mawe (rajm) ambayo iliteremshwa wakati wa uhai wa Mtume Muhammad lakini haipo tena kwenye Qur'an. Alionyesha wasiwasi kwamba vizazi vijavyo vinaweza kusahau hukumu hii muhimu kutokana na kutokuwepo kwa aya hiyo katika maandishi ya Qur'an:
"Ninauogopa wakati utakapopita kwa muda mrefu, watu wanaweza kusema, 'Hatuoni Aya za Rajam (kupiga mawe) katika Kitabu Kitakatifu,' na kwa sababu hiyo wanaweza kupotea kwa kuacha wajibu ambao Allah ameufunua."
Swali ni kwamba kwanini Allah aruhusu Quran yake isahaulike tena katika Aya Muhimu ya kupiga mawe mpaka kufa? na kama ni hivyo ni ngapi zimesahaulika na ni ngappi za uwongo zimeingizwa katika Quran ya sasa.
Hiyo ni sehemu tu ukitaka nyingine nitakuletea uache kukariri.