Wakulima tumpuuze Dr. Bashiru Ally hana jema kwa Taifa letu

Kasema ukweli mtupu wewe Juma Juma ndio wa kupuuza wakulima wanataabika lakini unajifanya msemaji wao wakati hujui wanapitia madhila gani kwa sasa bila kusikilizwa na kuwezeshwa
 
Ucha Ujuha wako wewe. Wakulima tumepata shida sana ya mbolea kwa ajili ya Mahindi na Viazi mkoni Njombe halafu unaleta ngongera zako hapo. Tunanunua mbole kwa foleni kama Manamba
 

Duh, Dr. Bsshiru ndio anamsema Mh. Rais moja kwa moja hivi.. Kweli hana shukrani, yaani pamoja na kupewa ubunge wa bure, aisee mimi ningefukuza mbali kabisa, huyo ni sumu kwa serikali ya Mama Samia.

Kama ulivyosema hapo juu, Dr Bashiru mnafiki na muongo sana, wakati akiwa Katibu Mkuu CCM na akiwa Katibu Mkuu Kiongozi, Tz nilipitia mateso mabaya sana, watu kuuawa, kuteswa, watu kunyang'anywa fedha zao, hofu kuu ilitawama watu Tz, sukuma gang iliharibu nchi, na wakulima walikuwa na hali mbaya na kila mmoja hata wananchi hali mbaya ilikuwa, na yeye alikuwa kazi kusifia sifia tu, leo anaongea upuuzi mtupu.
 
Bashiru kaongea kweli ila tatizo ni moja tu, kwanini awamu ya 5 nae alikuwa anasifu hadi anakufuru.

Hii nchi unafiki ni mwingi Sana.

Watu wanamshambulia Bashiru sio kwa sababu ya alichosema ila ni kwa sababu ya unafiki wake! Awamu ya 5 alikuwa analamba viatu hadi mtu unashangaa kama huyu ndo Mwl Bashiru ama mtu tofauti.

Ujinga mtupu.

Alafu mtu anatokea huko anasema watu fulani msiwachague kwa sababu watalipiza kisasi, sasa watu kama kina Bashiru unawaachaje ukichaguliwa?
 
Nyie nyote ccm ni wa kupuuza tu
 

Shida ya watu wa mjini mnajua mambo mengi ya kwenye makaratasi

Hamjui site kuna nn na mtu akisema mnakuja na maandiko kibao

Hao wakulima si ndio kila siku wanapiga kelele?

Nenda mtwara kwenye korosho ukajionee nenda kaulize mbolea na dawa za wadudu zimeenda wakati korosho zipo hatua gani?
 
Bashiru pamoja na mapungufu yake kwenye hili kaongea ukweli Wakulima tuungane tuwaondoe watawala huyu ndo the OG karudi kwenye line kwa kasi ya 5G
Mimi mkulima wa pamba misimu wa mwaka huu 2022 nimeuza kilo moja ya pamba Shilingi 2,000/= kwa kilo tena cash wakati bei iliyopangwa ilikuwa Shilingi 1560/= kwa kilo tofauti na miaka ya nyuma bei ilikuwa inapangwa lakini ukifika wakati wa mauzo unaambiwa kilo Shilingi 500 na pamba inachukuliwa kwa mkopo. Wakulima tumenufaika kipindi cha urais wa Mama yetu Samia Suluhu Hassan. Mwenyezi Mungu ambariki Rais wetu.
 
Litakuwa wapi hilo shamba zaidi ya pale zilipo ofisi zao za Lumumba!
Bora ata angekua lumumba angekuja na hoja tu ila ni fala flani tu shabiki apo Dr bashiru so alkua anaelezea role za chama sasa Kuna baya Gani kama sio mkurupukaji tu
 
Bashiru kaongea ukweli mtupu. Safi Sana kiongozi. Kwenye ukweli lazima niponheze hata kama sio wa chama changu.
ni bashiru huyuhuyu alkuwa kiongozi mkubwa tu kwenye awamu iliyopita,historia hanionyeshi chochote kizuri alichokifanya bashiru kwa wakulima hawa,. hakuwatetea kabisa kuhusu biashara ya mazao yao, hata tu kuwatafutia soko la ndizi nje ya nchi hakuwahi. ninavyohisi anaongea kwa hila na chuki lakini hana wakulima moyoni mwake.
 
Hata hiyo mbolea ya ruzuku wanayoisema ipo mjini badala ya vijijini walipo wakulima
 
Wewe ni Empty Skull Minded Person!
Ndani ya CCM hii,watu kama wewe ndio wanakula mema ya Asali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…