Utakuwa saidia polisi kwa sababu:
1. Wewe ni mtu wa mwisho kuwa na marehemu kabla ya kifo chake.
2. Ni rafiki yako.
3. Amefia kwako
4. Yawezekana unajua chanzo cha kifo chake.
5. Yawezekana wewe ni muhusika wa kifo na au umeshiriki.
6. Kama chanzo cha kifo chake siyo ugonjwa, basi ni wewe, au unafahamu muhusika.
7. Wewe ndiye utatoa muelekeo wa mashahidi wengine mfano, majirani. Majirani wataulizwa kama walimuona mtu anaingia kwako, na je, walisikia sauti? Kishindo? Mabishano? Wataeleza pia tabia yako na Kama una urafiki kiasi gani na marehemu.
8. Utaulizwa nyendo za marehemu kabla ya kuja kwako, mlipitia wapi, alikueleza nini, nk.
9. Marehemu atafanyiwa vipimo ili kuoanisha maelezo na hali halisi ya mazingira ya kifo kama ni ugonjwa au kauawa. Kama kauawa, basi kazi inaendelea.
10. Kumbuka gheto/ nyumba yako itakuwa scene of crime kwa muda.
11. Upelelezi utaendelea na jalada likikamilika, litapelekwa kwa wanasheria wa Serikali huko litachambuliwa, Kama Kuna udhaifu wa ushahidi na au Kuna watu wanahitajika basi wanasheria watashauri.
12. Mpaka hapo, wanasheria watajua kati washukiwa ni nani anafaa kuwa mtuhumiwa yaani ambaye ushahidi unaelemea kwake. Hapo, kama ni wewe utashtakiwa.
13. Kumbuka, kwenye kuchambua ushahidi wanasheria hupima upepo, wanaangalia mfano, A akiwa mtuhumiwa na B akawa shahidi, hii kesi tutashinda?
Kwa mantiki hiyo, wewe unaweza ukawa shahidi namba moja au mtuhumiwa namba moja. Inategemea na legal opinion humo kwa DPP.
Cha msingi usiogope. Kuwa mtulivu usaidie polisi na Mahakama kutafuta haki jinai.