Wakuu hebu tumalize utata hapa, INDUCTION COOKER vs MULTICOOKER nani ni mkombozi wa mapishi kwa umeme

Wakuu hebu tumalize utata hapa, INDUCTION COOKER vs MULTICOOKER nani ni mkombozi wa mapishi kwa umeme

Kuna kitu kimoja wanaume wenzangu huwa nawashauri, kazi za jikoni hazituhusu sawa lakini usipo invest kwenye tech jikon kwako ni ww mfuko utakutoboka, kwangu nina rice cooker, eletric pressure cooker, induction cooker, bread maker, blender kadhaa, juice maker, water boiler ya lita 10 nk vyote ni umeme, gas ya kilo 50 huu mtungi size ya kati huwa unatumika miez 3, mkaa ni kama situmii tena maana nlinunua kiroba kile cha 10,000 mwezi wa 4 huu kipo nusu, umeme nanunua 30,000 kwa mwez unatosha, so vitu vingi natumia umeme kuliko hizi energy source nyingine za gharama, sio kwamba sina watumiz mengine kama kufulia nk ila umeme wa 30k unatoboa safi kabisa, wekezeni jikon kwa technolojia muone ilivyo rahisi
Tatizo tunaishi nyumba za kupanga arafu umeme tunachanga siunajua so tuzidi ombeana tu tuvuke huu mtihani kuishi nyumba moja familia sita
 
Pole sana kiongozi, hata mimi nimeishia kusoma tu hayo mavitu ila sijui yanatumikaje.

Nishati yangu kuu ni gas na mkaa, kwa hiyo tuishi tunavyoweza siyo tunavyotamani au kusoma.
Tujifunze kuishi
1. Maharage hayapikwi masaa matatu, wala kuongeza maji mara nne
2. Mwanamke kukupeleka maji bafuni ya kuoga ni umaskini maji unatakiwa uyakute bafuni

Ngoja niishie hapa
 
Rice cooker je?
Hiyo tupa nunua pleasure cooker unapika mpaka ugali siku gesi imekata ndio utajua kumbe naweza pika ugali kwenye pleasure cooker na ukaiva
Procedure ni weka maji funga wacha maji yakichemka fungua weka unga anza kusonga ugali unaiva fresh tu toa kitu weka mezani anza kula hii ni moja ya addition ya pleasure cooker ambayo hata watengenezaji hawajaibainisha ila kutokana na changamoto mtumiaji kaivumbua
 
Infrated cooker tena ya plate moja achana na iyo ya coil mbili unafamilia?Jiko zuti sana wasikutishe ulaji wa Umeme hapana kabisaa..Jiko lipo kwenye Technology ambayo ni power saver na Environmental Friently kabisaa unaweza kupika kwa Unit za Umeme ndogo kabisa kama kunyoosha nguo,Kuwasha AC/Feni etc.

Kwa hiyo Multicooker kama ni mapishi ya wali ni safi kabisa iko chap nayo haili umeme kabisaa ila inawahi kuharibika

Yote 9 la 10 majiko yote tajwa ni mazuri ila Changamoto pekee ni yakiharibika mfano iyo induction coil jiko likidondoka likapasuka unaweza kuliweka stoo kwasababu wauzaji wengi kwenye warranty wasumbufu

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
Acc inatumia Hadi unit 1 Kwa saa Sawa na 24unit Kwa siku, yaani umeme WA 10k Kwa siku. Je hii ni cheap? Warrant huwa haikavi uzembe kama huo wa kudondosha majiko chini
 
Wakuu kama thread inavojieleza either kulingana na uzoefu wako au umeskia ndugu jamaa wanasema tupate, mkombozi wa mapishi kwa umeme.

Induction cooker
View attachment 2905663

Multi Cooker
View attachment 2905665
Inategemea unataka kupika nini. Jiko langu liko kama kiwanda kidogo, kuna majiko ya aina tofauti tofauti yakiwemo umeme na ya gas kuweka kuhimili mapishi ya aina yoyote.
 
