Domhome
JF-Expert Member
- Jun 28, 2010
- 3,198
- 3,950
Kwa upelelezi wa kiduanzi wa polisi ya Tanzania, hapa nilazima usagiwe kunguni tu...Hivi kwa mfano kama huyo mtu akawa njiani huko alikula kitu kisichofaa (poison) na safari yake ya mwisho ndio akaja "ghetto " na akarudisha namba. Uchunguzi ukionesha kuna viambata hatarishi mwilini mwake, je hali itakuwaje kwa mwenyeji?
NB: siku hizi watu wanabugia tu vitu hovyo hovyo barabarani, mara madawa ya asili, mara supu+juice na dawa nyinginezo na vinywaji nishati. Vitu hivi ni hatari sana kwa afya na vikimuondoa mtu lazima viache trace tatanishi.