Wakulima Manyara wamuunga mkono Rais Samia
Songa Mbele #Bashiru!
Bado kidogo tu na kitaeleweka!

Bashiru mmoja!
Anaitingisha CCM namna hiyo!

Hapo bado wapinzani wa nje ya CCM kina #Lissu na wengineo woote!

Jiwe la gizani limefanya kazi yake!

Limewapata wahusika na sasa tunaona Mayowe tupu!
CCM ni ileile hakuna cha bashiru wala nini hapo ni propaganda imetengenezwa na ccm ili watutoe kwenye mjadala wa maji,umeme na gharama za maisha, fisi hajawahi aminika hata akiwa kibogoyo katikati ya mbuzi
 
Mwaka huu wakulima tumeuza mazao yetu kwa bei ya juu na kupewa pesa taslimu papo hapo hakuna mkopo kama tulivyozoea kabla hajawa Rais.
Safi sana eti kwa juhudi hizi za Rais Samia Suluhu kufanikisha kupungua kwa gharama za kilimo utaacha kusema mama anaupiga mwingi
 

Rais Samia Suluhu leo yuko ziarani mkoani Manyara na wakulima wilayani Babati mkoani Manyara wameandamana kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapunguzia bei ya mbolea.

Wakijiandaa kumpokea Rais ambaye anaanza ziara mkoani humo leo wamesema walikuwa wakinunua mbolea kwa TZS 150,000 lakini sasa wananunua kwa TZS 70,000 tu.

Sababu kubwa iliyopelekea wananchi wampongeze ni kuongeza bajeti ya Kilimo (2021/22 mpaka 2022/23) kutoka 250b hadi 950b,bajeti ya ugani kutoka 603m hadi 15b, uzalishaji mbegu kutoka 10.53 hadi 43.03b, umwagiliaji kutoka 46.5 -lhadi361.5b

Ninaona wakulima wana kila sababu ya kumpongeza Rais Samia Suluhu maana amefanikiwa kupunguza gharama za kilimo, sasa mbolea wananunua kwa nusu bei, mama amefanikisha masoko ya mazao ya uhakika pia wakulima wanauza mazao kwa bei nzuri ukilinganisha na awali

pia Waziri wa kilimo, Mhe. Hussein Bashe anasema matatizo ya kilimo yamekua yakitatuliwa kwa matukio lakini Serikali ya awamu ya sita imeamua kutatua matatizo ya msingi kwa kuwekeza kwa muda mrefu ikiwemo uwekezaji wa mbegu na miradi ya umwagiliaji na ameongeza kua hakuna Mtanzania atakayekufa kwa njaa serikali imetunza chakula cha kutosha

Lengo la serikali ya Rais Samia Suluhu ni kuboresha sekta ya kilimo na maslahi ya wakulima, Sekta ya kilimo imeimarika chini ya Rais Samia Suluhu
Kwa Nini wasimpongeze? Subilieni kunyolewa 2025
 
Yes hao ni wakulima!, Utii ni pamoja na kuamini kila unachoambiwa!, hata kama macho yako yanaona zaidi, usiwe doubtful kama Tomaso, ukiambiwa hawa ni wakulima, amini ni wakulima!.
P
hahhaha jamani wakulima wa sasa sio wale tuliowazoea wa njaa njaa hawa wakulima wanauza mazao yao kwa bei ya juu ni halili yao kumpongeza Rais Samia Suluhu
 
Hili lote ni picha linalotengenezwa, ili uonekane Dkt Bashiru hana maana.

DKT BASHIRU, SONGA MBELE

Ni kawaida, Ukweli Mmoja, hupigwa na Mauongo zaidi ya buku.

Walakini, ukweli ni ukweli, na hushinda.

Tunakupenda na tunakuamini Dkt Bashiru, endelea kusimamia Falsafa zako na uwasameee wanyonge.


Na wewe kaandae wa kwako mkuu ambao Ni original
 
Kwamba hata mbolea mpaka tuagize ?

Na Pesa ya kununua hio Mbolea mpaka tuombe !!!, Kwa mtaji huu Matonya angekuwa Rais wetu angetufaa sababu inaonyesha qualification za hawa watawala ni kuombaomba na kutegemea vya kuagiza...
Kuna nchi gani hapa africa isiyoagiza vitu nje acheni kupinga kila kitu Rais Samia Suluhu kajitahidi sana kuwekeza katika kilimo
 
Back
Top Bottom