BAKIIF Islamic
JF-Expert Member
- Jul 11, 2021
- 600
- 1,843
Fikiria kutokula au kunywa wakati wa mchana kwa siku 30 mfululizo moja kwa moja sio jambo jepesi. "Mtazamo wa mwezi huu kimsingi sio kujizuia au kufunga, bali ni mkusanyiko wa nguvu na akili ya Muislamu juu ya utambuzi wa Mwenyezi Mungu na maisha ya ibada ya uchamungu."
Haipendezi bint wako wa kazi unamkataza kufunga kwakuwa familia yako hapo ni ya kikristo, unamkataza kujistiri na kuvaa ushungi kwasababu hupendezwi na mavazi hayo, hata sehemu ya kuswalia unamkataza asifanye ibada katika nyumba yako.
Vyema kumruhusu binti wa kazi kurudi nyumbani kwao kila mwezi wa Ramadhani ikiwa unakerekwa na yeye kufunga akiwa hapo nyumbani kwako, wengine mnawalazimisha waende kanisani na kudiriki kwenye maombezi ya kukemewa, na ibada mbalimbali za Kikristo hapo nyumbani mkijua kabisa huyu ni binti wa Kiisilamu.
Imani hailazimishwi bali inatengenezwa kwa namna wewe utavyomtendea na kumpa uhuru na kuamini kile anacho kiamini, na kumfanyia wema katika mahitaji yake ya ibada ikiwemo kumnunulia nguo ya sikukuu kama unavyofanya kwa watoto wako wakati wa pasaka, kisha kazi kwako itakuwa kumshawishi kwa hoja za ki-maandiko ili aikubali imani yako nasio vinginevyo.