Wakristo wenye wadada wa kazi wa Kiisilamu acheni kuwanyanyasa kwasababu ya kufunga Ramadhani

Siyo lazima ile chai mnayokunywa asbh yeye share yake anafuturu jioni basi. Na daku ile share yake ya usiku ni daku kufunga siyo kuharibu bajeti ya mwenye nyumba mkuu.
 

Zanzibar ni nchi ya kiislamu mkuu, kwahiyo inafuata taratibu za kiislamu. Hakuna alielazimishwa kufunga, Kilichokatazwa ni kula au kuuza chakula hadharani.
 
Vipi kwa wakristo wanaofanya kazi kwenye nyumba za waislam wanaruhusiwa kula mchana mwezi huu au kula kitimoto nyumbani?[emoji124]

wewe mpumbavu sana kiti moto imekatazwa kwenye bibilia msile nyama ya nguruwe biblia imekataza wewe nikristo wa wapi?
 
Mbn nyie mnakataza watu wasiuze vyakula mchana kama vule watanzania wote tumefunga ramadhani, ilo mbona hulisemi?

wee jizi watu wanazungumzia mtu na mtu nyumbani kwake sio biashara biashara waambie serikali wafungua hayo mahotel
 
Hii habari ni ya uongo kabisa.Katika watu wanaoheshimu imani za watu wengine kwa vitendo ni wakristu

Mkristu anampenda na anapenda kujifunza kutoka kwa watu wa imani nyingine na hawawezi kufanya supremacy imani yao

Ukiishi kwa mkristu akijua imani yako atakusisitiza kusali na kama ni mgeni atakupeka mwenyewe kwenye nyumba ya ibada ya imani yako

Atajitshidi mshitaji yote yanayobatana na imani yako kama mavazi ns vyakula

Katika hali ya kawaida Mkristu akikutana na mtu wa imani nyingine atamheshimu kwa kumsalimia salamu ya dini ya mwenzame kamwe hawezi kumsimia kwa salamu ya dini yake mtu asiye wa imsni yake

Kamwe mkristu hawezi kumuita mtu wa imani tofauti na yake majina mabaya kama makafiri

Mkristu , anaheshimu siku za ibada na sherehe za dini nyingine na kujitahindi hata kuvaa mavazi kama yao lakini kuna baadhi ya watu WATAKUDHIHAKI wakikuona na mavazi hayo utasikka " UMEPENDEZA" tafsiri ya hii ni mbaya sana kwa mtu aliyefanya kukuheshimu lakini wewe unamsifu kwa mgongo wa chupa ambayo in face of it amemaanisha...........

Wakristu wanaamini kwenye dirversity kamwe hawaamini kwamba dunia hii inawafaa wao tu lakini wanaamini kuwa tofauti zetu za lugha, mila, desturi , jinsia, rangi na dini ndio zinafanya ukuu wa Mungu uonrkane. Mungu angeamua kutuumba wote tufanane kama maharagwe kuanzia sura, jinsia, akili,lugha na imani angeweza ila sliamua hata wale mapacha ambao ni identical wanatofautina mambo mengi
 
Tungeanza na wale wanaotandikwa fimbo kiembembuzi na viunga vyake ati wamekula mchana
 
Lakini ukikaa na mfanyakazi wako akafunga ukimuwezesha kidogo hata kwa uji na futari simpo Kwani Kuna ubaya gani ?

Mbona ni jambo jema tu?!

Daku atakula shea yake ya chakula chake cha usiku mlichokula nyie wengine.

Kuhusu mavazi ya stara nayo Kwani yana ubaya gani?

Mbona kujisitiri ni jambo jema hata Biblia imeandika na kuagiza hivyo kuwa wanawake wavae mavazi ya staha?!

Tupendane na kuishi kwa kufuata maadili mema Kwani sisi sote ni ndugu watoto wa Baba yetu Ibrahim.
 
Yani kama kuna mtu anayafanya hayo madai ya Mleta mada Naomba ayatafakali na kujirekebisha.

Kumuwezesha yaya wako kufunga ni jambo la baraka kwenye familia.

Kufunga kunaondoa makando Kando mengi ndani ya moyo wa mtu.

Hata visirani na mawazo mabaya huondoka au kupungua wakati wa kufunga.

Kuhusu mavazi msiwazuie mavazi yao ni mazuri.

Kuweni na mtazamo chanya na upendo wa Kweli.
 
Kuna Binti alikuww anafabya kazi kwa broo saizi ametoka aemeenda kwa nyumba ya kikristo aise bint amebadilika mpaka skin taiti na alikuwa anaswal saiz kawa kivingine kabisa
 
Ila tuwe wakwel nyie mnabadilisha ratiba ya msosi tuu yaan unafunga afu unaamka saa 10 au 11 za asubuh kula???
Mtu anakula SAA 10 usiku. Wengine mnaamka na njaa, yeye muda huo Ameshiba NDIII halafu anaanza kuwaigizia Swaumu Inauma.

Unafiki kabisa
 
Mwisilamu anatakiwa ampe Uhuru mkiristo ambao autoaribu mambo yake ndani mfano ampe chakula ale ila asile mbele ya waliofunga mkiristo Naye ampe chakula mwisilamu wakati wa kufungua kusiwe na vineno kote uko.
 
Sio Zanzibar pekee Somalia Afghanistan etc zipo nchi kama ufaransa kuvaa ijabu tu imekuwa shida
 
Na pia wale ambao wanalazimisha Dada zao wa kazi nao wafunge kipindi cha Mfungo. Hii si sawa hata kidogo.
 
Ungesemea pande zote,binti wa kazi wa kikristo anaweza kula kitimoto kwa boss wake muisilamu?? Je binti wa kazi wa kikristo anaweza kula kipindi boss wake muisilamu kafunga Ramadan??
 
Umekariri mzee, watu wanafutari wali, ugali, mihogo, na hata kande, alokwambia kufutari unatakiw uwe na bajet ya elf 30 huyo haelewi anachokifanya.
Na wengine wanafanya kwa kujifurahisha ikishakua uwezo anao na ameamua mwenyew sio mbaya, lkn kufuturu sio lazima ayo mambo.
#Elimundokilakitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…