Umewahi kumsoma Cornelio? Yesu kafafanua vizuri kwamba kimuingiacho mtu hakiwezi kumtia unajisi maana chatoka kwenda chooni (Chakula), Bali kimtokacho mtu (mawazo) ndicho chaweza kumtia mtu unajisi.
Lakini pia imeshauriwa kuacha kula Kama kufanya hivyo kutamchukiza ndugu yako.
Yale Yale mnasoma Biblia Kama Gazeti , pia mnategemea kina Mwamposa,Gwajima ndio wawatafsirie Biblia ,mtapotea
Ishu ya Kornelio ,Ni Ndoto Kuhusu wayahudi(wasafi) na wamataifa(Najisi)
Nyie kwa Uroho wenu mmegeuza kichaka Cha kula mbwa,kenge,Mende,konokono,Nguruwe
NAOMBA NITOE ILO ANDIKO NA KUFAFANUA ,JAPO INAWEZA KUWA NDEFU ,NIWIE RADHI
#ALIVYOVITAKASA_ MUNGU_ USIVIITE_ WEWE_ NAJISI. #Matendo 10:15
Nawasalimu kwa jina la BWANA WETU YESU KRISTO.
Maono aliyooteshwa Petro mara nyingi yametumiwa na baadhi ya watu kuthibitisha kwamba ni halali kula chochote, kwa sababu kimeumbwa na Mungu.
#Matendo ya Mitume 10:15-16
Sauti ikamjia mara ya pili, ikimwambia, Vilivyotakaswa na Mungu, usiviite wewe najisi.
Jambo hili likatendeka mara tatu; kisha kile chombo kikapokewa tena mbinguni.
Sina dhana ya kupinga ulaji wa vitu najisi maana kama MTU alishaamua kupinda shingo ni vigumu kuinyoosha kwa kumkataza asile, bali nataka nipinge utumiaji vibaya wa Neno la Mungu.
Sasa wale wanaotumia fungu hili kwa kutetea ulaji wa nguruwe, kambare nk. Ni seme kwamba ni wapotoshaji wa maandiko. Maana hoja katika sura hiyo haihusiani na ulaji wa vyakula hata kidogo.
Ukisoma #matendo sura ya 10:1.... Inazungumzia habari za mtu mmoja anayeitwa #Kornelio, ambaye alikuwa Mrumi, Huyu ni mtu wa Mataifa hakuwa Myahudi.. Mtu huyu alikuwa mcha Mungu lakini alihitaji mtu wa kumfundisha vizuri na kumbatiza.
Mtu ambaye alikuwa karibu na Rumi ni Petro, ambaye alikuwa katika mji wa Yafa. Lakini sasa Petro alikuwa #Myahudi, na Wayahudi walikuwa hawachangamani na watu wa Mataifa waliwaona ni #NAJISI.
#Yohana 4:9 Basi yule mwanamke Msamaria akamwambia, Imekuwaje wewe Myahudi kutaka maji kwangu, nami ni mwanamke Msamaria? (Maana Wayahudi hawachangamani na Wasamaria.)
Kwa vyovyote Petro hangeweza kwenda kwa Kornelio, mtu wa mataifa, maana mtu ambaye alibainika akiwa anachangamana na watu wa Mataifa alikuwa anaonekana ni najisi na pia ilibidi atengwe, Kwa hiyo Petro alikuwa mwoga sana katika suala la kuchangamana na watu wa Mataifa kwa kuwaogopa Wayahudi wenzake: Na Paul anabainisha kwamba Petro alikuwa muoga kuchangamana na watu wa Mataifa.
#Wagalatia 2:11-12
Lakini Kefa alipokuja Antiokia, nalishindana naye uso kwa uso, kwa sababu alistahili hukumu.
Kwa maana kabla hawajaja watu kadha wa kadha waliotoka kwa Yakobo, alikuwa akila pamoja na watu wa Mataifa; lakini walipokuja wao, akarudi nyuma akajitenga, huku akiwaogopa waliotahiriwa.
hivyo lengo la Mungu ni kwamba kupitia yale maono AVUNJE utengano kati ya Wayahudi na watu wa Mataifa, maana Petro hangeweza kwenda bila KUVUNJA kwanza ule utengano. Na lengo la Mungu ni kumuokoa Kornelio ambaye ni mtu wa mataifa.
