Wakuu hebu tumalize utata hapa, INDUCTION COOKER vs MULTICOOKER nani ni mkombozi wa mapishi kwa umeme

Tatizo tunaishi nyumba za kupanga arafu umeme tunachanga siunajua so tuzidi ombeana tu tuvuke huu mtihani kuishi nyumba moja familia sita
 
Pole sana kiongozi, hata mimi nimeishia kusoma tu hayo mavitu ila sijui yanatumikaje.

Nishati yangu kuu ni gas na mkaa, kwa hiyo tuishi tunavyoweza siyo tunavyotamani au kusoma.
Tujifunze kuishi
1. Maharage hayapikwi masaa matatu, wala kuongeza maji mara nne
2. Mwanamke kukupeleka maji bafuni ya kuoga ni umaskini maji unatakiwa uyakute bafuni

Ngoja niishie hapa
 
Rice cooker je?
Hiyo tupa nunua pleasure cooker unapika mpaka ugali siku gesi imekata ndio utajua kumbe naweza pika ugali kwenye pleasure cooker na ukaiva
Procedure ni weka maji funga wacha maji yakichemka fungua weka unga anza kusonga ugali unaiva fresh tu toa kitu weka mezani anza kula hii ni moja ya addition ya pleasure cooker ambayo hata watengenezaji hawajaibainisha ila kutokana na changamoto mtumiaji kaivumbua
 
Acc inatumia Hadi unit 1 Kwa saa Sawa na 24unit Kwa siku, yaani umeme WA 10k Kwa siku. Je hii ni cheap? Warrant huwa haikavi uzembe kama huo wa kudondosha majiko chini
 
Wakuu kama thread inavojieleza either kulingana na uzoefu wako au umeskia ndugu jamaa wanasema tupate, mkombozi wa mapishi kwa umeme.

Induction cooker
View attachment 2905663

Multi Cooker
View attachment 2905665
Inategemea unataka kupika nini. Jiko langu liko kama kiwanda kidogo, kuna majiko ya aina tofauti tofauti yakiwemo umeme na ya gas kuweka kuhimili mapishi ya aina yoyote.
 
Tujifunze kuishi
1. Maharage hayapikwi masaa matatu, wala kuongeza maji mara nne
2. Mwanamke kukupeleka maji bafuni ya kuoga ni umaskini maji unatakiwa uyakute bafuni

Ngoja niishie hapa
Sasa kama mimi bado sijamudu kuishi hayo maisha, unataka niseme ninaishi hivyo?.
 
Halafu hizo induction cooker MOSFET yaani kipuli kinachochakata umeme kwenye inductor kikiungua ni mtihani matengenezo ni bahati nasibu
 
Sasa kama mimi bado sijamudu kuishi hayo maisha, unataka niseme ninaishi hivyo?.
Hayo ni maishaa ya kawaida sana kiongozi unapashwa kuishi wala si utajiri huo zaidi ya kufanya kazi kwa bidding yenye kupatia kipato na kuamua unataka uishi vipi
 
Mashine ya kufulia usiihofie, ninayo ya mchina Elekta, mwaka wa5.

Navaa na kurundika nguo kwa mwezi mzima ndiyo nakuja kuburuza.

Mzigo mkubwa sana nafua kwa unit 0.5.
Shukrani sana mkuu kwa ushauri, nitajipanga nipate moja.
 
Mkuu nina wasiwasi mmoja hivi hizo induction cooker zinaweza himili mchakamchaka wa mgandamizo wa sufuria wakati wa kupika ugali, make naona nyingi juu ni vioo.
Mkurya katika ubora wake… Bila kaugali maisha hayajaenda
 
Siyo sembe tu chief hadi chips zege na cake tunaivisha!.
 
Sasa wakubwa kwa uzoefu wako ipi ni brand bora ya Home appliances make sokoni kuna utitiri wa brand za mchina.
E.g Hisense, Evoli, West Point, Aborder, Sundar, Alitop, Itel n.k.
Samsung na LG sijazitaja make bei za vitu vyao na price to performance ratio ni mbingu na nchi.
 
Mi nacheka tu ulivyoandika pleasure
 
Kuna warabu wanauza wanatembeza majumbani ni nzuri sijalikariri jina ila kama vile wameandika Germany technology. Ninayo Pressure cook na microwave kutoka kwao mwaka sasa zinapiga mzigo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…