Wakristo wenye wadada wa kazi wa Kiisilamu acheni kuwanyanyasa kwasababu ya kufunga Ramadhani

Wakristo wenye wadada wa kazi wa Kiisilamu acheni kuwanyanyasa kwasababu ya kufunga Ramadhani

Fikiria kutokula au kunywa wakati wa mchana kwa siku 30 mfululizo moja kwa moja sio jambo jepesi. "Mtazamo wa mwezi huu kimsingi sio kujizuia au kufunga, bali ni mkusanyiko wa nguvu na akili ya Muislamu juu ya utambuzi wa Mwenyezi Mungu na maisha ya ibada ya uchamungu."

Haipendezi bint wako wa kazi unamkataza kufunga kwakuwa familia yako hapo ni ya kikristo, unamkataza kujistiri na kuvaa ushungi kwasababu hupendezwi na mavazi hayo, hata sehemu ya kuswalia unamkataza asifanye ibada katika nyumba yako.

Vyema kumruhusu binti wa kazi kurudi nyumbani kwao kila mwezi wa Ramadhani ikiwa unakerekwa na yeye kufunga akiwa hapo nyumbani kwako, wengine mnawalazimisha waende kanisani na kudiriki kwenye maombezi ya kukemewa, na ibada mbalimbali za Kikristo hapo nyumbani mkijua kabisa huyu ni binti wa Kiisilamu.

Imani hailazimishwi bali inatengenezwa kwa namna wewe utavyomtendea na kumpa uhuru na kuamini kile anacho kiamini, na kumfanyia wema katika mahitaji yake ya ibada ikiwemo kumnunulia nguo ya sikukuu kama unavyofanya kwa watoto wako wakati wa pasaka, kisha kazi kwako itakuwa kumshawishi kwa hoja za ki-maandiko ili aikubali imani yako nasio vinginevyo.

View attachment 2181318
Mnafunga au mnabadilisha ratiba ya kula? Futari na daku ni sawa tu na lunch na dinner.
 
Mimi wangu wife anamlazimisha kula misosi wakati wa kufungua na kumlazimiza aamke kula daku Ili apate nguvu ya kufanya kazi..before that alikuwa akishafungua hataki tena kula daku usiku...next day atalala siku nzima kwamba amefunga Hana nguvu ya kufanya kazi
 
Akili zinatofautiana,watu wanalazimishana Imani. Ukitaka kujua nguvu ya Imani,kuna mtu Alimlazimisha mtu Imani yake Halafu yeye Akahamia upande ule alotoka yeye,Sijui hii inaitwaje.
 
Wakati wa ramadhani ulaji wa mtu aliyefunga huongezeka mara dufu hivyo kuongeza gharama badala ya kupunguza, hivyo usitegemee mtu asiyejitegemea aongeze matumizi ya mwajiri wake kisa "kufunga"
Kuna ujinga mmoja umo humu ndani,asiyekuwa muhusika kuwasemea wahusika huo ni uzushi,mtu hapangiwi chakula cha kufuturu yeye na familia yake,kwa kawaida kifungua kinywa huwa uji,pana gharama gani hapo?anaweza kula wali,viazi,ndizi,mikate,chapati vitumbua,ugali n.k.Sasa kama anauwezo hakuna anayemkataza labda anafuturisha watu,

Kama yuko peke yake na familia yake ni ndogo unazani huo mtiririko wa vyakula ungekuwa peke yako utakula vyote?kumbuka baada ya hapo kuna swala ya Tarawehe almost ni saa moja na nusu mpaka mawili,unazani wewe utaweza?

