Wakuu hivi rafiki akifa ndani kwako Sheria inasemaje kuhusu hilo?

Wakuu hivi rafiki akifa ndani kwako Sheria inasemaje kuhusu hilo?

Heshima kwenu wakuu.

Naomba twende moja kwa moja kwenye mada tajwa hapo juu. Tuchukulie nina rafiki yangu amelala ndani kwangu then ikatokea bahati mbaya akafa akiwa usingizini, sheria inasemaje kuhusiana na hilo wakuu?

Naombeni muongozo tafadhali. Thanks.
Umemuua nani kijana, sema tu hatuji kukukamata.
 
Tukio kama hilo likikutokea kimbiza maiti hospitali wao ndo wakueleze kuwa amekufa maana wewe huna vipimo vya kuhitimisha umauti. Mengine yatafuata baada ya kuambiwa kuwa amekwishakufa na wewe ukalia kwa kujitupa tupa ardhini. Unaweza kuepuka usumbufu mwingi sana kwa hako kaigizo.

[emoji3][emoji3]
 
Utatoa Ripoti kwa Viongozi wa Eneo Lako Then Wao Watakusaidia Kutoa Taarifa Polisi, watakuja kufanya upelelezi wao then Watampeleka Hospital Kufanyiwa Uchunguzi wa Kisayansi na Madaktari.

Ila Kumbuka Suspect wa Kwanza Ni Wewe
Hivyo Utasaidia Zoezi la Upelelezi Kukamilika.
Itakuwa Usumbufu Kidogo Itakubidi Kuvumilia.

Pia Tunakuaga na Tendency ya Kukaribisha Wageni Bila Kutoa Taarifa kwa Viongozi wa Mtaa, Au Kuhama Mtaa Flani Bila Kutoa Taarifa.
Umuhimu wa Kutoa Taarifa ndio Utauona Tukio Kama Hill Likitokea.

Wajuvi Zaidi Nawasubiri Nami Najifunza.
Na kanuni ya Jeshi la Police ni: "Don't trust any body" Hivyo nadhani unaelewa maana yake.
 
Hivi kwa mfano kama huyo mtu akawa njiani huko alikula kitu kisichofaa (poison) na safari yake ya mwisho ndio akaja "ghetto " na akarudisha namba. Uchunguzi ukionesha kuna viambata hatarishi mwilini mwake, je hali itakuwaje kwa mwenyeji?

NB: siku hizi watu wanabugia tu vitu hovyo hovyo barabarani, mara madawa ya asili, mara supu+juice na dawa nyinginezo na vinywaji nishati. Vitu hivi ni hatari sana kwa afya na vikimuondoa mtu lazima viache trace tatanishi.

Upelelezi utafanyika kujua uhusiano wako na marehemu Kama kulikuwa na ugomvi Kama ulikuwepo basi uwezekano wa kumpa sumu upo. Watakuhoji kwa kina. Yaani hapa kwenye mahojiano ndipo watakata mzizi wa fitina. Wale jamaa Wana ujuzi sana. Kama umehusika watajua tu kwenye majibu yako. Hata kama utakataa watajua unaficha ukweli.

Mbali na mbinu za mbinyo, mtu mwenye hatia akihojiwa huwa hawezi kuficha hisia za hatia. Hata iweje. Binadamu tumeumbwa kusema ukweli, ukisema uongo utajulikana tu.
 
Kama hakuna mwenye ushahidi kwamba alikuja kwako na una nyumba ya fensi na una gari, weka kwenye buti.. kuna misitu na mapori mengi ya kutupa.

Hiyo ndo njia 'salama' kuliko zote.

Otherwise, 'justice' system ya TZ 'itakushughulikia' kwenye 18 zake.
 
Rafiki kivipi lakini uchunguzi utafanyika na ukweli utajulikana. Kama ni natural death utaachwa huru, otherwise kifungo kitakuhusu depending whether it's murder or manslaughter
 
Ukipokea mgeni yoyote ni shart kutoa taarifa katika uongozi wa mtaa wako tatizo lolote litakalo tokea utakua mtuhumiwa wa kwanza wewe
 
Hizo zisikie tu, kuna kipindi nilikuwa nasikia "kusaidia polisi kufanya uchunguzi" nikawa najua na wewe unapewa vitendea kazi kama askari unaingia field kutafuta ushahidi, walivyonipiga pingu na makofi mawili matatu ndio akili ikaelewa maana yake halisi
 
mi dem wangu alizimia geto karibu masaa 6 haamki wala hahemi na moyo haudundi...!sitakaa nisahau nilivyopata wenge na akili kuruka.ikabidi niite washkaji na wakaingia geto dem yuko uchi kbs ili tushauriane cha kufanya.mwisho ilikuwa ni kusubiri ifike usiku wa manane tukamtupe.mungu mkubwa alivyopiga chafya tuu nilimbeba mgongoni adi kwao nikamshusha na uhusiano ukaisha.adi leo ikifika kuhusu kudinya nachkua logde room 2 yaani naenda kudinya afu narudi room kwangu.staki ujinga
 
Back
Top Bottom