Tujifunze kuishi
1. Maharage hayapikwi masaa matatu, wala kuongeza maji mara nne
2. Mwanamke kukupeleka maji bafuni ya kuoga ni umaskini maji unatakiwa uyakute bafuni

Ngoja niishie hapa
Sasa kama mimi bado sijamudu kuishi hayo maisha, unataka niseme ninaishi hivyo?.
 
Mimi natumia. Zote mbili, zote ni muhimu hiyo malt cooker/ pressure coocer ni nzuri na haitumii umeme mwingi, induction cooker ni nzuri kwa vitu vya chap chap na kukaanga. Changamoto ya wabongo ni kuuziwa infrared cooker na kuambiwa ni induction cooker, na wengi wahazijui zaidi na zinafafana kwa kiasi kikubwa. Kama hiyo uliyoweka hapo ni infrared cooker na sio induction
Halafu hizo induction cooker MOSFET yaani kipuli kinachochakata umeme kwenye inductor kikiungua ni mtihani matengenezo ni bahati nasibu
 
Sasa kama mimi bado sijamudu kuishi hayo maisha, unataka niseme ninaishi hivyo?.
Hayo ni maishaa ya kawaida sana kiongozi unapashwa kuishi wala si utajiri huo zaidi ya kufanya kazi kwa bidding yenye kupatia kipato na kuamua unataka uishi vipi
 
Mashine ya kufulia usiihofie, ninayo ya mchina Elekta, mwaka wa5.

Navaa na kurundika nguo kwa mwezi mzima ndiyo nakuja kuburuza.

Mzigo mkubwa sana nafua kwa unit 0.5.
Shukrani sana mkuu kwa ushauri, nitajipanga nipate moja.
 
Mkuu nina wasiwasi mmoja hivi hizo induction cooker zinaweza himili mchakamchaka wa mgandamizo wa sufuria wakati wa kupika ugali, make naona nyingi juu ni vioo.
Mkurya katika ubora wake… Bila kaugali maisha hayajaenda
 
Hiyo tupa nunua pleasure cooker unapika mpaka ugali siku gesi imekata ndio utajua kumbe naweza pika ugali kwenye pleasure cooker na ukaiva
Procedure ni weka maji funga wacha maji yakichemka fungua weka unga anza kusonga ugali unaiva fresh tu toa kitu weka mezani anza kula hii ni moja ya addition ya pleasure cooker ambayo hata watengenezaji hawajaibainisha ila kutokana na changamoto mtumiaji kaivumbua
Siyo sembe tu chief hadi chips zege na cake tunaivisha!.
 
Sasa wakubwa kwa uzoefu wako ipi ni brand bora ya Home appliances make sokoni kuna utitiri wa brand za mchina.
E.g Hisense, Evoli, West Point, Aborder, Sundar, Alitop, Itel n.k.
Samsung na LG sijazitaja make bei za vitu vyao na price to performance ratio ni mbingu na nchi.
 
Hiyo tupa nunua pleasure cooker unapika mpaka ugali siku gesi imekata ndio utajua kumbe naweza pika ugali kwenye pleasure cooker na ukaiva
Procedure ni weka maji funga wacha maji yakichemka fungua weka unga anza kusonga ugali unaiva fresh tu toa kitu weka mezani anza kula hii ni moja ya addition ya pleasure cooker ambayo hata watengenezaji hawajaibainisha ila kutokana na changamoto mtumiaji kaivumbua
Mi nacheka tu ulivyoandika pleasure
 
Sasa wakubwa kwa uzoefu wako ipi ni brand bora ya Home appliances make sokoni kuna utitiri wa brand za mchina.
E.g Hisense, Evoli, West Point, Aborder, Sundar, Alitop, Itel n.k.
Samsung na LG sijazitaja make bei za vitu vyao na price to performance ratio ni mbingu na nchi.
Kuna warabu wanauza wanatembeza majumbani ni nzuri sijalikariri jina ila kama vile wameandika Germany technology. Ninayo Pressure cook na microwave kutoka kwao mwaka sasa zinapiga mzigo.
 
Back
Top Bottom