Hauna tofauti na watu wanaosema Waisilamu hawafungi ila wamebadirisha ratiba ya kula,basi baadilisha na wewe kama utaweza
 
Haipendezi bint wako wa kazi unamkataza kufunga kwakuwa familia yako hapo ni ya kikristo, unamkataza kujistiri na kuvaa ushungi kwasababu hupendezwi na mavazi hayo, hata sehemu ya kuswalia unamkataza asifanye ibada katika nyumba yako.
Wadada wengine wanapenda tu style ya maisha ya kikristu, na unakuta hata hujamwambia lakini yeye anafanya. Mimi wa kwangu alikuwa anang'ang'ania kuhudhuria misa za juma kuu, yaani Alhamis Kuu, Ijumaa Kuu, mkesha wa Pasaka, Pasaka yenyewe na Jumatatu ya Pasaka
 
Kuna ujinga mmoja umo humu ndani,asiyekuwa muhusika kuwasemea wahusika huo ni uzushi,mtu hapangiwi chakula cha kufuturu yeye na familia yake,kwa kawaida kifungua kinywa huwa uji,pana gharama gani hapo?anaweza kula wali,viazi,ndizi,mikate,chapati vitumbua,ugali n.k.Sasa kama anauwezo hakuna anayemkataza labda anafuturisha watu,

Kama yuko peke yake na familia yake ni ndogo unazani huo mtiririko wa vyakula ungekuwa peke yako utakula vyote?kumbuka baada ya hapo kuna swala ya Tarawehe almost ni saa moja na nusu mpaka mawili,unazani wewe utaweza?

Hauna tofauti na watu wanaosema Waisilamu hawafungi ila wamebadirisha ratiba ya kula,basi baadilisha na wewe kama utaweza
Jiulize kwa nini bei ya vyakula hupanda wakati wa ramadhani badala ya kushuka
 
Jiulize kwa nini bei ya vyakula hupanda wakati wa ramadhani badala ya kushuka
Wanaopandisha ni wafanya biashara kutokana na mahitaji ya chakula cha aina fulani,mfano aina yote ya viazi,Magimbi,sukali na mengineyo,huu ni ulafi wao wenyewe
 
Ni ngumu sana kuishi nyumba ya mtu ambaye hamko Imani sawa hata Kama ni ndugu tu, maana dini zote zinafundisha kwamba hakikisha walionyumbani kwako wanaamini kama wewe.

Ni vyema kwenda kufanya kazi kwa mtu ambaye unajua kabisa Imani ziko sawa ili kuepusha migongano.

Au kama ni Imani tofauti basi hakikisheni mnawekeana utaratibu kabla ya kuingia mkataba na Kila mtu anauridhia

Mm nikaa na mabint wa kikristo wengi sana kwa wema tu wengi wanaslim bila shuruti, upande wa mavazi tu lazima nicontrol coz siwez muacha avae uchi mm ni
Mzaz kwake
 
Mm nikaa na mabint wa kikristo wengi sana kwa wema tu wengi wanaslim bila shuruti, upande wa mavazi tu lazima nicontrol coz siwez muacha avae uchi mm ni
Mzaz kwake
Kitu Kama hicho kipo pia kwa wakristo, Binti wa kiisilam kaenda kufanya kazi kwa mkristo then kaamua kuwa mkristo. Ingawa katika tukio lako na tukio nililosema ndugu wa huyo mfanyakazi watajua umemrubuni na wanaweza mtoa kwako au kumtenga na familia.

Kurudi kwenye point, Kama mtakubaliana kabla ya kazi kuhusu kuvaa hijab basi hakuna shida. Lakini vipi saiv mnamruhusu kula mchana na asubuhi?
 
Funga Kwa Ndugu zetu ni kama wanakuwa wamelazimishwa na Kama wako jela na hawataki bughudha. Eti majaribu. Sasa wao wamefunga ila jiran akipika huo mtit wake huko Zenj ni Balaa. Unatakiwa ujifiche na chakula usiweke hta vinukizi...
Hawa jamaa ni tatizo kabisa hadi wanaleta kero kwa watu wasiofunga au upande wao kiimani
 
Mimi MTAG mwezi wa kwanza kuja wa pili tulifunga siku 21. Binafsi nina kifungo yangu ya siku 3 hadi wiki pale nipatapo nafasi au utulivu kazini. Sijawahi lazimisha au laumu majirani au wafanyakazi wenzangu wasile au kupika nikiwa kwenye mfungo kwani ni mimi ndio nafunga. Kuna kipindi huwa tuna vikao na chakula kinaandaliwa ofisini ila natoka nje naacha wenzangu wanakula then nitarudi kuendelea na kikao. Hii ni tofauti na wenzetu. Nifahamuvyo,wengi wa wenzetu wanalazimishwa kufunga ila hayatokei mioyoni mwao kwa lengo la kumtafuta Mungu wao ndio maana wanalazimisha na kuwatafutia wengine sababu.
 