#HIVYO BASI: wale
#wanyama, ndege na wadudu ambao ni Safi waliashiria Taifa la Israeli, ambao walikuwa WAMETAHIRIWA
#Wanyama, ndege na wadudu najisi waliashiria watu wa Mataifa, ambao hawakuwa WAMETAHIRIWA.
#MAMBO YA #KUJIHOJI:
1. Kumbuka haya ni maono, si kitu halisi, kilichotumika hapa ni lugha ya picha, Mfano Nabii Daniel katika Danieli sura ya saba aliona maono na ndoto : Na katika maono haya aliona wanyama wanne wanatoka baharini wanyama hao ni Simba, Dubu, Chui, na mnyama wa kutisha. Sasa tukisema tuchukulie Maono/ ndoto kwamba ni kitu halisi; sasa jiulize ni lini Simba, Dubu na Chui wakaishi baharini?
2. Petro ni mwanafunzi aliyeishi na Yesu miaka mitatu na nusu, na ikiwa Yesu aliruhusu kula vitu najisi, Peto hangekataa kwa kusema:
#Matendo ya Mitume 10:14 …, Hasha, Bwana, kwa maana sijakula kamwe kitu kilicho kichafu au najisi.
3. Kauli ya Petro ya kusema: Hasha, Bwana, kwa maana sijakula kamwe kitu kilicho kichafu au najisi. Ni uthibitisho tosha kwamba Petro ambaye ni mtume wa Yesu alifahamu vitu najisi na visivyo najisi, na ndio maana alikataa kula.
4. Kauli ya Petro ya kusema: Hasha, Bwana, kwa maana sijakula kamwe kitu kilicho kichafu au najisi. Ni uthibitisho tosha kwamba Yesu hajawahi kuruhusu kula vitu najisi hadi anakufa. Na laiti kama Yesu aliruhusu, Petro hangekataa.
Na ndio maana Petro mwanyewe ijapokuwa aliona wanyama, ndege na wadudu, Lakini alijua yale ni maono tu, na hivyo alitaka kujua maana halisi ya yale maono: na wakati Petro anafikiria maana halisi ya yale maono, ndipo na mlango unagongwa, na wale watu waliotumwa na Kornelio wakaingia:
#Matendo ya Mitume 10:17 Hata Petro alipokuwa akiona shaka ndani ya nafsi yake, maana yake ni nini maono hayo aliyoyaona, wale watu waliotumwa na Kornelio, wakiisha kuiulizia nyumba ya Simoni, wakasimama mbele ya mlango,
Kwa hiyo Petro akawa ameshafahamu maana halisi ya yale maono kwamba yalimhusu Yeye kama Myahudi inabidi aende akachangamane na Familia ya Kornelio ambaye alikuwa ni mtu wa Mataifa.
Na ndio maana Petro baada ya kufika kwa Kornelio anathibitisha kwa kusema.
#Matendo ya #Mitume:10.28
Akawaambia, Ninyi mnajua ya kuwa si halali mtu aliye Myahudi ashikamane na mtu aliye wa taifa lingine wala kumwendea, lakini Mungu amenionya, nisimwite mtu awaye yote mchafu wala najisi.
#NOTE: Kwa hiyo kauli ile ya kusema:….., Vilivyotakaswa na Mungu, usiviite wewe najisi. #Matendo ya Mitume 10:15
Ilimaanisha kwamba kifo cha Yesu kilishaondoa utengano kati ya Waisrael na watu wa Mataifa, Hivyo Petro hapaswi kuwatenga watu wa Mataifa kwa kuwaona ni Najisi/ Hawafai, Maana Biblia inasema:
#Wagalatia 3:28 Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu.
Hivyo Mungu alitumia maono ya wanyama, na ndege na wadudu, kwa sababu Petro alifahamu kwamba Si kila kitu kinafaa kuliwa.
#NOTE: Sasa ili ujue kweli kwamba hoja kubwa ilikuwa ni utata wa kuchangamana na watu wa Mataifa, hebu tusome matendo sura ya 11, baada ya Petro kurudi Yerusalemu akitokea kwa Kornelio nini kilitoke:
#Matendo ya #Mitume 11:2-8
Na Petro alipopanda kwenda Yerusalemu, wale walio wa tohara wakashindana naye,
wakisema, Uliingia kwa watu wasiotahiriwa ukala nao.
