Wakuu hebu tumalize utata hapa, INDUCTION COOKER vs MULTICOOKER nani ni mkombozi wa mapishi kwa umeme

mimi natumia kuni za kutoka pori la mlima kitonga au mara mojamoja mkaa, maisha ndio haya haya
Pole sana kiongozi, hata mimi nimeishia kusoma tu hayo mavitu ila sijui yanatumikaje.

Nishati yangu kuu ni gas na mkaa, kwa hiyo tuishi tunavyoweza siyo tunavyotamani au kusoma.
 
Pole sana kiongozi, hata mimi nimeishia kusoma tu hayo mavitu ila sijui yanatumikaje.

Nishati yangu kuu ni gas na mkaa, kwa hiyo tuishi tunavyoweza siyo tunavyotamani au kusoma.
Ndio mkuu kujipa sifa vitu sijawahi kuviona hua siwezi,
 
Kweli kabisa kiongozi.

Ila ninaamini asilimia kubwa humu tuko kwenye matumizi ya kuni, mkaa na kidogo gas ingawa wengi wanaigiza ili waonekane sio wanyonge kama sisi tulivyo.
Mimi hapa sina sababu ya kudanganya, hata chai nakunywa mara mojamoja sana, maana nakula ugali asubuhi mapema, naondoka kuhangaika ili mambo yasogee
 
Mimi hapa sina sababu ya kudanganya, hata chai nakunywa mara mojamoja sana, maana nakula ugali asubuhi mapema, naondoka kuhangaika ili mambo yasogee
Ukweli unatuweka huru
 
Wabongo acheni kuishi miaka 4000 nyuma ..



Dunia ni Kijiji agizeni hizi sufuria Kwa matumizi ya hizo induction cooker.
 

Attachments

  • 1714416399349.png
    289.4 KB · Views: 24
  • 1714416376201.png
    231 KB · Views: 20
Agizeni hizi
 

Attachments

  • 1714416980371.png
    151.5 KB · Views: 25
  • 1714416972864.png
    436.3 KB · Views: 27
  • 1714416980371.png
    151.5 KB · Views: 25
  • 1714416972864.png
    436.3 KB · Views: 23
Wakuu kama thread inavojieleza either kulingana na uzoefu wako au umeskia ndugu jamaa wanasema tupate, mkombozi wa mapishi kwa umeme.

Induction cooker
View attachment 2905663

Multi Cooker
View attachment 2905665
Both induction na multi cooker ni mkombozi kwa mapishi ya umeme. Tofauti kati ya induction cooker na multi cooker ipo katika matumizi na namna vifaa hivyo vinavyofanya kazi.

Induction cooker ni jiko la kawaida kama yalivyo majiko mengine ya umeme uliyozoea kuyaona mtaani. Tofauti ya induction cooker na majiko ya kawaida ya umeme, ni teknolojia ya magneticfield (sumaku) inayopatikana kwenye jiko la induction.

Multi cooker ni nzuri kwa ajili ya kuchemsha vyakula. Teknolojia yake ya kuzuia mvuke usitoke, kunawezesha chakula kinacho chemshwa kiweze kuiva kwa muda mfupi kuliko inavyopaswa kuwa endapo ungechemsha kwa kutumia sufuria na majiko ya kawaida, hivyo kuokoa gharama ya umeme.
 
Hapo kwenye bold ndipo ulipokosea, induction cooker zinatumia technology ya usumaku, na infrared cooker zinatumia hiyo mionzi ya infrared.
 
Hapo kwenye bold ndipo ulipokosea, induction cooker zinatumia technology ya usumaku, na infrared cooker zinatumia hiyo mionzi ya infrared.
I was left stranded for awhile, infrared is something heat related radiation while induction is on electromagnetic field coupling means.
 
Juzi juzi nimezunguka kko nzima hakuna induction cooker ya plate mbili wala moja, wao wananipa infrared/ceramic cooker wakidhani ni induction, mtoa mada ameweka picha ya silver crest, sidhani kama ni induction cooker hiyo.
Nenda HomeCity wanazo
 
Mashine ya kufulia usiihofie, ninayo ya mchina Elekta, mwaka wa5.

Navaa na kurundika nguo kwa mwezi mzima ndiyo nakuja kuburuza.

Mzigo mkubwa sana nafua kwa unit 0.5.

Ila inalemaza mashemeji wanabweteka wanakuwa tipwa tiipwa😆😁😜
 
30,000 kwa mwezi umeme? Sijajua unatumiaje. Mi natumia 90,000 umeme kwa mwezi.
 
Kama hamjui induction cooker, ceramic cooker au infra red cooker, Nyie mnaishi dunia ya ccm.
Hamna tofauti na yule bibi yenu anayezurura na lile airbus 220 letu duniani kote huku akijinasibu anaenda kutuletea maendeleo
 
Acha mbwembwe. Hata ukiwa na ac, washing machine, friji, etc huwezi kutumia umeme wa 90,000/= {240 kw} kwa mwezi.
 
Guys Mimi nauza Induction Cooker yangu brand ya Envoil : Cooker Ina plate 2, brand new, nilinunua lakini Supply ya Umeme mtaani kwetu ni ndogo, nimesubiria transformer Tanesco waweke Mwaka Sasa unaenda kimya, vitu vingi vya umeme nashindwa kutumia

Bei: 500,000 ,: ukitaka na Sufuria zake nakupa 100k zipo set nzima mpya kabisa: Please DM for more
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…