Kwa kuwa sisi ni wakristo ni kwamba sisi tunafata nyayo za Yesu Kristo. Ni vipi kitu ambacho hakusema Yesu Kristo kinawekewa mabano ya kuweka uchambuzi wa maono ya waliotafsiri biblia? mbaya zaidi kuna biblia hata hayo mabano hayamo, uchambuzi umeunganishwa kuonekana ni maandiko matakatifu yaliyokuwemo kwenye biblia.
Kimuingiacho mtu hakimtii unajisi ni jibu alilotoa Yesu baada ya kuulizwa kwanini wanafunzi wake waliokuwa na njaa walikula mahindi wakiwa njiani bila kuosha mikono, kwa sheria walizojiwekea viongozi wa mda huo waliona kwamba kula bila kuosha mikono kunamtia mtu unajisi, Yesu ndipo akawasahisha kwamba sheria zao hazipo sawa na kwamba kula bila kuosha mikono hakumtii mtu unajisi. Sasa je, hapa kulikuwa na haja ipi ya watafsiri kuongeza maneno yao kwamba maana yake ilikuwa ni karuhusu kula vyakula ambavyo havikutakaswa kama mijusi, kenge na nguruwe wakati kilichokuwa kinazungumziwa ni kula bila kuosha mikono?
Wasabato walipuuzia hayo mabano maana hayakuwa maneno ya Yesu na kazi ya watafsiri sio uchambuzi, Wakristo wengine wakadhani ni Yesu kawapa kibali wakaona ni ruksa ya kula chochote.
Sasa najiuliza kwamba mbwa, konokono, vinyonga, kunguru, paka, chunusi, kobe, n.k wanaweza kuliwa?
Mfano kuna samaki na wanyama wana sumu ama huleta madhara wakiliwa na wakawekwa kwenye kundi la vyakula visivyofaa, Mungu alikosea kusema hawatakiwi kuliwa?
Halafu pia nashangaa Biblia za sikuhizi za kiswahili zimeunganisha hayo maneno bila kuweka mabano, ni wazi kabisa wakristo wengi wanaamini haya maneno yalikuwemo bila kujua kuna uhuni umefanyika kuyaunganisha, maskini mweee! Mtu anabisha mpaka mishipa inamtoka shingoni kwasababu ya mistari iliyopachikwa ambayo haikuwahi kuwepo, ni ujanja ujanja tu ukafanyika kupachika.