CCM ni ileile hakuna cha bashiru wala nini hapo ni propaganda imetengenezwa na ccm ili watutoe kwenye mjadala wa maji,umeme na gharama za maisha, fisi hajawahi aminika hata akiwa kibogoyo katikati ya mbuzi
 
Mwaka huu wakulima tumeuza mazao yetu kwa bei ya juu na kupewa pesa taslimu papo hapo hakuna mkopo kama tulivyozoea kabla hajawa Rais.
Safi sana eti kwa juhudi hizi za Rais Samia Suluhu kufanikisha kupungua kwa gharama za kilimo utaacha kusema mama anaupiga mwingi
 
Kwa Nini wasimpongeze? Subilieni kunyolewa 2025
 
Yes hao ni wakulima!, Utii ni pamoja na kuamini kila unachoambiwa!, hata kama macho yako yanaona zaidi, usiwe doubtful kama Tomaso, ukiambiwa hawa ni wakulima, amini ni wakulima!.
P
hahhaha jamani wakulima wa sasa sio wale tuliowazoea wa njaa njaa hawa wakulima wanauza mazao yao kwa bei ya juu ni halili yao kumpongeza Rais Samia Suluhu
 
Na wewe kaandae wa kwako mkuu ambao Ni original
 
Kwamba hata mbolea mpaka tuagize ?

Na Pesa ya kununua hio Mbolea mpaka tuombe !!!, Kwa mtaji huu Matonya angekuwa Rais wetu angetufaa sababu inaonyesha qualification za hawa watawala ni kuombaomba na kutegemea vya kuagiza...
Kuna nchi gani hapa africa isiyoagiza vitu nje acheni kupinga kila kitu Rais Samia Suluhu kajitahidi sana kuwekeza katika kilimo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…