Niache Nteseke
JF-Expert Member
- Apr 29, 2020
- 2,162
- 2,616
- Thread starter
- #121
Kwann umewaza mbali hivyo au yamekukuta nini
Daaaaah acha tu mkuu...! Kuna kitu kinaendelea nikasema niwaulize wakuu ili kujua tunaki-handle vipi mkuu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwann umewaza mbali hivyo au yamekukuta nini
Hahaha..?Huyo rafiki yako tayari kafia ghetto kwako au umeamua tu kuulizia
Chukua hiyo maiti ukaitupe mtoni kabla haijaanza kutoa harufu. Utakuja kunishukuru
huu ndo bonge la ushauri nmejikuta nmecheka sana walah[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Tukio kama hilo likikutokea kimbiza maiti hospitali wao ndo wakueleze kuwa amekufa maana wewe huna vipimo vya kuhitimisha umauti. Mengine yatafuata baada ya kuambiwa kuwa amekwishakufa na wewe ukalia kwa kujitupa tupa ardhini. Unaweza kuepuka usumbufu mwingi sana kwa hako kaigizo.
Kikubwa ni kumuomba MUNGU kila siku akuepusha na majaribu ya namna hiyo..
Inategemea aina ya mgeni.Mkuu wewe huwa unafanyaa hivo?? Kutoa taarifa kwa mjumbe kila upatapo mgeni??
Mkuu wakati mwingine bila igizo mambo yanakwama.huu ndo bonge la ushauri nmejikuta nmecheka sana walah[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Anza Mkuu unasubiri nini mpaka sasa,
Nikupe mfano kuna jirani mtu wa maji siku zote huchelewa kurudi kwake.
Alikuta mtu kaanguka mbele ya lango lake hakujua kama kafa ,na bila hivyo gari haiwezi pita ikabidi ashuke na mkwara mwingi ,akamvuta akamuweka pembeni.
Kesho yake kilichoendelea imekuwa ni hadithi mpaka leo, jamaa anasota mahabusu mwaka wa 2 sasa.
Utakuwa saidia polisi kwa sababu:
1. Wewe ni mtu wa mwisho kuwa na marehemu kabla ya kifo chake.
2. Ni rafiki yako.
3. Amefia kwako
4. Yawezekana unajua chanzo cha kifo chake.
5. Yawezekana wewe ni muhusika wa kifo na au umeshiriki.
6. Kama chanzo cha kifo chake siyo ugonjwa, basi ni wewe, au unafahamu muhusika.
7. Wewe ndiye utatoa muelekeo wa mashahidi wengine mfano, majirani. Majirani wataulizwa kama walimuona mtu anaingia kwako, na je, walisikia sauti? Kishindo? Mabishano? Wataeleza pia tabia yako na Kama una urafiki kiasi gani na marehemu.
8. Utaulizwa nyendo za marehemu kabla ya kuja kwako, mlipitia wapi, alikueleza nini, nk.
9. Marehemu atafanyiwa vipimo ili kuoanisha maelezo na hali halisi ya mazingira ya kifo kama ni ugonjwa au kauawa. Kama kauawa, basi kazi inaendelea.
10. Kumbuka gheto/ nyumba yako itakuwa scene of crime kwa muda.
11. Upelelezi utaendelea na jalada likikamilika, litapelekwa kwa wanasheria wa Serikali huko litachambuliwa, Kama Kuna udhaifu wa ushahidi na au Kuna watu wanahitajika basi wanasheria watashauri.
12. Mpaka hapo, wanasheria watajua kati washukiwa ni nani anafaa kuwa mtuhumiwa yaani ambaye ushahidi unaelemea kwake. Hapo, kama ni wewe utashtakiwa.
13. Kumbuka, kwenye kuchambua ushahidi wanasheria hupima upepo, wanaangalia mfano, A akiwa mtuhumiwa na B akawa shahidi, hii kesi tutashinda?
Kwa mantiki hiyo, wewe unaweza ukawa shahidi namba moja au mtuhumiwa namba moja. Inategemea na legal opinion humo kwa DPP.
Cha msingi usiogope. Kuwa mtulivu usaidie polisi na Mahakama kutafuta haki jinai.
Iwe iwavyo cha msingi hapo asiwe amekufa kwa kulazimisha kifo chake vinginevyo una kesi ya kujibu.
Kama umekamatia Dem akafa lodge au hotel,we sepa tu,Tena potea kabisa,Kama Ana smatifone chukua katupe chooni.
Tukio kama hilo likikutokea kimbiza maiti hospitali wao ndo wakueleze kuwa amekufa maana wewe huna vipimo vya kuhitimisha umauti. Mengine yatafuata baada ya kuambiwa kuwa amekwishakufa na wewe ukalia kwa kujitupa tupa ardhini. Unaweza kuepuka usumbufu mwingi sana kwa hako kaigizo.
Upelelezi utafanyika kujua uhusiano wako na marehemu Kama kulikuwa na ugomvi Kama ulikuwepo basi uwezekano wa kumpa sumu upo. Watakuhoji kwa kina. Yaani hapa kwenye mahojiano ndipo watakata mzizi wa fitina. Wale jamaa Wana ujuzi sana. Kama umehusika watajua tu kwenye majibu yako. Hata kama utakataa watajua unaficha ukweli.
Mbali na mbinu za mbinyo, mtu mwenye hatia akihojiwa huwa hawezi kuficha hisia za hatia. Hata iweje. Binadamu tumeumbwa kusema ukweli, ukisema uongo utajulikana tu.
Ila nako si kufungwa mpendwa..!!?
😂😂😂😂 Ila Kuna comments humu dah!!!
Ts the best option maana huwezi sema amekufa sababu kuna vigezo huangaliwa ili kusema mtu amekufa.Aisee inahitaji moyo kiongozi ila sidhani bado kama wataweza kukuacha kirahisi mkuu.
Hizo zisikie tu, kuna kipindi nilikuwa nasikia "kusaidia polisi kufanya uchunguzi" nikawa najua na wewe unapewa vitendea kazi kama askari unaingia field kutafuta ushahidi, walivyonipiga pingu na makofi mawili matatu ndio akili ikaelewa maana yake halisi
Kwa hiyo unahukumiwa kabla ya kuthibitika kuwa una kosa?Unafungwa jela maisha hadi hapo itakapothibitika huna kosa.