Wakuu hivi rafiki akifa ndani kwako Sheria inasemaje kuhusu hilo?

Wakuu hivi rafiki akifa ndani kwako Sheria inasemaje kuhusu hilo?

Ni shida, sababu jeshi letu huwa wavivu kuchunguza, hivyo wewe utawekwa ndani hadi uchunguzi utakapokamilika na wakajiridhisha kwamba hukuhusika na kifo chake; labda kama ukiwapa grease uchunguzi unaweza ukakamilika ndani ya masaa tu na ukaachiwa huru, hiyo ni kama huusiki kweli lakini...
 
Anza Mkuu unasubiri nini mpaka sasa,
Nikupe mfano kuna jirani mtu wa maji siku zote huchelewa kurudi kwake.

Alikuta mtu kaanguka mbele ya lango lake hakujua kama kafa ,na bila hivyo gari haiwezi pita ikabidi ashuke na mkwara mwingi ,akamvuta akamuweka pembeni.

Kesho yake kilichoendelea imekuwa ni hadithi mpaka leo, jamaa anasota mahabusu mwaka wa 2 sasa.
 
Heshima kwenu wakuu.

Naomba twende moja kwa moja kwenye mada tajwa hapo juu. Tuchukulie nina rafiki yangu amelala ndani kwangu then ikatokea bahati mbaya akafa akiwa usingizini, sheria inasemaje kuhusiana na hilo wakuu?

Naombeni muongozo tafadhali. Thanks.
Kwanza umemuua lini huyo rafiki yako, na unaishi maeneo gani hapa mjini?
 
Utakuwa saidia polisi kwa sababu:

1. Wewe ni mtu wa mwisho kuwa na marehemu kabla ya kifo chake.

2. Ni rafiki yako.

3. Amefia kwako

4. Yawezekana unajua chanzo cha kifo chake.

5. Yawezekana wewe ni muhusika wa kifo na au umeshiriki.

6. Kama chanzo cha kifo chake siyo ugonjwa, basi ni wewe, au unafahamu muhusika.

7. Wewe ndiye utatoa muelekeo wa mashahidi wengine mfano, majirani. Majirani wataulizwa kama walimuona mtu anaingia kwako, na je, walisikia sauti? Kishindo? Mabishano? Wataeleza pia tabia yako na Kama una urafiki kiasi gani na marehemu.

8. Utaulizwa nyendo za marehemu kabla ya kuja kwako, mlipitia wapi, alikueleza nini, nk.

9. Marehemu atafanyiwa vipimo ili kuoanisha maelezo na hali halisi ya mazingira ya kifo kama ni ugonjwa au kauawa. Kama kauawa, basi kazi inaendelea.

10. Kumbuka gheto/ nyumba yako itakuwa scene of crime kwa muda.

11. Upelelezi utaendelea na jalada likikamilika, litapelekwa kwa wanasheria wa Serikali huko litachambuliwa, Kama Kuna udhaifu wa ushahidi na au Kuna watu wanahitajika basi wanasheria watashauri.

12. Mpaka hapo, wanasheria watajua kati washukiwa ni nani anafaa kuwa mtuhumiwa yaani ambaye ushahidi unaelemea kwake. Hapo, kama ni wewe utashtakiwa.

13. Kumbuka, kwenye kuchambua ushahidi wanasheria hupima upepo, wanaangalia mfano, A akiwa mtuhumiwa na B akawa shahidi, hii kesi tutashinda?

Kwa mantiki hiyo, wewe unaweza ukawa shahidi namba moja au mtuhumiwa namba moja. Inategemea na legal opinion humo kwa DPP.

Cha msingi usiogope. Kuwa mtulivu usaidie polisi na Mahakama kutafuta haki jinai.
 
Hivi kwa mfano kama huyo mtu akawa njiani huko alikula kitu kisichofaa (poison) na safari yake ya mwisho ndio akaja "ghetto " na akarudisha namba. Uchunguzi ukionesha kuna viambata hatarishi mwilini mwake, je hali itakuwaje kwa mwenyeji?

NB: siku hizi watu wanabugia tu vitu hovyo hovyo barabarani, mara madawa ya asili, mara supu+juice na dawa nyinginezo na vinywaji nishati. Vitu hivi ni hatari sana kwa afya na vikimuondoa mtu lazima viache trace tatanishi.
Hapo ndo litakamilika lile neno la siyo Kila alie jela ana hatia yani kwa kifupi unafungwa
 
Tukio kama hilo likikutokea kimbiza maiti hospitali wao ndo wakueleze kuwa amekufa maana wewe huna vipimo vya kuhitimisha umauti. Mengine yatafuata baada ya kuambiwa kuwa amekwishakufa na wewe ukalia kwa kujitupa tupa ardhini. Unaweza kuepuka usumbufu mwingi sana kwa hako kaigizo.
 
Back
Top Bottom