Wakristo wasio Wasabato wanaruhusiwa kula paka, panya, kobe, kinyonga, kenge, kunguru, nyani, n.k?

Wakristo wasio Wasabato wanaruhusiwa kula paka, panya, kobe, kinyonga, kenge, kunguru, nyani, n.k?

Suala la yesu kusafisha vyakula vyote limeweka kwenye mabano kuashiria hayo maneno hayakuwemo bali ni uchambuzi wa waliondika biblia hizi mpya zilizotafsiriwa

Nashangaa kuona biblia za kiswahili zimeunganisha kabisa moja kwa moja bila mabano ili ionekane kwamba maneno haya yalikuwemo kwenye biblia

Hivyo basi, Biblia za kiswahili zimechachachuliwa kudanganya waumini, ukiwemo wewe unaebisha mpaka mishipa kukutoka shingoni ukidhani kwamba maandiko hayo yalikuwemo kwenye biblia kumbe kuna mhuni kayatoa mabano ionekane ni maandiko yaliyokuwemo, poleni sana kwa kuchezewa akili mda wote huu mkiaminishwa uongo.

Hebu cheki matoleo haya tofauto ya biblia za kiingereza wameweka mabano, hata google wameweka mabano,

View attachment 2412821

alieandika biblia ya kiswahili kahujumu wakristo wengi wa Tanzania wanaoendelea kula vichafu wakidhani Yesu alivitakasa
Context katika hilo fungu haikuwa aina ya chakula bali issue ilikuwa ni kunawa mikono
Kwenye mjadala Yesu na wanafunzi haikuwa aina gani ya chakula iliwe au isiliwe
waroho wanadakia kula kila kitu
 
Uzoefu wangu kwenye hizi nyama, binafsi nguruwe sili kabisa japo sizuiwi na yeyote yule lakini Nyani nilikula kwa wamatengo mbinga, Ngedere nilikula butembo congo wao wanaita makako, mamba supu yake nilikula Masakaa Uganda, maduduwasha yale nilikula zambia na shima au ugali, Nyoka nilikula kwa jamaa mmoja bangedaido kama unaenda kisangani, wale panya wakubwa nilikula mtwara, na kuna vindege fulani nilikula kondoa, katika vitu vyote sikuwahi kuona tatizo lolote hivo toka nimekula hivo vitu hua siwezi kumhukumu mtu kwa sababu ya kitu anachokula maana hata hivyo nilivyokula wala sikuwahi kudhurika, hivo tuheshimiane kama wewe hauli acha wanaokula waendelee kula sio kesi
uzoefu wako hauwezi kuwa ndo marking scheme ya ulaji
mtoa mada ameonyesha kile biblia inasema
 
Sili nguruwe ni mchafu sana kama mwenzake bata. Ila nikiwa na njaa na hakuna alternative nitaomba na ndimu. Haya mengine mbwembwe za dini tu tukiwa tumeshiba, hakuna binadamu wa kushindana na njaa.
 
Achana na sheria za Wayahudi, fuata maelekezo ya Mungu. Kumbuka, sheria zile ziliwataka hata wazinzi wauawe. Sasa kwa nini mmeendelea na ya nguruwe mkiacha ya wazinzi?

2 Hata asubuhi kulipokucha akaingia tena hekaluni, na watu wote wakamwendea; naye akaketi, akawa akiwafundisha. 3 Waandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka katikati. 4 Wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini. 5 Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake namna hii; nawe wasemaje? 6 Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika nchi.

7 Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe. 8 Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika nchi. 9 Nao waliposikia, wakashitakiwa na dhamiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata wa mwisho wao; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke amesimama katikati. 10 Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia?

11 Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena.]
Aliyekudanganya ya kupiga wazinzi imeondolewa Nan?

Soma BIBLIA VIZURI , HIYO SHERIA IPO ILA WAPIGAJI HAWAPO

SHARTI LA WAPIGAJI MAWE LAZIMA WASIWE NA DHAMBI

YESU ALIRUHUSU APIGWE MAWE ,

7 Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.

Tatizo mnasoma Biblia Kama mnafukuzwa,ndio maana kina Gwajima wanawaburuza, kina mwamposa wanawauzia maji na chumvi.
 
Ukiacha ukristo, lila kiumbe kinaliwa inategemea uko upande gani wa Ulimwengu huu.
 
1 WAKORITHO 6:12 Kila kitu ni halali kwangu,”lakini si kila kitu kina faida. “Kila kitu ni halali kwangu,”lakini sitatawaliwa na cho chote.
BIBLIA HAISOMWI HIVO, NDIO MAANA MNAFUNGUA MAKANISA KAMA UYOGA

Ikiwa kuna aya zinazowachanganya Wakristo wengi, pamoja na Waislamu, ni zinazotoka katika Nyaraka za mtume Paul, na ndio maana hata mtume Petro alitoa angalizo juu ya usomaji wa nyaraka za Paulo na akatoa onyo lifuatalo:
#2 Petro 3:15-17
Nanyi uhesabuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa ni wokovu, kama vile na ndugu yetu mpenzi Paulo alivyowaandikia kwa hekima aliyopewa;
vile vile kama katika nyaraka zake zote pia, akitoa humo habari za mambo hayo; katika nyaraka hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wayapotoavyo na maandiko mengine, kwa uvunjifu wao wenyewe.