Petro akaanza kuwaeleza kwa taratibu, akasema,
Nalikuwa katika mji wa Yafa, nikiomba, roho yangu ikazimia, nikaona maono; chombo kinashuka, kama nguo kubwa inatelemshwa kutoka mbinguni kwa pembe zake nne, kikanifikilia.
Nikakitazama sana, nikifikiri, nikaona wanyama wa nchi wenye miguu minne, na wanyama wa mwituni, nao watambaao, na ndege wa angani.
Nikasikia na sauti ikiniambia, Ondoka, Petro, ukachinje ule.
Nikasema, Hasha, Bwana, kwa maana kitu kilicho kichafu au kilicho najisi hakijaingia kabisa kinywani mwangu.
#Waweza #Endelea…….
Hivyo ndugu zangu mnaotumia aya hiyo ya matendo 10:15, kuwafundisha watu wale chochote kilicho mbele yao mnakosea sana na ikiwa kuna mtu amefundishwa hivyo basi jua ulidanganywa na hao walimu wa uwongo.
Na ikiwa kuna mtu amekuwa akiwafundisha watu kula vitu najisi kupitia aya hiyo, Nakusihi kwa mamlaka ya jina la Yesu uache maana unapotosha watu.
Yesu mwenyewe alitambua kuna chakula na visivyo liwa:
#Luka 11:11-12
Maana ni yupi kwenu aliye baba, ambaye mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe au samaki, badala ya samaki atampa nyoka?
Au akimwomba yai, atampa nge?
Yesu amebainisha kabisa kwamba vipo vitu vingine sio vyakula na haipaswi watu wapewe, ina maana #Jiwe sio chakula, #Nyoka sio chakula, #Nge sio chakula:
Hivyo ukimuona mtu anakula nyoka , Panya, Nguruwe, Kambare, Nge NK. Jua ni tamaa zake, na uchu wa chakula, na sio agizo la Mungu.
Kwa hiyo wale mnaosema Kimwingiacho mtu hakimtii unajisi, bali kimtokacho, basi fikirieni pia kauli hiyo ya BWANA YESU. Lakini pia fikirieni juu ya mlevi anayekunywa pombe, maana naye inamwingia kinywani na inaenda kutoka chooni.
Mtume Paul naye anasema si kila kitu kinafaa kuliwa:
1 #Wakorintho 10:23 Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vifaavyo. Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vijengavyo.
Ni kweli vitu vyote ni halali kwa sababu vimeumbwa na Mungu, lakini sio kila kitu kimeumbwa kwa lengo la kuliwa, maana vingine havijengi mwili bali vinabomoa mwili.
Pia Paulo anasema: 1 #Wakorintho 10:31 Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.
Sasa ikiwa unataka kujua ni Chakula gani ukila ni kwa utukufu wa Mungu? Basi Nenda:
#Kumbukumbu la Torati 14:4-8
Wanyama mtakaokula ni hawa ng'ombe, na kondoo, na mbuzi,
kulungu, na paa, na kongoni, na mbuzi wa mwitu, na paa mweupe, na pofu, na mbuzi wa mlima;
na kila mnyama aliyepasuliwa ukwato, ukapasuka ukwato wake zikawa mbili, naye ni mnyama mwenye kucheua akatafuna tena, katika wanyama wote, ndiye mnyama mtakayemla.
Lakini, hawa msile katika wale wenye kucheua, na hao waliopasuliwa ukwato; ngamia, na sungura, na kwang'a, kwa kuwa hucheua, lakini hawakupasuliwa kwato, ni najisi kwenu;
na nguruwe, kwa kuwa amepasuliwa ukwato lakini hacheui, huyu ni najisi kwenu msile nyama zao, wala mizoga yao msiiguse.
Hivyo maana halisi ya maono haya MUNGU alikuwa anataka kuondoa dhana potofu kwa Petro ya kuwaona watu wa Mataifa ni NAJISI, hawafai kuokolewa.
Jambo la msingi pia: IKIWA Yesu aliruhusu ulaji wa nguruwe, bila shaka Petro hangekataa kula maana ameishi na Yesu miaka mitatu na Nusu. Hivyo kwa jibu la Petro la kusema Kwa maana sijakula kamwe kitu kilicho kichafu au najisi inaonesha Petro hajawahi kula nguruwe, wala Yesu hajawahi kuruhusu kula nguruwe?
Ikiwa Petro ambaye ndiye mtume mkubwa anasema hajawahi kula vitu vichafu, je wewe unamfuata mtume gani anayeruhusu kula vitu najisi?