uislamu mafundisho yake umejaa makasiriko na vitisho vingi
Mkuu, karibu kwenye ukumbi! Maadamu tunajifunza ni busara kuweka na ushahidi. Tusaidie ushahidi tafadhali!
uislamu sehemu kubwa unafundisha chuki na mauaji
Tusaidie ushahidi na hapa Mkuu ili tuendelee zaidi kujifunza kutoka kwako Mkuu!
uislamu unawadharau sana wanawake unawaona wapo kwa ajili kutomb...wa tu na hawana maana yeyote katika dunia hii( refer stori za mtume na kuoa mtoto wa miaka 9 pia refer bunge la Iraque nini limekifanya siku za hivi karibuni)
Na hapa pia, tusaidie ushahidi tafadhali ili kumbukizi kama hizi tuziweke sawa!
uislamu umejaa ubaguzi kwa wasio waislamu ( japo waislamu wa Tanzania na Senegal pongezi kwenu hili hamjalizingatia sana) ukitaka kuamini nenda Somalia,Northern Nigeria, Chad n.k utaamini haya ninayoyasema)
Halikadhalika, hapa napo tusaidie ushahidi Mkuu ili tuzidi kuneemeka na maarifa yako!
wachina hawataki kuisikia hiyo dini
Mchina si kwamba hataki uislamu bali dini yoyote! Wachina wameingia mtafaruku na kanisa katoliki kwa muda mrefu. Utaratibu wa kanisa ni kuchagua mwakilishi wao ambaye atakuwa anahudumu kwa niaba yao akiwemo China. Serikali ya China haitaki hilo! Imemchagua kuongozi wao wenyewe ndiye ambaye atahudumu China kwa niaba ya Catholic. Nukta yake: Wengi sana majasusi na wanatumikia sana kanisa kuliko nchi yao!
wahindi hadi leo wanaipigania kashmir dhidi ya waislamu wa pakistan
Hufahamu mpaka leo mgogoro uliyopo baina ya wahindi (Hindu stan) na wapakistan? Hufahamu kuwa ilikuwa nchi moja? Hufahamu tangu mwaka 1947 nchi ilivyojigawanya na kuwa nchi 2 tangu hapo uhasama wao ulianza kugombania hilo eneo Mkuu?
msumbiji haina hamu na hao watu
Mkuu, na hili kweli hulifahamu? Mbona kuna Uzi ulianzishwa juu ya hili? Hufahamu Wagner waliajiriwa na serikali ya Msumbiji kupambana nao ila waliondoka? Sababu kubwa hao magaidi wanashirikiana na serikali kwa vurumai za ndani ya nchi yao?
Kwa ufupi ni mradi wa wakubwa! Maeneo ya huko yana mafuta mengi. PDF zipo, ikiwa kama unahitaji kuzisoma usisite kuniambia tutasaidiana kukupatia.
mashariki ya kati ndio usiseme
Mkuu, ni kweli hufahamu kinachoendelea mashariki ya kati? Syria sababu Bashar Al Assad kukataa kupitisha bomba la mafuta na gesi kutokea Qatar ambalo lilikuwa linasimamiwa na US na washirika wake. Lengo kuu lilikuwa kumdhoofisha kiuchumi Russia kwa nchi za Ulaya zisiwe moja kwa moja zinamtegemea Russia. Ndiyo maana Russia aliingia mazima kumsaidia Assad.
Palestina na Israel wanagombania mipaka ya nchi na kila siku wana maazimo yao baraza la usalama wa Taifa yapo!
Yemen ni kugombania madaraka, rais hatakiwi na raia ila Marekani na Saudia wanamtaka kumbakisha madarakani. Hiyo ndiyo sababu ya ugomvi!
Iraq inafahamika iliingia vitani na USA kwa kutolewa sababu zisizokuwa na ushahidi kuwa wanamiliki silaha za maangamizi. Baraza la Usalama wa Taifa lilikataa azimio la USA kwani halikuona ushahidi lakini USA aliivamia hivyo hivyo!
Na ndiyo maana Tony Blair aliomba msamaha kwa kusema taarifa za kiusalama ziliwapotosha!
ulaya na marekani hawana hamu na hawa watu tangu wawakaribishe
Mbona hao watu Uholanzi wapo, Germany wapo, UK wapo, Italy wapo! Ulaya ipi Mkuu?
Na Marekani wapo! Mwisho wa campaign ya Trump na K. Harris si wamemalizia kwenye majimbo yanayokaliwa na raia wengi wenye asili ya ME, na wakatoa ahadi ya kumaliza vita ya Palestina na Israel? Marekani ipi haiwataki Mkuu?