Sio Petro tu ndio anadai kwamba nyaraka za Paul ni ngumu, bali hata watu wengine pia wanasema nyaraka za Paul ni ngumu, Na Paul yeye mwenyewe anashuhudia kwamba watu wanasema nyaraka zake ni nzito/ ngumu:

2 Wakorintho 10:9-10

nisije nikaonekana kana kwamba nataka kuwaogofya kwa nyaraka zangu.
Maana wasema, Nyaraka zake ni nzito, hodari; bali akiwapo mwenyewe mwilini ni dhaifu, na maneno yake si kitu.
 
Wala hakuna haja ya kwenda mbali, ingia google tu utaona biblia karibia zote zimewekea mabano,,, Biblia hizi za kiswahili zilizounganisha bila mabano ni uhuni mtupu wa kuwalaghai waumini wadhani yalikuwa ni maandiko halisi...

Poleni sana kwa kudanganywa kwa muda mrefu, mabano haya hapa 👇👇

View attachment 2412827
Acha kuweka assumptions zako, original manuscripts zitaonesha.

Hata hivyo kama ungekuwa umejifunza hebrew, aramaic na greek language utagundua maneno mengi sana kwenye kingereza na hatimaye kiswahili yaliongezwa ili kuleta tafsiri inayoshabihiana na kilichoandikwa kwenye original manuscripts. Hii inatokana na fact kwamba kiingereza na kiswahili ni lugha zenye maneno machache kuliko hebrew na greek language.
 
Biblia ya kwanza kutafsiriwa kuja kiingereza mwaka 1600 king james haikuongeza kitu wala kupunguza kitu, walitafsiri kama maandiko yalivyo, biblia hiyo haina mabano kama biblia hizi mpya, huku biblia za kiswahili ndio kabisa wameunganisha maneno ya kwenye mabano
 
Nimesoma na kuupenda ujengaji wako wa hoja katika mada hii japo kuna mistari kwenye wakolosai hujaigusa.

Pia ninaona ni dhahiri kuna kitu bado haujakifahamu kuhusu ujio wa Yesu Kristo duniani na mtu anayemuamini Yesu anakuwaje ndani ya Kristo.

Ni jambo la kustaabisha kwamba mtu anaamini kuwa ukila nyama fulani utahukumiwa. Ni kukosa kulijua tumaini la wito wetu katika Kristo Yesu.

Pia kuna kitu kimoja cha hatari sana unakifanya ambacho kinanifanya nipate mashaka makubwa unasimama kweli ndani ya Kristo? Unawezaje kuwataja kwa majina na kuwakejeli watumishi wa Mungu?

Paulo mtume alifuta kauli na tamko alilofanya kinyume na kuhani mkuu ingawa ilikuwa dhahiri kwamba kuhani alikuwa amekosea. Unafanya makosa makubwa sana kumsema mtumishi yeyote hata kama yupo wrong.

Kazi yetu ni kuwaombea tu, warumi 14:4 unasema, " u nani unayemhukumu mtumishi wa mwingine? Kwa bwana wake mwenyewe yeye husimama au huanguka. Naam, atasimamishwa, kwa kuwa Bwana aweza kumsimamisha"
Hakuna alipomuhukumu Mtumishi wa Mungu yeyote isipokuwa amewachukulia mfano kwa kupotosha maandiko matakatifu (BIBLIA) kwa watu wa Mungu.

2 TIMOTHEO 3:16-17.

[16]Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;

[17]ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.

Basi yakupasa kuwa mpole watu wanapoelekezwa maana pia YESU ananena ole wake atayemuonea aibu mbele za watu naye atamuonea aibu mbele za Mungu Baba (YEHOVA).
 
Nimesoma na kuupenda ujengaji wako wa hoja katika mada hii japo kuna mistari kwenye wakolosai hujaigusa.

Pia ninaona ni dhahiri kuna kitu bado haujakifahamu kuhusu ujio wa Yesu Kristo duniani na mtu anayemuamini Yesu anakuwaje ndani ya Kristo.

Ni jambo la kustaabisha kwamba mtu anaamini kuwa ukila nyama fulani utahukumiwa. Ni kukosa kulijua tumaini la wito wetu katika Kristo Yesu.

Pia kuna kitu kimoja cha hatari sana unakifanya ambacho kinanifanya nipate mashaka makubwa unasimama kweli ndani ya Kristo? Unawezaje kuwataja kwa majina na kuwakejeli watumishi wa Mungu?