Dah....., Uko Sawa. Ni Kama Vile Waislamu Wengine Kipindi Cha Mfungo Kuwalazimisha Wengine Wote Wafunge sio Sawa.

Mifano ipo nimeiweka akiba wapi Wanalazimisha!
Na huu upuuzi ni mwingi sana mitaani.
 
kwa MIAKA 15 ya kuishi na wafanyakazi 6, watano ni waislamu. wote walikuwa na majini. wengine watatu waliniambia walitibiwa na kusomewa yakaondoka. usiku baada ya chakula mimi na mke na watoto hisali pamoja. wao huwa chumbani. cha ajabu tukiwa katika maombi hulipukwa majini. mimi huwaombea na kuyatoa kwa jina la yesu. Mungu ni mwema wote walishampatia YESU maisha. Wanakili uwezo wa YESU hauna mfano.
 
Manalia lia wakati michezo hio mnayo wenyewe
 
Moja ya vitu vilivyofanya kutokua muumini wa hizi dini. Hakuna upendo wa kweli baina ya binadamu
Nakumbuka nilipata kuishi famili ya kisabato/kilokole katika vitu vilivyokua vinanikwaza ni kulazimishwa kusali na kufuata maamrisho katika mambo ambayo binafsi nilifanya ili kiridhisha watu machoni lakini moyoni mwangu hakuna ninachojivunia
Na hata hawa wengine wanaweza kuwa na upendo uliopambwa kama sukari ya juu katika keki ila katika mioyo yao ni balaa tupu.
Kuishi nje ya misingi ya hizi dini ni furaha na amani ya kweli,
 
Infact dini zote zinajaribu kulazimisha kwamba watu wote wa nyumba yako uhakikishe wamejiunga na wewe na wakikataa uwatenge au uwachukie. Sometimes wanatumia nafasi ya wewe kuwa mfanyakazi wao kukulazima indirect kuwa member wa dini yao.

Hata kwenye familia ni tatizo Sana. Sisi ni wakristo wa dini Fulani na hata dada zangu na kaka ni waumini wa hiyo dini. Sasa katokea mjukuu mmoja kaamua kwenda dini nyingine ambayo ni antogonist na dini yetu ingawa bado ni ukristo.

Lakini alipokuja home wakawa wanamlazimisha kwenda kwenye dini yetu wakati wanajua yeye ni WA Ile nyingine. Dogo aliposhikilia msimamo wake wakaanza kum ignore na kumuona kapotea Sana.

Nikawaambia yule kashafika miaka 18 na ana uhuru wa kuchagua sehemu ya kuabudu na hakuna sababu kumtreat vibaya wakati ni haki yake. Walikubali lakini kishingo upande Sana. Chakushukuru yule dogo alienda kupanga geto na kuendelea na dini yake na mambo yanaenda poa kwa Sasa na anauhusiano mzuri na familia yetu na hata ndoa yake familia yangu waliishighulikia vizuri akiwa hukohuko kwenye dini yake.
 
Yes, ile concept “alikuja kwangu akapendezwa na dini yangu akaifuata” naona effectiveness yake ni 0.2% huwa hakuna uhalisia kwa uzoefu wangu pia mkuu 😅
 
Kipindi hiki ni kigumi kwa wote, hata kwa mabinti wa kikristo wanaofanya kazi kwenye nyumba ambazo mabosi ni waislamu...

Kanuni ya maisha ipo palepale, mtumwa hufuata matakwa ya bwana wake...
 
Back
Top Bottom