Paulo mtume alifuta kauli na tamko alilofanya kinyume na kuhani mkuu ingawa ilikuwa dhahiri kwamba kuhani alikuwa amekosea. Unafanya makosa makubwa sana kumsema mtumishi yeyote hata kama yupo wrong.

Kazi yetu ni kuwaombea tu, warumi 14:4 unasema, " u nani unayemhukumu mtumishi wa mwingine? Kwa bwana wake mwenyewe yeye husimama au huanguka. Naam, atasimamishwa, kwa kuwa Bwana aweza kumsimamisha"
Mwamposa na wanaofanana nae hawajawahi kuwa watumishi wa Mungu

Mtumishi gan nitajie anauza maji,mafuta,chumvi , n.k

Nitajie kwenye maandiko, ndipo utajua hao ni MATAPELI
 
Mwamposa na wanaofanana nae hawajawahi kuwa watumishi wa Mungu

Mtumishi gan nitajie anauza maji,mafuta,chumvi , n.k

Nitajie kwenye maandiko, ndipo utajua hao ni MATAPELI
ISAYA 8:19-20.

[19]Na wakati watakapokuambia, Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong’ona; je! Haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? Je! Waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai?

[20]Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi.

Mungu ananena Manabii wanapaswa kuenenda kwa "SHERIA na USHUHUDA"

* SHERIA = AMRI 10 ZA MUNGU/KANUNI NA TARATIBU ALIZOWEKA MUNGU KWETU BINADAMU ILI TUZIFUATE.

* USHUHUDA = MATENDO WALIYOFANYA MANABII NA YESU.

Je Nabii yupi alikuwa anauza maji, mafuta, chumvi ili kueneza injili ya Mungu?

Yesu alielekeza wapi huduma za Mungu ziwe zinauzwa?

MATHAYO 10:8.

[8]Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.

Roho Mtakatifu hutoa karama za UNABII, KUOMBA, KUFUNDISHA, KUNENA KWA LUGHA, KUTAFSIRI NDOTO, kwa kadri anavyopendezwa tena wala si kwa thamani yoyote ile ya gharama.

Hao akina Mwamposa, Gwajima n.k. wajitafakari sana njia zao maana Mungu anaonya;

MATHAYO 18:7

[7]Ole ni wa ulimwengu kwa sababu ya mambo ya kukosesha! Maana hayana budi kuja mambo ya kukosesha; lakini ole wake mtu yule aliletaye jambo la kukosesha!
 
Kwa kuwa sisi ni wakristo ni kwamba sisi tunafata nyayo za Yesu Kristo. Ni vipi kitu ambacho hakusema Yesu Kristo kinawekewa mabano ya kuweka uchambuzi wa maono ya waliotafsiri biblia? mbaya zaidi kuna biblia hata hayo mabano hayamo, uchambuzi umeunganishwa kuonekana ni maandiko matakatifu yaliyokuwemo kwenye biblia.

Kimuingiacho mtu hakimtii unajisi ni jibu alilotoa Yesu baada ya kuulizwa kwanini wanafunzi wake waliokuwa na njaa walikula mahindi wakiwa njiani bila kuosha mikono, kwa sheria walizojiwekea viongozi wa mda huo waliona kwamba kula bila kuosha mikono kunamtia mtu unajisi, Yesu ndipo akawasahisha kwamba sheria zao hazipo sawa na kwamba kula bila kuosha mikono hakumtii mtu unajisi. Sasa je, hapa kulikuwa na haja ipi ya watafsiri kuongeza maneno yao kwamba maana yake ilikuwa ni karuhusu kula vyakula ambavyo havikutakaswa kama mijusi, kenge na nguruwe wakati kilichokuwa kinazungumziwa ni kula bila kuosha mikono?

Wasabato walipuuzia hayo mabano maana hayakuwa maneno ya Yesu na kazi ya watafsiri sio uchambuzi, Wakristo wengine wakadhani ni Yesu kawapa kibali wakaona ni ruksa ya kula chochote.

Sasa najiuliza kwamba mbwa, konokono, vinyonga, kunguru, paka, chunusi, kobe, n.k wanaweza kuliwa?

Mfano kuna samaki na wanyama wana sumu ama huleta madhara wakiliwa na wakawekwa kwenye kundi la vyakula visivyofaa, Mungu alikosea kusema hawatakiwi kuliwa?

Halafu pia nashangaa Biblia za sikuhizi za kiswahili zimeunganisha hayo maneno bila kuweka mabano, ni wazi kabisa wakristo wengi wanaamini haya maneno yalikuwemo bila kujua kuna uhuni umefanyika kuyaunganisha, maskini mweee! Mtu anabisha mpaka mishipa inamtoka shingoni kwasababu ya mistari iliyopachikwa ambayo haikuwahi kuwepo, ni ujanja ujanja tu ukafanyika kupachika.
Maelezo yote haya bila kuweka kifungu/Vifungu vya biblia ni ubatili mtupu
 
Kwanza wasabato sio wakristo.

Wasabato bila kujua ni wafuasi wa freemasonry.
 
Back
Top Bottom